Makosa ya Hayati Magufuli hayasahihishiki

Makosa ya Hayati Magufuli hayasahihishiki

Hata tundu lisu hajui mpaka sasa kwamba dishi limeyumba japo tunamwambia kila siku. Kama wewe uko tofauti naye basi changanya na zako
Mawazo yako wewe mwenyewe huyaelewi. Ni kama mtu mwenye matatizo ya uoni wa rangi ( Color Blind ) halafu anataka kuwabishia watu wanaomuelezea utofauti wa rangi nyekundu na bluu kwenye shati lake.
 
Kosa kubwa kufanywa magufuli ni kutaka kuua upinzani alisahau kua upinzani ni wanainchi na ukigombana na wanainchi hapo unaingia kwenye ugomvi WA moja kwa moja Na MUNGU
Nadhani wakti wa Magufuli upinzania ulikuwa na nguvu ila ukawa unaelekeza nguvu hizo kusikohusika; kwa mfano kwenda kufanya fujo gerezani au kupinga mambo kwa data za kufikirika. Sasa hivi ndiyo hamna upinzani kabisa.
 
Mstaarab ni mstaarab tu. Mtumia mabavu hawezi kuwa mstaarabu hata siku moja.
kwani yule kiwete anaelelewa ubeligiji aliambiwa mara ngapi aache kumdhihaki raisi,😂😂😂!? How many times na mahakamani alifikishwa kwa maonyo. Ila mwisho alivuna alichokipanda.

Nakumbuka kuisikia hii kauli morw than 1 time.. "Muda wa kampeni za kisiasa umeisha mniache nifanye kazi"

Ila yule mbwiga akaona kumletea maneno ya kanga raisi ni mchezo..Magufuli ni dikteta uchwara tu, alichokitafuta alikipata lakini.
 
Acha ushoga wewe, Magufuli alitumia bunduki ipi usinilishe maneno ntakuchenjia mda sio mrefu...Mama wewe
Kwa kweli matumizi ya Bunduki katika kuendesha mambo ni jambo baya sana. Ni dalili ya udhaifu wa kiuongozi.
 
Hayo ni mawazo yako tu.
Mwelekeo ulikuwa ndio huo. Ule mfano wa "Msaliti huwa anafanywa nini" wengi bado tunaukumbuka.

Damu ya mwanadamu ikimwagika Ardhini huwa haiendi bure bali hulia mbele ya kiti cha enzi cha MUNGU.
 
Upinzani wa tz ni dhaifu sana!

Fikiria mtu yuko belgiji mwingine canada mwingine ameungana na ccm kuramba asali ili kumkomoa marehemu alafu 2025 utaona wanahaha wakitegemea nao watashinda
[emoji23][emoji23][emoji23]
Hujui kitu kabisa yaani !!
 
Kwa watu wenye fikra fupi kama mkia wa mbuzi mtaona yote aliyofanya Magufuli ni makosa tu. Ila kwa watu wenye upeo wa hali ya juu wanaelewa how strategic that nigga was.

Jamaa hakupenda siasa za kinafiki na uzanidiki na focus yake ilikuwa ni kuleta maendeleo ya haraka sana hakutaka mambo ya kujivuta na siasa za chokochoko ndio maana aliwafyeka mikia wajinga wajinga wote waliokatiza katika anga zake.

As opposed watanzania wengi walizoea kubembelezwa kutekeleza majukumu yao ila kipindi cha huyo mzee watu waliwajibika ipasavyo sababu walijua anytime mtaa unaweza ukakupokea kwa fedhea kubwa. Ilikuwa bahati mbaya kwa wenye vyeti feki pia sababu watu wote waliokuwa wanaishi kimagumashi walitubu [emoji23][emoji23][emoji23] na hawa ndio miongoni mwa waombolezaji wengi ambao walikuwa wanashangilia kifo cha mwamba na kuspin mabandiko ya kipuuzi kila kukicha humu.
Leo yuko wapi ? unajua kwanini ?
 
Nadhani wakti wa Magufuli upinzania ulikuwa na nguvu ila ukawa unaelekeza nguvu hizo kusikohusika; kwa mfano kwenda kufanya fujo gerezani au kupinga mambo kwa data za kufikirika. Sasa hivi ndiyo hamna upinzani kabisa.
Huo uzushi wa kusikohusika umeutoa wapi ?
 
SGR kwanza siyo teknolojia bali ni upana wa Reli. Treni za umeme zilikuwapo hata kabla ya kuja kwa reli za SGR. Na hoja ya kuongezeka kwa ufanisi kwa kuwa reli imekuwa ni SGR siyo kweli. Ufanisi hauletwi kwa kuwa na reli pana bali ubora wa menejimenti.

Haya ya bei ya umeme kuwa rahisi kwa kuwa unazalishwa kwa maji (Hydroelectricity) ni ya uongo. Gharama za umeme zinakokotolewa kutokana na mambo mengi sana.
Mkuu hongera na pole. Unabishana na watu mnaopishana sana IQ na wenye fixed mindset. Hamtakaa mkubaliane kitu.

Kwa mtazamo wangu mimi Magufuli alikuwa “matokeo” tu ya janga au msiba wa mfumo fyongo wa CCM ambao bado tunao unaoendelea kulitesa taifa hili. Hakika alikuwa kielelezo kikali sana cha jinsi tulivyowezesha utawala wa kiimla (tyrannical rule) nchini. Kama hatukujifunza pale ole wetu huko mbeleni. The future will be really bleak.

Utaona hata utawala wa sasa hauko tayari kufagia mabaya yote ya awamu ya tano. Wanabakiza kidogo yale yaliyo na “manufaa” kwa CCM na serikali yake; yanaoupa utawala mkono wa chuma dhidi ya wananchi. Wasiojuwa wanafikiri waathirika ni “wapinzani” tu bila kujiuliza hao wapinzani ni kina nani hasa?

Nyerere naye alipokuwa nje ya madaraka, alilalamika hivyo hivyo kwa awamu ya pili kama vile si yeye aliyeliumba hilo zimwi: eti “wameacha mazuri yetu wamekumbatia makosa tuliyofanya. Udikteta umeongezeka. Rushwa imekithiri. Haki za binadamu zinachezewa chezewa tu!…
 
Mkuu hongera na pole. Unabishana na watu mnaopishana sana IQ na wenye fixed mindset. Hamtakaa mkubaliane kitu.

Kwa mtazamo wangu mimi Magufuli alikuwa “matokeo” tu ya janga au msiba wa mfumo fyongo wa CCM ambao bado tunao unaoendelea kulitesa taifa hili. Hakika alikuwa kielelezo kikali sana cha jinsi tulivyowezesha utawala wa kiimla (tyrannical rule) nchini. Kama hatukujifunza pale ole wetu huko mbeleni. The future will be really bleak.

Utaona hata utawala wa sasa hauko tayari kufagia mabaya yote ya awamu ya tano. Wanabakiza kidogo yale yaliyo na “manufaa” kwa CCM na serikali yake; yanaoupa utawala mkono wa chuma dhidi ya wananchi. Wasiojuwa wanafikiri waathirika ni “wapinzani” bila kujiuliza wapinzani ni kina nani hasa?

Nyerere naye alipokuwa nje ya madaraka, alilalamika hivyo hivyo kwa awamu ya pili kama vile si yeye aliyeliumba hilo zimwi: eti wameacha mazuri yetu wamekumbatia makosa tuliyofanya. Udikteta umeongezeka. Rushwa imekithiri. Haki za binadamu zinachezewa chezewa tu!…
Ni kweli jamaa ana akili kubwa mno lakini anabishana na watu duni sana !
 
Kuna fikra za baadhi ya watu wanaotamani itokee siku moja "makosa" ya kimtazamo na kiutendaji ya Hayati John Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tano wa serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania YAREKEBISHWE.

Kiuhalisia makosa hayo hayawezi kurekebishwa kwa kuwa umbali aliotufikisha Magufuli inakuwa ngumu sana kurudi kwenye njia sahihi kiurahisi. Kitu pekee kinachoweza kufanyika ni kusuluhisha mitazamo yetu na uhalisia wa mambo.

Kwa mfano; chuki kati ya wafuasi wake na wale waliokuwa wanaipinga falsafa yake ya undeshaji nchi inarekebishwaje? Jee watu waliodhurika wakati wa utawala wake wanaponaje ama wale waliopotea wanapatikanaje? Leo hii hawa kina Ben Saanane, Simon Kanguye, Azor Gwanda nani anajua walipo na inawezekana wakarudishwa kwa familia zao. Lissu na wengine waliopata ulemavu zama hizo maisha yao yanaweza kurejerezwa?

Nani mwenye akili timamu anayeweza kusimamisha ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere kwa hatua ililofikia. Au SGR inawezaje kuwachwa wakati tayari mabilioni ya shilingi yameteketea kwenye mradi huo tayari. Nani ataruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa wakati CCM amri ya marufuku hiyo haiwahusu?​

Suluhisho ni nchi kugawanyika. Wanaotaka kiongozi kama Magufuli wakae upande mmoja na wasiotaka wakae upande mwingine. Taifa likishaanza kugawanyika kifalsafa haliwezi kubaki pamoja kwa amani. Vietnam iligawanyika Kusini na Kaskazini kila upande na kiongozi wa falsafa tofauti, Korea nayo iligawanyika Kusini na Kaskazin kwa namna hiyo hiyo.
 
Baba wa hivyo ni mzuri sana!

Kuliko kutumbua minyama, bora ujibane ule makande kila siku ili ujenge vitegauchumi vitakavyowasaidia watoto baadae ambavyo vitakuja kuwafanya wale minyama miaka yote hapa duniani
Ndio mawazo yako yameishia hapo?
Ina maana huna uhakika wa kupata kipato kila siku ili uumie leo kwa njaa kwa ajili ya kesho?
Hao watoto tunaowaachia hawana elimu baada ya miaka mi5 wameshakua ombaomba😂😂😂
 
Back
Top Bottom