Malawi: Mahakama ya Katiba yabatilisha matokeo ya Uchaguzi wa Urais wa nchi hiyo uliofanyika Mei 21 mwaka 2019

Malawi: Mahakama ya Katiba yabatilisha matokeo ya Uchaguzi wa Urais wa nchi hiyo uliofanyika Mei 21 mwaka 2019

Wewe jamaa sikuelewagi aisee,
Juzi kati hapa ulikua ukilalamikia bodi ya mikop HESLB, leo uko Kenya!!!

Bro utakua unanifananisha, nitafute nini kwenye bodi ya mikopo.
 
Katiba hazifanani.... yatupasa kupigania katiba mpya kwanza kabla ya kuwaza hizi chaguzi za kiini macho.
 
Nimetafakari sana juu ya mfumo wa chaguzi zetu hasa uchaguz mkuu. Kwamba hakna kuupinga mahakamani..hata kama wananchi wamepokwa mamlaka yao juu ya viongozi walowachagua. Je, kwanini sasa bunge lisjifunze toka Malawi uchaguzi upingwe mahakamani.?

Hawa wenzetu wamepinga matokeo ya uchaguzi mahakamani kwa Amani Bila vurugu. Na uchaguz unaenda kurudiwa!! Je Taifa letu linashindwa nini kuexercise ustaarabu huu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama inaweza tumika kuhalalisha Matokeo. Uchaguzi ukirudiwa msishangae Rais aliyepo Madarakani na Ambaye ushindi wake umebatilishwa akarejea Ikulu Kiulaini Sana.

Haya yalishatokea hata Kenya. Pia ninajiuliza iweje Watu 3 TU wapewe mamlaka kuamua hatima ya mamilioni ya Wapiga kura Nchini Malawi?

Suala la Gharama nalo linatazamwaje ukichukulia kuwa Malawi Ni nchi masikini sana?
 
Kenyan,

Mkuu hii ni TAMU zaidi:

"Chilima ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa rais Mutharika yeye alipata asiliamia 20.2 ya kura nae akidai uchaguzi haukuwa huru na uligubikwa na dosari nyingi, matamshi yaliyoungwa mkono na waangalizi wa kimataifa isipokuwa wale kutoka umoja wa Afrika."

Hata Jaji Lubuva alikuwa karidhika kabisa na matokeo yaliyotenguliwa baadaye na Mahakama ya Kenya.

Ama kweli mamlaka za Africa zimerogwa. Hata hivyo walafi nyie wa madaraka mwisho wenu waja. Siku ya siku hakika mtawajibishwa - 'you shall be held to account.'
 
Mahakama za tanzania ni ujanja ujanja tu,,,hakuna haki..zinaongozwa na serikali ya maccm,ndio shida..nchi zingine mfumo wa mahakama unajitegemea kimaamuzi,

Njaa (mayala) baba!
 
Mahakama za tanzania ni ujanja ujanja tu,,,hakuna haki..zinaongozwa na serikali ya maccm,ndio shida..nchi zingine mfumo wa mahakama unajitegemea kimaamuzi,
Tz mazingaombwe ebu angalia chaguzi serikali za mitaa yaani mpaka unajiuliza kama kweli sisi Tanzania ni watu kweli au misukule?! Hakuna cha mahakama, bunge, tume au hata serikali wote utazani miroboti imekuwa programmed kufanya ujinga jinga yaani taabu tu!!
 
safi sana...hii ni Signal alert kwa viongozi wa TANZANIA toka cha tawala...... wakati umefika sasa wanapaswa kubadilika... kama wasipo badilika basi wakati uta wabadilisha wao
 
Nawaza mwandishi wa hii twiti yuko kwenye hali gani?
Vyombo vyetu vya ujasusi vilishindwa kumtonya uchaguzi huo una rafu za kutosha??
Hatukuwa na mwakilishi kama muangalizi wa kimataifa??

Cc Chakaza imhotep jingalao
 
Back
Top Bottom