Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Nafikiri wengi tunakubaliana kwamba utoaji wa huduma za umma za watumishi katika sekta na maeneo mbalimbali una urasomu uliopitiliza, changamoto na usumbufu mkubwa sana. Kuna aina fulani ya uvivu, uzembe, wizi wa mali za umma na mazoea ambapo imekuwa kama utamaduni sasa katika watumishi wa umma.
Ushahidi mmojwapo mkubwa katika udhaifu mkubwa wa utumishi wa umma ambao umekuwepo kwa muda mrefu umekuwa ukipatikana katika ripoti mbalimbali ambazo zimekuwa zikitoa hali ya urahisi wa kufanya biashara barani Africa, mara nyingi zimetuweka nyuma ya Rwanda, Kenya na Uganda katika urahisi wa kufanya biashara.
Sasa mfumo anaotumia Makonda kufokeana na kuwakaripia kama watoto wadogo watumishi wa umma ni sahihi sana katika mazingira kama haya ila tatizo linaonekana kwamba hana "moral authority" ya kufanya hivyo kutokana na shutuma na tuhuma nyingi sana kubwa na ndogo na pia jinsi anvyoendesha mambo yake , chukulia mfano ufahari ambao mara zote umekuwa ukiambatana naye katika hii mikutano yake. Makando kando mengi ya Makonda na vinyongo vya baadhi ya wenzake ndio inafanya yeye kupata upinzani mkubwa anavyotekeleza mambo yake ila kama angekuwa anafanya hivi mtu kama Dotto Biteko wala kusingekuwa na shida au kelele nyingi.