Pre GE2025 Malasusa hakuanza leo kuwa mwana CCM, alishajitenga na dini akabakia kwenye siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu;

Malasusa anapotoka makusudi kwa kusema maandamano ni machafuko. Kama kiongozi wa dini na mlinzi wa amani anatakiwa kuwa neutral kwenye maswala ya siasa.

Hapaswi kuiongoza serikali jinsi na nguvu gani itumie kukabiliana na maandamano ya amani na haki kwa kutoa tafsiri ya uongo.

Malasusa anafahamu fika kuwa maandamano mengi kama sio yote nchini yamekuwa yakiharibika baada ya polisi kuingilia waandamanaji badala ya kuwalinda!

Askofu inaonekana hajui na wala haguswi na umaskini au ufukara wa waumini wake! Yamkini hata bei ya Sukari, mafuta na athari ya umeme havimuathiri ama kwa sababu vinalipiwa na sadaka za waumini ambao wapo hoi bin taban au kwa asali anayolambishwa na serikali kama kada na shushu!

Kama kweli ni Askofu mwenye hofu ya Mungu asimame kama wazee wa imani mathalan Jeremiah, Musa, Eliya na kadhalika!

Malasusa achague kuwa askofu Mkuu wa waumini wake masikini au Askofu wa chama tawala, CCM!
 
Huyo ni mamluki
Mkuu;

Shida ipo pale ambapo askofu Mkuu wa Kanisa kubwa anaposema uongo wa wazi tena Kanisani mbele ya Kamera, mchana kweupe kuwa maandamano ni machafuko! Je usiku atasema uongo kiasi gani???

Jambo ambalo sio kweli. Anapoashiria kuwa maandamano ni kinyume cha sheria au ni uvunjifu wa amani. Maandamano ni halali kwa mujibu wa katiba yetu. Kwanini atake kuyaharamisha Kanisani kinyume na sheria???

Ina maana hajui kuwa waumini wake wote waliokuwa Kanisani wameandamana kwenda kwenye ibaada kutoa mashtaka dhidi shetani! Je, hajui makutano ya Kanisani ni maandamano ya kukataa dhuluma ya shetani??? Je maandamano hayo ya imani nayo ni machafuko???

Asipotoshe watanzania!
 
Kashashikwa sana ugoni huyo, nashangaa walomchagua.
 
Dk Shoo alikuwa anashinda sebuleni kwa Mbowe asubuhi mpaka jioni, waumini wanamsubiri kanisani hawamuoni hata wiki mbili.

Jioni Mbowe anachukua hata milioni mbili tatu za ruzuku, anampa
 
Kanikera sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mnavyomshambulia Dkt Malasusa mnathibitisha KKT ya Dkt Shoo ilikuwa ya wachaga per se. Yaani nyie mmeshindwa kabisa kuzuia hisia zenu.
 
Reactions: Tui
Ni pamoja na kuikosoa pale inapo bidi siyo kuisifia sifia tu
 
Mkuu hapo ulipo nani kakushikia bunduki ili uwe Chadema, acha uongo, kimsingi wewe ndiye unaye hubiri na kueneza uongo na chuki.
Itoshe tu kumuita ni mnafiki mkubwa
 
Fanyeni maandamano dhidi ya Askofu. Wajinga wakubwa mtu asipokubaliana na ujinga wenu lazima mmtukane na kumkejeli.
Tuliza kidonda chako mzee,maana mchezo huu kamwe hauhitaji hasira
 
Aisee watu mmejaliwa kipaji cha kupangilia jambo na likaeleweka.
 
Dk Shoo alikuwa anashinda sebuleni kwa Mbowe asubuhi mpaka jioni, waumini wanamsubiri kanisani hawamuoni hata wiki mbili.

Jioni Mbowe anachukua hata milioni mbili tatu za ruzuku, anampa
Naona umepatikana maana kila ngonjera unazoanzisha watu wanaziponda tu dadeeeekiiii[emoji1787][emoji1787]
 
Maccm yamefurahi sana hii dini ya KKKT kuwa na wapuuzi wao akina Malasuso?
 
Mkuu

Mkuu ni vitu vingapi Mwenyekiti wa CCM Kawapa watu mbali mbali zikiwemo taasisi za dini? Waliopewa naye wazirudishe?
Uchungu wa mtoa bandiko dhidi ya malasusa kuiunga mkono serikali kumenifanya nichokoze nyuki kwa mbali, tena kwenye kajambo kadogo kama haka unakokajibu wewe......

Askofu Dr. Shoo was a darling of Chadema katika uongozi wake wote politically speaking, hiyo haikua tatizo right?

Kuna tatizo gani Askofu Dr Malasusa kuwa darling wa serikali ya CCM right now?

Au ndio ile mkuki kwa ngurue kwa binadamu mchungu
 
Reactions: Tui
Rudia kusoma ulichoadika labda utakifanyia editing
Mzee Askofu shoo kapewa li v8 la kisasa na Chadema kwa mgongo wa chairman Taifa,

Unataka mie ninywe sumu badala niendelee kumuona Dr. Shoo akila maisha huku, wewe na wenzie mkichukia Malasusa kuiunga mkono Serikali
 
Reactions: Tui
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…