Pre GE2025 Makonda: Dereva wangu alikuwa anafunga namba za RC DSM na kutapeli watu

Pre GE2025 Makonda: Dereva wangu alikuwa anafunga namba za RC DSM na kutapeli watu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Bashite hawezi kukwepa mkono wa sheria. Labda aokolewe na kifo cha mapema. Omba uhai tu. Kwani Magufuli alijuwa angekufa kirahisi vile kwa namna alivyojifanya mungu mtu
 
Ndugu Lior je unayo elimu kidogo kuhusu sheria au umeandika kwa kuwa ulihitimu la Saba B? Kwenye jinai parties ni Republic ndiyo plaintiff na individual ndiyo defendant. Hakuna yeyote mwenye capacity ya kufungua shtaka la jinai dhidi ya Makonda mpaka kwa ruksa ya DPP
Yawezekana hata la 7 sijafika, niliishia la pili.
Uliwahi fata utaratibu wa kisheria DPP akakataa kukusikiliza? Au unamaanisha DPP ndio final stage?
 
Jana kwenye nyama choma aliyoandaa kwa Wakuu wa Mashirika Mjini Arusha, anasema alipokuwa RC Dar, wakati yeye yupo amepumzika ndani, Dereva wake alikuwa anakuja kuchukua gari kisha kuweka namba za RC Dar na bendera kisha kwenda kwa matajiri kuomba/ kuchukua fedha kwa jina lake.

My Take:
Huyu anatafuta kujisafisha tu, ila iko siku atatuambia alimficha wapi Roma na alimzika wapi Ben Saanane
Nyamitako mwongo sana hizo pigo alikuwa anapiga mwenyewe mfano hai ni ile ya GSM.
 
Jana kwenye nyama choma aliyoandaa kwa Wakuu wa Mashirika Mjini Arusha, anasema alipokuwa RC Dar, wakati yeye yupo amepumzika ndani, Dereva wake alikuwa anakuja kuchukua gari kisha kuweka namba za RC Dar na bendera kisha kwenda kwa matajiri kuomba/ kuchukua fedha kwa jina lake.

My Take:
Huyu anatafuta kujisafisha tu, ila iko siku atatuambia alimficha wapi Roma na alimzika wapi Ben Saanane
Madereva wengi wa ma rc, dc na wakurungezi wa mashirika ni usalama inamaana anasema watumishi waliopo usalama hawana maadili..TISS ebu fokeni huko mlipo tujue mbivu na mbichi..
 
Yawezekana hata la 7 sijafika, niliishia la pili.
Uliwahi fata utaratibu wa kisheria DPP akakataa kukusikiliza? Au unamaanisha DPP ndio final stage?
Nenda kafanye review ya kesi aliyofungua Wakili Madeleka dhidi ya mbunge Gekul aliyemuingiza Ally chupa mkundini. Ukishajua ilifika wapi njoo hapa unijibu
 
Nenda kafanye review ya kesi aliyofungua Wakili Madeleka dhidi ya mbunge Gekul aliyemuingiza Ally chupa mkundini. Ukishajua ilifika wapi njoo hapa unijibu
Na nikikujibu kuwa wewe ni mtu mwoga na muongo nitakosea ?
Kama madeleka alishindwa kwa kesi ambayo hakuna mauaji. Je wewe ambae una ushahidi wa kushuhudia hayo mauaji na hujachukua hata hatua yoyote huoni uoga wako?
 
Hapa kama kweli ndiye kasema, niuwongo wa kiwango cha juu kabisa. Aende sekretarieti ya maadili akiri utajiri alionao, na aeleze vyanzo vya kuupata.
Akamueleze nani wakati kiongozi mkuu alishawaruhusu kula kwa urefu wa kamba zao!?

Hiyo sekretarieti walioko ni hao hao kambale..hakuna wa kumnyooshea mwingine kidole.
 
Huyu jamaa zero sana na sasa hizo hela anazotapeli za kulipiwa gharama za hoteli milion 6 kwa siku na wafanyabiashara ni dereva wake anayelala huko hotelini?
 
Tumemsikia yule aliyekuwa Konda kwenye ile Kampuni ya mabasi awaku ile akimrushia lawama aliyekuwa Dereva.
Je, ametumia fasihi katika kumrushia lawama aliyekuwa dereva wake kwamba maovu yale yalifanywa na yule dereva ila lawama ma chuki akarushiwa yeye?

Je, Inawezekana huu ni mwendelezo ambao kila anayepewa nafasi ya kuhudumu kwenye kampuni hii ya sasa ya mabasi chini ya Dereva wake Mpya, amekuwa akijaribu kujitakasa kwa kumtumia lawama yule aliyekuwa Dereva wa mabasi ya kipindi kile.

Safari hii tumemsikia aliyekuwa Kondakta kipindi kile akisimama hadharani na kuamua kumtupia lawama aliyekuwa Dereva wake, ingawa lawama hizo amejaribu kutumia fasihi na tafsida kiasi kwamba wengi wanadhani anayelaumiwa ni Dereva kwa maana ya Dereva, ila kiuhalisia nianayerushiwa lawama na huyu Kondakta ni Dereva.
Masikini Dereva yule, mwisho wa siku hata waliomuwezesha kuipata ile ajira na wenyewe watamiana.
sema dereva yule usukani wake uli legea, ange kaza mikono wange kimbia seat
 
Jana kwenye nyama choma aliyoandaa kwa Wakuu wa Mashirika Mjini Arusha, anasema alipokuwa RC Dar, wakati yeye yupo amepumzika ndani, Dereva wake alikuwa anakuja kuchukua gari kisha kuweka namba za RC Dar na bendera kisha kwenda kwa matajiri kuomba/ kuchukua fedha kwa jina lake.

My Take:
Huyu anatafuta kujisafisha tu, ila iko siku atatuambia alimficha wapi Roma na alimzika wapi Ben Saanane
Hii story inafanana na story ya polisi [TANPOL] kukana kuhusika na matukio ya utekaji watu, kutesa na kuwaua na kisha kuwatupa misituni.......

Cha ajabu ni kuwa, kundi hili la ujambazi na ugaidi linatumia jina la TANPOL kufanya matukio haya ya uhalifu na mauji na polisi hawashituki wala kuchukua hatua yoyote ili kuwatia ktk mikono ya sheria watu hawa hatari kabisa ndani ya nchi yet, tafsiri yake rahisi kabisa ni kuwa POLISI WANADANGANYA. NI WAO NDIO WANAHUSIKA........!!

Kwa sababu jukumu kubwa la polisi kwa mujibu wa sheria na katiba ni KULINDA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO. Kwa polisi mpaka sasa kushindwa kulitia nguvuni kundi hili la kigaidi na ujambazi, ni wazi kuwa wanaukana wajibu wao huu muhimu wa kisheria na kikatiba......!

Je, wanastahili kuwepo na kuendelea kulipwa kwa kodi zetu na kutumia hovyo misaada ya wafadhili ya mabeberu wa Ulaya, America na Asia....?

Upande wa pili kuna huyu (PAUL MAKONDA a.k.a ALBERT BASHITE MALYANGILI). Yeye ktk kujivua kwake lawama anachukua mzigo wa lawama dhidi ya uhalifu, makosa na dhambi zake anamtwisha huyo anayemwita kuwa ni "dereva wake"......

Kama aliweza kugundua kuwa dereva wake hufanya ujambazi na uhalifu huo kwa kuji - "impersonate" kama RC wa DSM, tujiulize alichukua hatua gani huku yeye akiwa ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa DSM.? Kama hakuchukua hatua, tafsiri yake kama ilivyo kwa polisi, YEYE NDIYE ALIKUWA ANAMTUMA, YEYE NI MUHUSIKA KTK KILA UHALIFU HUO PAMOJA NA DEREVA WAKE NA KIKOSI CHAKE CHOTE. Asijaribu kupima intelligence yetu....!

Kwa upande wa pili, inashangaza kuwa hata wale waliokuwa wanamsikiliza akitema utumbo huu walikuwa wanachekelea na kumpigia makofi na bila shaka pale palikuwepo watu wasomi, wenye vyeo, na wenye akili timamu kabisaaa lakini wakakubali kumezeshwa utumbo na uchafu huu.....!!

Kwake yeye Makonda huku ni kuweweseka kulikofikia hatua ya juu kabisa kuelekea ktk uangamivu na mwisho wake. Shetani anamsereresha kidogo kidogo kuelekea mautini na kaburini kwake.......

Na anasikitisha na kushangaza sana kwa kukosa unyenyekevu mbele ya Mungu na badala yake ameruhusu kiburi kitawale nafsi na roho yake.......

Anachopaswa kufanya kuchukua hatua ya ujasiri, kwenda msalabani pa mwokozi Yesu Kristo na kwa Mungu Baba Mwenyezi atue mizigo yake ya dhambi na makosa yote aliyoibeba hapo. Huku ndiko kupona kwake......

Lakini huu ujanja janja wa kishetani hautamfikisha popote huyu jamaa badala atakufa kifo cha kijinga sana wakati ana fursa nzuri sasa ya kujiokoa mwenyewe....

Hatumhukumu Paul Makonda. Lakini tabia na mwenendo wake unathibitisha kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake tangu nyakati zile ni za kweli.......

Aombe rehema na neema ya Mungu ktk Kristo Yesu naye atapata amani na furaha tena.....
 
Jana kwenye nyama choma aliyoandaa kwa Wakuu wa Mashirika Mjini Arusha, anasema alipokuwa RC Dar, wakati yeye yupo amepumzika ndani, Dereva wake alikuwa anakuja kuchukua gari kisha kuweka namba za RC Dar na bendera kisha kwenda kwa matajiri kuomba/ kuchukua fedha kwa jina lake.

My Take:
Huyu anatafuta kujisafisha tu, ila iko siku atatuambia alimficha wapi Roma na alimzika wapi Ben Saanane
Kama hakuweza kumdhibiti dereva, ataweza vipi kuongoza mkoa?
 
Back
Top Bottom