Makonda: Marufuku kudai nyongeza ya mshahara! Nashangaa watu wanapita na mabango, mie ningewachapa

Nimegundua wewe una akili kubwa sana lakini umeamua kuzidumaza na kujifanya hamnazo sijui kwanini umeamua hivyo labda unanufaika kwa namna moja au nyingine ndiyo sababu uko hapa kucha kutwa kuwatetea hawa wahuni na mafisadi. Pole zako nyingi.

Nashukuru kaka nawe najua una akili kubwa.

Ila duh!!! kaka awamu hii unaita viongozi wetu wahuni na mafisadi...hii siikubali kwa kweli. Kama unawajua wataje weka na proof JPM awashughulikie.

Mengine juu yangu naona umeandika kwa sababu mimi na wewe hatupo upande mmoja...ila na wewe umebadilika sana tangu awamu hii ianze. Na pia upande wenu huo mawezana wenyewe na maneno yenu wengi wenu makali na machafu mnayowaita viongozi. Mimi siwezi kuwa hivyo, na naamini sana awamu hii inaenda mengi mazuri, kabla ambayo wengi tulifikiri tutayaona ndotoni tu.

Utafurahia tu siku moja na kulishangilia lori la Raisi wetu, bila kumsahau mpendwa Makonda.

Kabla sijasahau pale napoponda mengine ya viongozi wengine au hatua zao, awamu hii ninayoona haikuwa sawa mbona haunipi tano!? Nitakusubiria
 
Sio lazima mtu akutamkie wewe ni kijakazi wake lakini kauli zingine ni dharau kubwa sana na hii ni sawa na kukuona wewe kama kondoo kwamba hata akutamkie nini huwezi kumfanya kitu.

Haya matamshi ni ya kikoloni lakini sio ya kutolewa baada ya watu kujitawala.

Ipo siku atakuja na kauli mbaya kuliko hii ya kutaka kuchapa watu viboko kwasababu hakuna anaemkemea kila mtu yuko kimya.

Analelewa sana huyu na mtoto umleavyo ndivyo akauavyo.

Haya mambo yanawezekana hapa kwetu ila ingekuwa ni nchi nyingine kiingeeleweka.

Hata Wakenya wasingekubali

Alafu nyie viongozi wa dini ndio mnakaa meza moja na watu wa aina hii!!!
 
Watz tutulie tu. maana wakati ule wanasema "wacha waisome namba" Kuna 95% waliamini wao hayawahusu.
 
Bwana DAB Daudi Albert Bashite nafkiri Gwajima amesikia hilo la kuchapwa viboko,atakujibu jumapili,over
 
Kuna kila dalili kwamba viboko haviko mbali

Kuna kila dalili kwamba yule mkuu wa wilaya aliyefukuzwa kwa kuwacharaza walimu viboko atakumbukwa soon na kupewa madaraka

Kuna kila dalili kwamba yule mwalimu mwanafunzi wa kule mbeya sijui anaitwa msigwa nani vile...anaweza kulamba cheo soon

Wenye mikono myepesi wajiandae kulamba madaraka
 
TIBISII NDIO IMEKUWA KIMBILIO LAKE SASA HIVI AKITAKA KUUZA sura EE...KLAUZI WAMEMRUKA MITA 10000 [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimekwambia una akili kubwa sana lakini umeamua kuzidumaza. Pole zako labda iko siku utaamua kubadilika na kutumia akili zako vile ambavyo unastahili kuzitumia badala ya hivi ilivyo sasa, kukubali kuitumia akili ya vile ambavyo mtu A au B anataka uitumie.

Siku ukiwa huru kwenye matumizi ya akili yako nitakuwa wa kwanza kukupongezea na kukupigia makofi. Natumai hiyo siku haiko mbali sana.

 
Atakayedai nyongeza aweke kwanza vyeti hadharani - Bashite[emoji2]
 


Ila unaona navutiwa na lori la JPM, sijawahi kufatilia ya serikali kabla kama ninavyofanya awamu hii.

Kwa hiyo upande wenu huko kuja mmmmmh, labda sijui iweje. Au Mbowe aniachie kiti chake eeeeeeh unajua ni utani.... mnahitaji kiongozi kama JPM kuwaongeza.

Humu nitaendelea nilivyo, huyu ni Cocochanel...eeeh Bak kaa salama.
 
Reactions: BAK
Shukrani sana. Baada ya Kikwete niliamini hatatokea Rais mwingine mbovu zaidi kwenye utendaji kama yeye lakini baada ya miezi michache ya huyu dikteta uchwara nikagundua dhana yangu haikuwa sawa hata chembe na ndiyo kwanza mwaka mmoja tu sijui baada ya miaka mitano nchi yetu itakuwa katika hali gani. Usitegemee kuona lolote la maana kutoka sera MUFILISI, kudharau katiba na Bunge na maamuzi ya kukurupuka. Huko lori linakokwenda kuna giza nene sana, lori halina taa wala break na dreva haoni vizuri ana matatizo ya macho hivyo ni MAJANGA TU!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…