Makonda huna mamlaka juu ya Mawaziri na Wakuu wa Mikoa

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
7,021
Reaction score
11,475
Umesikika katika hotuba yako ya leo kuwa utawarukia mawaziri na wakuu wa mikoa. Nakutahadharisha wewe ni kama Ahmed Ally wa Simba au Ali Kamwe wa Yanga, huna nguvu ya kujipangia unachotaka. Una ripoti kwa Katibu Mkuu, ndiyo anakupa kitu cha kuongea.
Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu huyu hakuna kikao cha CCM asichoshiriki kwa ngazi yoyote ile...yaani mauchafu yote ya CCM yanayopangwa kuhusu nchi hii yeye yumo na anahusika...

Hivyo anachokiongea anakijua na anajua mamlaka yake... sasa hivi yupo jikoni kabisa.


Unakumbuka Nape akiwa kwenye nafasi hiyo aliwahi kusema kuna Mawaziri mizigo, na baadhi ya mawaziri wakatumbuliwa.
 
Acha ujinga wewe unajua cheo cha katibu wa halmashauri kuu ya taifa itikadi na uenez??


NapitaKamaRadi
Lile jumba bovu la CCM sasa ndiyo limepata mtu wa kuanguka nalo. Hamna namna Samia ataweza kupindua kura za wananchi kama alivyofanya Dikteta Magufuli. Wakati wa UPINZANI kuchukua nchi unarejea
 
Baada ya kuwasema Mawaziri je ni nani aliweza kumvua Gamba? Si walimlenga Andrew Chenge? Je nini kilitokea?
 
Baada ya kuwasema Mawaziri je ni nani aliweza kumvua Gamba? Si walimlenga Andrew Chenge? Je nini kilitokea?
Mkuu hayo ni mswala ya ndani ya chama...lengo langu ilikuwa ni kuelezea mamlaka ama nafasi aliyonayo ndani chama kwa sasa.

Kumbuka hata bunge letu linaogopa zaidi chama kuliko serikali...

Makonda kwa sasa kuonana na Rais haitaji kibali ni simu moja tu.
 
Wakumbushe hao ma zwaza, Makonda piga kazi mpaka maji waite inya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…