Makontena 115 ya sukari iliyofichwa yakamatwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Makonda

Makontena 115 ya sukari iliyofichwa yakamatwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amebaini sukari zaidi ya makontena 115 iliyofichwa kwenye bandari kavu ya PMP, Mkuu wa Mkoa ametoa taarifa kuwa kuna zaidi ya Makontena 162 na sio 115 kama ilivyoripotiwa hivyo ameagiza zoezi la ukaguzi wa sukari liendelee kwenye Bandari kavu hiyo.
kwa maono yangu madogo na kielimu changu cha kubabaisha nadhani sasa ifike muda sasa hizi public stunt zinabidi kupunguzwa nadhani hii ni serikali ya kazi tu..lets promote good working conditions kuliko kuchafuliana majina nadhani wengi waliamini watu wanaficha sukari lakini hao polisi na TRA( ambao ndio serikali) wanaoshughulikia suala hilo wanapingana..nadhani kabla ya kutangaza sukari imefichwa lazima serikali iulize na ichunguze kwanini ana hifadhi sukari nyingi na kama kweli haiuzi..
nadhani tukiacha siasa na public stunt na kufanya kazi kwa bidii lazima yatafichuka mengi sana,
 
Ubaya wa Hizi ni Kama Bongo Muvi...Hazina Consistency Nzuri!
Kama Wanafanya Kutusahaulisha LUGUMI,Well and Good!Marofa wa Chache Labda!Every Action Has Its Reaction...Sasa Kama Hivi Muvi ya Sukari Ililenga Hilo,Imefanya Mazuri Kwa Watazamaji Kuliko Watazamwa!:
a)Imetuongezea Dharau Wapinzani Dhidi ya Serikali...Tulicho Kitegemea Kwa Huyu ni Tofauti na Tukionacho
b)Wamew ongezea meno wapinzani!kuna kipindi nilihofu kasi ya jpm itaua upinzani,ila Sukari imeni prove wrong!
c)Acha Tuanze Kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 naona badala yakuzi tafuta,Magufuli anatupa mwenyewe wapinzani!
 
kwa maono yangu madogo na kielimu changu cha kubabaisha nadhani sasa ifike muda sasa hizi public stunt zinabidi kupunguzwa nadhani hii ni serikali ya kazi tu..lets promote good working conditions kuliko kuchafuliana majina nadhani wengi waliamini watu wanaficha sukari lakini hao polisi na TRA( ambao ndio serikali) wanaoshughulikia suala hilo wanapingana..nadhani kabla ya kutangaza sukari imefichwa lazima serikali iulize na ichunguze kwanini ana hifadhi sukari nyingi na kama kweli haiuzi..
nadhani tukiacha siasa na public stunt na kufanya kazi kwa bidii lazima yatafichuka mengi sana,
wakisubiria uchunguzi,ukweli utakuwa hadharani,na unafikiri nyago watauza?
 
wakisubiria uchunguzi,ukweli utakuwa hadharani,na unafikiri nyago watauza?
ahahaa ahaa haaa.....sasa huku kuuza nyago wakati mzigo upo sehemu inayokuwa controlled na serikali nakusema imekutwa kutawatoa jasho siku moja watakuja kumlipa mtu fidia kubwa sana...nakuanza kutumbuana wenyewe kwa wenyewe
 
Watakamata hadi sukari inayoenda Zambia au Rwanda ,halafu watasema ilifichwa kumbe ilikuwa kwenye mchakato wa kusafirishwa.

Serikali iache kufanyia kazi kwa mizuka.
Halafu tutakuja lalamika nchi jirani zinaacha safirisha mizigo yake bandari zetu, tusiingilie kazi za watu sio kila sukari inayoletwa ya wizi au imefichwa zingine zinaenda nchi jirani.
 
hahahahahaha...eti imefichwa bandarini....hawa wakuu wa mikoa hawana hata JD...leo president akifanya hili na wao haooooo.....mkumbo....this is very very dangerous
ni mwendo wa kufatisha kiitikio Mkuu,1,2,3...... haya twendeeee!!
 
Afanye fasta kusajili haki miliki kwny huo ugunduzi kabla mwingine hajamuwai.
 
Wauze wakti inapita kwenda Nchi zingine. Ni transit Good hiyo. Kama hujui maana yake GOOGLE
Ni njia ya kukwepa kodi tu, kama hujui mi najua zaidi yako. Haiendi kokote, na kama huamini fuatilia.
 
Wazungu sasa hivi wapo wanagundua Ma virus na ma ant-virus, Makonda anagundua sukari iliyo hifadhiwaa? Sukari aliyoigundua mwisho wa siku tutaambiwa ni ile ambayo serikali iliangiza
 
Binafsi ninaposikia kauli kutoka upande wa mfanyabiashara kuwa "sukari ilikuwa transit" siwezi kuamini moja kwa moja kwa kuzingatia historia. Kwani mara ngapi tumesikia wafanyabiashara wakidai mzigo fulani (mafuta etc) kuwa unakwenda nchi jirani kumbe wakifika Kibaha mzigo unashushwa na kuuzwa humu humu nchini?

Hapa sana sana kilichotokea ni hao kina Zakaria walikuwa kwenye mchakato wa kukwepa kodi kwa kusingizia kuwa mzigo uko transit au ni kwa ajili ya kutengenezea juice nk. Na kwa hili TRA ndiyo inatakiwa wabanwe vizuri kwanza.
 
Ile ishu Paul Makonda aliumbuka pale yule mzee wa ki Islam alipomjibu kuwa, "nimenunua hii sukari kwa ajili ya kwenda kutoa sadaka"

Paul Makonda ikabidi abadili kosa, sasa anamlaumu yule mzee wa ki Islam kwa kuweka sukari ghorofa ya 6 katika nyumba isiyoisha.

Jamani, tani 4 ni sawa na 4,000kg
4000kg * 2000 Tshs = 8,000,000 Tshs

Wakati mwingine watu wawe wanatumia akili, sio kutaka kick kwa 8mil. Waende huko kwenye migodi ya Barrick ambapo kuna upotevu wa mabilioni.
Akhsante mkuu kwa mrejesho
 
Hayo itakuwa serikali ndiyo imeyaficha, washtakiwe. Maana bandari kavu zipo chini ya usimamizi wa idara za serikali.

Afadhali wewe umeamua kuunganisha kichwa chako na kiwili wili!

Kuna wenzio huko upande wa pili (Lumumba) vichwa vilishatengana na kiwiliwili cha mwili, wanafyatuka tu!!
 
Huh kiukweli hawa watu wanatutania
Kesho utasikia mmiliki anajitokeza
 
Back
Top Bottom