Tumemsikia yule aliyekuwa Konda kwenye ile Kampuni ya mabasi awaku ile akimrushia lawama aliyekuwa Dereva.
Je, ametumia fasihi katika kumrushia lawama aliyekuwa dereva wake kwamba maovu yale yalifanywa na yule dereva ila lawama ma chuki akarushiwa yeye?
Je, Inawezekana huu ni mwendelezo ambao kila anayepewa nafasi ya kuhudumu kwenye kampuni hii ya sasa ya mabasi chini ya Dereva wake Mpya, amekuwa akijaribu kujitakasa kwa kumtumia lawama yule aliyekuwa Dereva wa mabasi ya kipindi kile.
Safari hii tumemsikia aliyekuwa Kindakta kipindi kile akisimama hadharani na kuamua kumtupia lawama aliyekuwa Dereva wake, ingawa lawama hizo amejaribu kutumia fasihi na tafsida kiasi kwamba wengi wanadhani anayelaumiwa ni Dereva kwa maana ya Dereva, ila kiuhalisia nianayerushiwa lawama na huyu Kondakta ni Dereva.
Masikini Dereva yule, mwisho wa siku hata waliomuwezesha kuipata ile ajira na wenyewe watamiana.