Askofu ana haki binafsi ya kuelezea msimamo wake wa kisiasa, lakini msimamo wake si kwa niaba ya KKKT.Vinginevyo, kwa wadhifa au uongozi alionao atashindwa kutoa angalizo kwa Serikali inapotenda yasiyo haki. Binafsi mimi nilishtuka siku moja JPM akiwa Rais, Askofu alimsimamisha Makonda asalimie waumini Kanisani pale Azania. Ndiyo ilikuwa siku ya kwanza kwangu kulazimishwa kumsikiliza Makonda. Niliishiwa nguvu mwilini. Kilichonishangaza ni kama kweli Askofu alikuwa hana taarifa za usanii, ubambikizaji makosa watu, ukiukaji wa sheria wa wakati huo, mambo ambayo kijana huyu alikuwa anayafanya hadharani lakini akampa heshima ya kuitwa mbele ya Kanisa ambayo kwangu ilikuwa kama kumsafisha au kuunga mkono mambo ambayo kijana huyu alikuwa anayafanya kinyume kabisa na maadili ya Ukuu wa Mkoa. Hayo ndiyo Askofu itabidi atenganishe kati ya utashi wake binafsi na Kanisa! Hadithi ya Askofu Shoo kuwe mbwa mzee inabidi ajifunze michezo mipya ndiyo kama hiyo. Vinginevyo ninamwombea Baba Askofu Malasusa uongozi mzuri uliotukuka.