A
Anonymous
Guest
Jana nilipigiwa simu na mke wangu nikapewa taarifa kwamba mama yangu amekamatwa Buza kwa Lulenge na jiji kwenye eneo lisiloruhusiwa kufanya biashara, japo hapakuwa hata na uthibitisho kwamba anauza bidhaa yoyote. Wakawachukua na baadhi, wengine waliokamatwa wamechukuliwa pesa zao na wengine waliambiwa watoe pesa ili waachiwe, na wakatoa.
Baada ya hapo wakaanza kuzunguka nao; mara wanawapeleka Kituo cha Buza Polisi, haipiti dakika kumi unasikia wamepelekwa kituo kingine. Kuanzia saa 11 jioni mpaka saa 3 usiku ndipo wakawapeleka Kituo cha Mbagala Maturubai. Mama yangu alikua amefungwa jana Alhamisi. Wakasema hawawezi kuongea chochote wala kutoa dhamana, wakatuambia tuje leo.
Wakati nipo njiani naelekea kituoni, nikapigiwa simu kwamba wamepelekwa Halmashauri ya Temeke, hapa karibu na Uwanja wa Taifa. Tumefika hapa tunaambiwa tulipe laki 3 ndio atoke.
Watu wamehoji ni makosa gani yamepelekea kukamatwa. Wengine wametumwa kutoa hela kwa Wakala na wamekamatwa, wengine wameenda kuchukua watoto shule, kakutwa kasimama pia kakamatwa. Walichojibu ni kwamba wanawaamini sana vijana wao kwa sababu wamewapa mafunzo na hakuna maongezi kwenye hilo. Yaani hata kama utatoa taarifa ngazi ya juu, hakuna msaada utakao patikana.
Ndo tuko tunapambana hapa, kila mmoja amtoe ndugu yake.