Mizania
JF-Expert Member
- May 17, 2023
- 3,812
- 3,277
Mkuu;Askofu ana haki binafsi ya kuelezea msimamo wake wa kisiasa, lakini msimamo wake si kwa niaba ya KKKT.Vinginevyo, kwa wadhifa au uongozi alionao atashindwa kutoa angalizo kwa Serikali inapotenda yasiyo haki. Binafsi mimi nilishtuka siku moja JPM akiwa Rais, Askofu alimsimamisha Makonda asalimie waumini Kanisani pale Azania. Ndiyo ilikuwa siku ya kwanza kwangu kulazimishwa kumsikiliza Makonda. Niliishiwa nguvu mwilini. Kilichonishangaza ni kama kweli Askofu alikuwa hana taarifa za usanii, ubambikizaji makosa watu, ukiukaji wa sheria wa wakati huo, mambo ambayo kijana huyu alikuwa anayafanya hadharani lakini akampa heshima ya kuitwa mbele ya Kanisa ambayo kwangu ilikuwa kama kumsafisha au kuunga mkono mambo ambayo kijana huyu alikuwa anayafanya kinyume kabisa na maadili ya Ukuu wa Mkoa. Hayo ndiyo Askofu itabidi atenganishe kati ya utashi wake binafsi na Kanisa! Hadithi ya Askofu Shoo kuwe mbwa mzee inabidi ajifunze michezo mipya ndiyo kama hiyo. Vinginevyo ninamwombea Baba Askofu Malasusa uongozi mzuri uliotukuka.
Malasusa anapotoka makusudi kwa kusema maandamano ni machafuko. Kama kiongozi wa dini na mlinzi wa amani anatakiwa kuwa neutral kwenye maswala ya siasa.
Hapaswi kuiongoza serikali jinsi na nguvu gani itumie kukabiliana na maandamano ya amani na haki kwa kutoa tafsiri ya uongo.
Malasusa anafahamu fika kuwa maandamano mengi kama sio yote nchini yamekuwa yakiharibika baada ya polisi kuingilia waandamanaji badala ya kuwalinda!
Askofu inaonekana hajui na wala haguswi na umaskini au ufukara wa waumini wake! Yamkini hata bei ya Sukari, mafuta na athari ya umeme havimuathiri ama kwa sababu vinalipiwa na sadaka za waumini ambao wapo hoi bin taban au kwa asali anayolambishwa na serikali kama kada na shushu!
Kama kweli ni Askofu mwenye hofu ya Mungu asimame kama wazee wa imani mathalan Jeremiah, Musa, Eliya na kadhalika!
Malasusa achague kuwa askofu Mkuu wa waumini wake masikini au Askofu wa chama tawala, CCM!