Pre GE2025 Makonda ataibuka aanze kuwananga watesi wake hawamuwezi, Sabaya atalamba teuzi. Tutahamia kwenye ubuyu mwingine, wameshajua ndio tulivyo!

Pre GE2025 Makonda ataibuka aanze kuwananga watesi wake hawamuwezi, Sabaya atalamba teuzi. Tutahamia kwenye ubuyu mwingine, wameshajua ndio tulivyo!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbona mtakoma safari hii
Sasa mnaambiwa SGR inahujumiwa na wanaopanda kwa buku
Halafu mtaambiwa faida ipatikane wapi kwa kukusanya buku buku muache kudandia bure
Ila kama mihogo ipo kuleni tu
Yaani ni upuuzi kila sehemu, halafu kuna watu wanapata ujasiri wa kuwa chawa sababu ya vichenchi anavyopewa!
 
Amechukuliwa na 'watu wasiyojulikana' nadhani ni wiki ya pili au tatu mpaka sasa, zishaanza kuzuka taarifa huenda ashafikishwa asipatikane mzima
Aisee anakutana na limtu kazi yake kutesa tu yaan kutesa ndio furaha yake akiona unatoboka unataka damu ndio anachekelea anakukata masikio huku anachekelea wakati huo Wewe unalia, kazi za laana kitengo cha mateso
 
Endeleeni kufuatilia propaganda za kijinga sisi tunaendelea kuchapa kazi za Ujenzi wa Taifa..
 
Yanga ndio haohao CCM
Yanga,Simba,Kagera Sugar n.k ni vilabu vya michezo nchini na vinashindana kutumia sheria 17 za mpira wa kandanda.

Na huku kwenye siasa za vyama vingi siasa ni mvuto kwa washabiki na wanachama wake.

Chukulia Gen Z huko Kenya iliokuwa inataka kukomesha unyonyaji unaongozwa na wanasiasa kutoka katika vyama vya siasa ambao wanajali zaidi matumbo yao.
Angalia jinsi Gen Z walivyoungwa mkono na lika zote.

Kwa hiyo ukiona watu wa Bongo hawashabikii sio wajinga.Siasa ni sera,na sera nzuri ni zile zenye nyenzo.

Ukiona watu wenye chama chao wao kwa wao wanavutana na wanapasuana tena mbele ya wapita njia ujue mle kuna walakini.

Hata Samsung ya Korea Kusini ikivulunda toleo fulani la bidhaa zake inafanya total recall wanateketeza hiyo bidhaa, wanarudi kwenye drwawing board kuunda bidhaa upya.
 
Wakuu wakati tunavuta mashuka nimeona nipite kidogo....

Wenye nchi wameshatujua, tunapenda umbea kuliko hata uhai, wanapiga mziki ule ule ambao tumezoea kuusikia na sisi bila hiyana hao rumba tunalisakata.

Sakata la sukari na Bashe jiii, bodi imetoa maelezo ya kipuuzi ndio imeisha hiyo.

Suala la binti wa Yombo, wamekamatwa vijana lakini mafia mwenyewe anafichwa fichwa, taratibuuu tushaanza kuachia.

Suala la watu kupotea hovyo, kariakoo vijana walikuwa wanachukuliwa akipatikana kashafika kwa Sir God, Sativa, Shadrack mpaka sasa hajulikani alipo, TLS imetoa list yake ya watu 83 waliotekwa, taratibu linaenda kuzimika.

Tumeletewa vya kutuzuga kwa muda; uteuzi na utenguzi, saivi kila sehemu ni kona ni Ummy na mwenzake aliyechukua nafasi hiyo mishipa ikitusimama kujadili alikotoa mganga wake🤦.

Huku Lissu kapokea mchango toka CCM, ni kutoka kwa wale wale anaowatuhumu kila siku kuwa watesi wao🤦.

Huo ni mwanzo tu, naona kuna bomu linakuja, na safari hii 'mama' atasepa na kijiji. Huku Makonda, kule Ole anarudishwa kwenye mfumo, mpaka tunakuja kushtuka kila kitu kimezikwa. Hao tunarudi kusubiri tuletewe kingine kama mazuzu.

Lini tutazinduka kwenye ujinga huu?

Wewe umechukua hatua gani, kiongozi?
 
Unadhani hizi drama zinawasaidia ccm na wananchi?? Au ni dilly dallying tactics za kipumbavu ili walaji wa nchi waendelee kuwa kwenye comfort zone!

Sidhani kama kuhairisha tumbo la kuhara kuliwahi msaidi mtu

Sisi wazalendo tutaendelea kudai! Tunataka katiba mpya
 
Back
Top Bottom