Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

INASIKITISHA sana serikali yaani TRA kumhujumu Makonda ili hali ni jasho la wana DIASPORA waliojitolea kwa ajili ya maendeleo ya wa Dar es salaam , watu wamejinyima ili kuletea watanzania maendeleo na sasa yanakwamishwa kwa sababu ya wivu sie wana diaspora mnatuvunja moyo kabisa .Tuanaomba kwa dhati Rais aingilie kati jambo hili kwa mstakabali wa maendeleo ya Mkoa wa Dar es salaam. Chonde Mheshimiwa Raisi tuko chini ya miguu yako tusaidiwe tumalize jambo hili mkoa wa Dar ufaidi matunda ya wana Diaspora.
Daaah nani sijui Dayaspora vile ndo mnavoitwa eeeh? Mmejitolea kwa moyo mkunjufu na pengine kujinyima mengi ili kutoa msaada kwa ndugu zenu veeeeeri guud. Sasa mko katika kazi nyingine kumbembeleza mhashimiwa Jiwe afanye jitihada kidogo ili msaada mlioutoa ufike kwa wasaidiwa. Naam serikali ya wanyonge na sikivu ambayo kwa bahati mbaya tu ikaweka vikwazo kwa wanyonge kufikiwa na misaada kutoka kwa ndugu zao dayaspora sijui nini nini huko, nadhani imesikia na mkuu wa malaika mtarajiwa baada ya nyie kuwa chini ya miguu yake atawezesha wasaidiwa kupata misaada waliosaidiwa na watoa msaada<
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana alifanya ibada maalum kanisani kwa ajili ya makontena yake yenye samani za shule yanayoshikiliwa na TRA

Katika ibada hiyo Makonda alionya watakao nunua makontena yake watapata laana kali

Pia aliwarushia dongo TRA akisema ni watu wabaya wasio na huruma na kudai kuwa wanamchukia Makonda

"Kama wanachukia Makonda waondoe nembo ya majina yangu kwenye makontena hayo" alisema Makonda

Ni mara nyingine viongozi wa serikali wanasuguana na taasisi za serikali katika kutekeleza majukumu yake huku kiongozi huyo wa mkoa akihisi anaonewa na ni wivu unaofanywa na TRA kisa anafanya vizuri katika mkoa wake

Juzi Paul Makonda alikaririwa na vyombo vya habari kuhusu kupigwa mnada makontena yake,akisema yeye hatishiki na ni mlima hawezi kuyumbishwa na wale wasiomtakia mema katika harakati zake za maendeleo ya Dar es salaam

Kwa hali ilivyo sasa ni dhahiri kuwa Makonda analaumu serikali kumhujumu na hakubaliani na TRA na mambo inayomfanyia

Sheria za kodi zinaeleweka consignee anaandikwa kwenye bill of lading na siyo kwenye mzigo husika. Hata ukivuta jina kwenye mzigodocuments zilizosafirisha mzigo zinatambua mmiliki halali wa mzigo ni yule aliyeandikwa kwenye bill of lading
 
Kwa sababu wameichimbia shimo nafsi yangu, njia yake na iwe giza na utelezi, malaika wa bwana akimfuatia kwa upanga, na wavu aliouweka umnase yeye mwenyewe.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka hata nassari ilibidi atumie fedha zake kulipia ambulance aliyonunua kwa ajili ya wananchi, imewatokea wengi sana hata kama ni kwa nia njema, sheria zimewekwa ili zifuatwe, ikikiukwa mara moja itakiukwa kila mara kukiwa na mfano hai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka hata nassari ilibidi atumie fedha zake kulipia ambulance aliyonunua kwa ajili ya wananchi, imewatokea wengi sana hata kama ni kwa nia njema, sheria zimewekwa ili zifuatwe, ikikiukwa mara moja itakiukwa kila mara kukiwa na mfano hai

Sent using Jamii Forums mobile app
Basi Makonda nae alipe kama sheria inavyotaka au wampe muda itakuwa jambo la busara zaidi, wanaagiza vya nini bila kujipanga? Ona sass wamekutana waziri wa mipango, Mpango
 
Lile Lori aliloleta boni kwaajili ya kuchakata uchafu kwa manispaa ya kinondoni toka ujerumani limekwama hadi leo, kwan lile halikuwa kwa manufaa ya wananchi? kama wizara na taasisi za serikali zinaagiza vitu nje na wakifika bandarini wanalipa Kodi, sasa yeye mtu binafsi anataka msamaha, akipewa huu msamaha, ntaamini yeye ni mkuu wa raisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie naona kama ni vifaa vya shule na Makonda alikusudia kuyasambaza mashuleni,washirikiane na TRA shule zipate vifaa.

Wakipiga mnada ina maanisha shule binafsi zitanufaika zaidi

[emoji252] [emoji479]
Tuanzie hapa kwanza kwani sheria za kodi zinasemaje??kwani yeye kabla ya kuagiza hizo samani alikuwa hajui utaratibu kuwa zikifika hapa kuna kodi itapaswa kulipwa??na tukisema kila mtu awe ana ingiza vitu kwa kingezo kuwa ni za mashule haitakuwa na afya ki kodi!!kwani yeye ndio wa kwanza kupigiwa mnada vitu vyake??kila siku vitu vinapigwa mnada !!hapa kuna kitu cha ziada
 
M
Kwan makonda ni nan hasa kias kwamba awanyime uhuru taasisi kubwa ya kiserikali kufanya kazi zake kwa uhuru?

Kuna mambo mengine viongoz Wetu wanafanya kias kwamba unajiuliza uyu mpaka leo anafanya nin kwann asipangiwe kazi nyingine ya kufanya au apigwe tuu chin..!!!!

Uyo jamaa kwa jinsi magu anavyo mlea ipo siku atakuja toa kauli za dhiaka kwa rais na uwongoz wake....

Sent using Jamii Forums mobile app
Makonda ni mtoto wa malaika na alishapewa kibali na baba yake apitishe bure huyu Dr mpango anajisumbua tu hana jeuri ya kubishana na ikulu na mwisho wa siku makontena hayatapigwa mnada,mwisho wa picha utakuja kuamini maneno yangu
 
Tuwekee picha ya hotel yake

group-of-people-sitting-outside-a-village-shop-in-kololi-in-the-gambia-ANNGBM.jpg
 
Back
Top Bottom