Capitano
JF-Expert Member
- Apr 7, 2011
- 1,959
- 1,633
Daaah nani sijui Dayaspora vile ndo mnavoitwa eeeh? Mmejitolea kwa moyo mkunjufu na pengine kujinyima mengi ili kutoa msaada kwa ndugu zenu veeeeeri guud. Sasa mko katika kazi nyingine kumbembeleza mhashimiwa Jiwe afanye jitihada kidogo ili msaada mlioutoa ufike kwa wasaidiwa. Naam serikali ya wanyonge na sikivu ambayo kwa bahati mbaya tu ikaweka vikwazo kwa wanyonge kufikiwa na misaada kutoka kwa ndugu zao dayaspora sijui nini nini huko, nadhani imesikia na mkuu wa malaika mtarajiwa baada ya nyie kuwa chini ya miguu yake atawezesha wasaidiwa kupata misaada waliosaidiwa na watoa msaada<INASIKITISHA sana serikali yaani TRA kumhujumu Makonda ili hali ni jasho la wana DIASPORA waliojitolea kwa ajili ya maendeleo ya wa Dar es salaam , watu wamejinyima ili kuletea watanzania maendeleo na sasa yanakwamishwa kwa sababu ya wivu sie wana diaspora mnatuvunja moyo kabisa .Tuanaomba kwa dhati Rais aingilie kati jambo hili kwa mstakabali wa maendeleo ya Mkoa wa Dar es salaam. Chonde Mheshimiwa Raisi tuko chini ya miguu yako tusaidiwe tumalize jambo hili mkoa wa Dar ufaidi matunda ya wana Diaspora.