Makonda ni mpuuzi kama wapuuzi wengine tu na hatupaswi kumpuuza kwa upuuzi wake hata kama anatumwa

Makonda ni mpuuzi kama wapuuzi wengine tu na hatupaswi kumpuuza kwa upuuzi wake hata kama anatumwa

Chadema baadhi msipende kulialia kimama mawaziri,makocha watu mashuhuri wameugua korona na kutangazwa mtoto was mbowe imekuwa maajabu? Raid mnamdhihaki ninyi mkisemwa mnalialiaaa acheni upimbi. Zitto kuwa mshirikina so kawaida tuu mbona makonda alifoji vyeti na nikawaida!! Tupambanie vitu vya maana kama tunadaije time guru bila kukutana na siyo vimaneno vya kutoana relini
 
Hata kama Mbowe ni mwanasiasa, taarifa za ugonjwa wa mtoto wake hazikustahili kutoka hadharani. Yeye akiridhia zitolewe.
Makamanda ugonjwa huu mlikuwa mnashangilia ufike nchini imekuwaje mnataka Siri baada ya mtoto wa kamanda mmoja kupatwa na Corona mnataka siri?
 
Makamanda ugonjwa huu mlikuwa mnashangilia ufike nchini imekuwaje mnataka Siri baada ya mtoto wa kamanda mmoja kupatwa na Corona mnataka siri?
Mpaka ufike kwenye yale mawe ya Chamwino ndiyo tutajua imeingia corona Tanzania.
 
TUMSIKILIZE NANI WAZIRI MKUU AU MAKONDA?

Na Thadei Ole Mushi.

"Never Outshine your Master"

Hii ni law ya kwanza kabisa katika kitabu cha 48 Laws of power Kilichoandikwa na Robert Green.

Tafsiri yake kwa lugha ya mkoloni ni kuwa "With those above you, however, you must take a different approach, when it comes to power, outshining the master is perhaps the worst mistake of all."

Usije kufanya kosa hili hata siku moja kujiona unajua kuliko boss wako. Hata kama una akili kiasi gani hii ni kanuni kuwa jishushe na jifanye hujui kumzidi Boss wako. Yaani Boss wako akikuambia hii ni Blue wewe ukamwambia hii ni Nyekundu utajikuta matatizoni.

Kuna mtu aliyeitwa Gallileo huyu alikuwa mwanasayansi mbobezi na mwanahisabati. Aliwahi kugundua vitu vingi sana vya kisayansi kwa kuijua principle hii alijishusha na vitu vyote alivyogundua alivitunuku kwa Familia na Ukoo wa Medic ambao ulikuwa ukiitawala Italia kwa wakati ule.

Mtawala wa kipindi kile kutoka kwa ukoo huu wa Medic (Cosmos II) alifurahishwa sana na alivyokuwa anafanya Galileo na kumtunuku kuwa mwanafalasafa wa mahakama nchini Italia.

NATAKA KUSEMA NINI

Kauli ya Waziri mkuu kuhusu Corona Ni kwamba Kuna watu maalumu ambao watahusika na Utoaji wa taarifa zake. Leo mkuu wa Mkoa wa DSM kamwonyesha Waziri mkuu kuwa yupo juu yake kwa Mambo mengi Sana tu. Sidhani Kama Kuna mkuu wa Mkoa mwingine atakayethubutu kuita mikusanyiko na kuzungumzia Corona baada ya Tamko la Waziri mkuu. Labda nipo njee ya wakati je Waziri mkuu kashatengua kauli yake kuhusu wasemaji wa janga la Corona?...

Jamii inachukuliaje hali hii? Sijui ila Viongozi vijana Kuna Mambo ya kujifunza sana katika masuala mazima ya uongozi.

KUHUSU MBOWE NA CORONA.

Juzi nikiandika hapa kuwa Viongozi wa Sasa watambue kuwa jamii ya Sasa si ile aliyoongoza Nyerere, Mwinyi, Mkapa Wala JK. Hii Ni jamii nyingine kabisa yenye utofauti mkubwa mno na jamii zilizopita hivyo kudili nayo inatakiwa maarifa mapya kabisa.

Hebu tujiulize swali Moja tu case ya Kwanza ya Corona nchini ilitangazwa lini na muda gani? Nani aliyetangulia kutoa speech Kati ya Waziri Ummy Mwalimu na Mbowe? Sasa katika Hilo jamii hii yenye access ya Mambo mengi namna hii unaweza kuwadanganya na Fallacy information Kama hizi? Hata ambao alikuwa anawahutubia hapo stand huoni sura zao na kuelewa kuwa wanakuchora? Ipo wazi kuwa Mbowe alitangulia kutoa Speech kabla ya mgonjwa wa Corona hajatangazwa. Nakuuliza CCM yangu inajificha kwenye agenda ndogo Kama hizi?

Naamini sisi CCM tupo smart zaidi ya haya maigizo tunayofanya. Tunaweza kufanya makubwa zaidi ya haya.

Leo Narudia jalalani.

Ole Mushi
0712792602
 
Na juzi Rais alisema wenye mamlaka ya kutoa taarifa ya wagonjwa wa Corona lakini sijasikia Makonda au mkuu wa mkoa, na hapa serikali itakaa kimya lakini itokee Atangaze Mdee, au wewe uone moto wanaokuwashia! Nasisi sasa tutaabza kuwawashia moto
Huna madaraka subiri mwaka 3025
 
Makonda alikuwa anatoa mwongozo wa jinsi ya kujikinga na Corona Jambo ambalo kila kiongozi analifanya.

Mwezi uliopita Mbowe alitangaza mikutano ya siasa nchi nzima na kauli hiyo hakuifuta mpaka hiyo juzi. Ukisemacho juu ya kauli ya Mbowe ya kutangaza mikutano ilianza kabla ya kauli ya kutangazwa ugonjwa wa Corona Tanzania ni Cha kweli. Wengi tulitegemea kuona Mbowe anafuta kauli hiyo baada ya kuona hali imekuwa mbaya lakini hakufanya hivyo. Kwa Nini?

Hakufanya hivyo kwa sababu alikuwa na Nia ya kuendelea na mikutano licha ya hali mbaya kwa wengine lakini mtoto wake alivyougua tu akasitisha. Je, kiongozi wa namna hii anajali watu?

Alichofanya Makonda ni kuujulisha umma ambao walitaka kuandamanishwa na kukusanywa licha ya Corona, ikiwa na maana kwamba Mbowe alikuwa hajali hali za wengine. Kingine kauli ya Makonda haikuwa na maana ya kumdharau Mhe. Majaliwa ,ninachokiona ilikuwa na nia nzuri ya kuwatahadharisha watu kuepukana na wanasiasa wasiowajali lakini wanajali familia zao. Hiyo ni moja ya elimu muhimu watu wanayopaswa kuijua kipindi hiki Cha Corona.
 
Makamanda ugonjwa huu mlikuwa mnashangilia ufike nchini imekuwaje mnataka Siri baada ya mtoto wa kamanda mmoja kupatwa na Corona mnataka siri?
Wewe Said kumbe hujui ustaarabu kuna njia ya kumuelezea mgonjwa hata umauti kuna staa acha upumbavu
 
Back
Top Bottom