Maktaba ya Utalii

Maktaba ya Utalii

Funa the Wild

Senior Member
Joined
Aug 1, 2022
Posts
167
Reaction score
282
Utalii wa Majini
Miongoni mwa maeneo ambayo utaweza kufanya utalii wa majini na nchi kavu basi hifadhi ya taifa Saadan ni miongoni mwa hifadhi ambayo inaweza kukupatia utalii wa aina iyo.

Hifadhi hii ipo mkoa wa Tanga nchini Tanzania. Ni hifadhi ambayo utafahamu mambo mbali mbali yanayohusiana na Kasa/Sea turtles wanaopatikana ndani ya bahari ya hindi katika eneo la hifadhi ya Saadan. Miongoni mwa kasa wanaopatikana ndani ya hifadhi iyo ni pamoja na,

Sea Green turtles/Kasa wa kijani
KASA WA KIJANI (Sea Green turtle/chelonia mydas)........ KWA NINI HUITWA KASA WA KIJANI??.....

e890ee46939318a46e950076d73997ed(1).png

Asilimia kubwa ya walio wengi huwa wanapata ugumu wa kutofautisha KASA na KOBE kitu kinachofanya kuzidi kuwa na maswali mengi juu ya hawa viumbe wawili kiuhalisia kuna tofauti kubwa japo wote wanapatikana kwenye familia Moja.

Duniani kuna aina mbalimbali za KASA na wanatabia tofauti tofauti, Tanzania ni mwiongoni mwa nchi zilizojaaliwa kuwa na KASA. Wanapatikana kwenye bahari ya hindi. Kwa Tanzania, hupatikana Tanga kwenye hifadhi ya Taifa SAADAN. Pia hupatikana kwenye visiwa vya MAFIA.

KASA WA KIJANI NI NANI??
KASA wa kijani ni kasa wa pili kwa ukubwa Duniani hupatikana bahari ya hindi, huzaliwa na urefu wa millimita 30 na huzeeka na urefu wa Mita 1.5 na uzito wa kilo 400. Ana magamba 13 mgongoni na mawili (2) kichwani. Hutaga mayai kuanzia 80 hadi 150 kwa mda mmoja.

KASA WA KIJANI chakula chake kikubwa ni mimea inayopatikana chini ya bahari kitaalamu inaitwa Sea grasses.

KWANINI HUITWA KASA WA KIJANI??
Huitwa Kasa wa kijani kutokana na aina ya chakula anchokula (mimea inayopatikana chini ya bahari/sea grasses). Anapokula mimea hii, hutengeneza rangi ya kijani kwenye mafuta yanayopotikana ndani ya mwili wa kasa.
 
Tanzania tuna vitu vizuri sana vya kujivunia kama taifa
 
Utalii wa milimani.
Ukiachilia mbali hifadhi ya taifa ya Mikumi na Uzdungwa basi safu za milima Uluguru ni miongoni mwa maeneo ambayo shughuli za ki utalii zinapamba moto sana.

Uluguru Mountains/Milima Uluguru (Eastern Arc Mountains).
Milima Uluguru hupatikana Tanzania katika mji wa Morogoro. Kuna aina 12 za milima tofali katika ukanda wa Afrika mashariki milima Uluguru ndiyo milima tofali mirefu zaidi kuliko milima tofali mingine. Ina urefu wa mita zisizopungua 2600 kutoka usawa wa bahari.

Milima hii ni miongoni mwa milima inayotumika kama hifadhi ya viumbe ambavyo vipo katika hatari ya kutoweka kutokana na shughuli mbalimbali za kibanadamu kitaalamu maeneo kama hayo hufahamika kama

Biodiversity hotspots.
Milima hii ni chanzo cha maji ya mto Ruvu unaosambaza maji yake katika maeneo ya Kibaha na jiji la Dar es salaam. Pia kwa wakazi wa Morogoro huwa wanapata maji kutoka kwenye safu za milima iyo.

Upekee wa Mlima Uluguru.
Unaweza ukashangaa lakini huo ndiyo uhalisia. Ivi unajua kwamba kuna baadhi ya viumbe vinapatikana eneo moja tu ulimwenguni kote na huvikuti maeneo mengine..!!

Ndani ya safu za milima Uluguru kuna jamii ya ndege hufahamika kama Uluguru Bush Shrike. Hii ni jamii ya ndege inayopatikana ndani ya safu za milima Uluguru pekee na hutoikuta maeneo mengine duniani kote kitaalamu huitwa Endemic Species (Viumbe wanaopatikana eneo moja pekee na hawapatikani maeneo mengine) . Imeitwa ilo jina kutokana na eneo ambalo hupatikana ndege uyo.

0db45d6c2c597a330163719df2b96d59.png

Mbali na uwepo wa ndege hao. Pia kuna shughuli mbalimbali za utalii huwa zinafanyika, kama kupanda milima, kutembelea maporomoko ya maji mfano Choma, Hululu. Kutembelea makazi ya wajerumani waliokuwa wakiishi miaka ya nyuma na njia walizopita, Kutembelea kanisa la wajerumani, kuona mawio na machweo, kupunga upepo na kutuliza mawazo. Kutembelea makazi ya chief wa waluguru wa kumi na tano aliyefahamika kwa jina la Chief Kingalu.
 
View attachment 2312719

ASANTE KWA TAARIFA NZURI YA UTALII
 
72f685f076f7330f04b5c6a2cb3c9e9d.png

Saltwater Crocodiles, Hawa ni mamba wanaopatikana zaidi Asia na Australia. Ni mamba wanaoishi kwenye maji chumvi na ni wakubwa kuliko mamba wote duniani wana kilo 1000kg. Si kawaida hapa kwetu Africa kuwa na aina ya mamba wanaoishi kwenye maji chumvi lakini kwa Tanzania utawakuta mamba wa aina iyo.

Mto Wami ni miongoni mwa mito inayomwaga maji yake bahari ya hindi. Mto huu umekatiza ndani ya hifadhi ta taifa Saadani ikiwa ndani yake kuna viumbe kama Mamba, Samaki na Viboko.

Kipindi cha kupwa (Kupungua) na kujaa (Kuongezeka) kwa maji ya bahari. Maji bahari yakiongezeka huchanganyikana na maji ya mto Wami na kusababisha mchanganyiko wa maji Chumvi(Bahari) na maji yasiyo chumvi (mto).

Mwendelezo wa kitendo icho hupelekea maji ya mto kuwa chumvi na mamba wanaoishi ndani ya mto kuzoea mazingira ya maji chumvi (Adaptation).
 
View attachment 2313786

asante kwa taarifa chief
 
"Mlima wa Mungu" (Ol Doinyo Lengai).

6675e41f2198db1a968b552fd6a98a85.png

Ol doinyo Lengai ni neno la kimasai likimaanisha "Mlima wa Mungu". Mlima huu unapatikana kaskazini mwa nchi ya Tanzania katika mkoa wa Arusha mwishoni mwa upande wa mashariki mwa ziwa Natron.

Ni miongoni mwa milima yenye volcano iliyo hai (Active Volcano). Una mita za urefu zisizopungua 2900. Mlima huu una aina ya lava inayofahamika kama "Carbonatitic" ambapo ndani yake kuna kiwango kikubwa cha madini ya Sodium na Calcium. Na kiwango kidogo na Silica.

Kwa nini huitwa Mlima wa Mungu?
Wamasai hutumia mlima huu kama sehemu ya ibada. Hufanya ibada kwenye mlima huo ili kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili ikiwemo matatizo ya uzazi.
 
Nakumbuka kuna mwaka tulip8ta hapo na ATC anga lilikuwa dusty sana pilot akatangaza kuwa mlima Oldonyo Lengai umelipuka volcano
 
Back
Top Bottom