Malawi wameweza, Tanzania tunafuatia

Malawi wameweza, Tanzania tunafuatia

Atakwambia ni lumumba chini ya mwalimu chakubanga
Chuo kikuu gani ulisoma Politica Science na mimi nitume application mkuu. Maana anona unweka very nice substances / material hapa jamvini.
Hongera sana kwa ufahamu murua kabisa.
 
Mgombea wa Chama Kikuu cha Upinzani Nchini Malawi (MCP) Dr. Lazarus Chakwera anaongoza kura kwa zaidi ya 60% dhidi ya Prof. Peter Mutharika anayetakiwa kuondoka Ikulu ya Malawi wakati wowote kuanzia sasa.

Hatua hii ni baada ya Mahakama kutengua Ushindi wa hujuma uliofanywa na Serikali ya Chama tawala cha DPP chini ya Prof. Peter Mutharika anayeondolewa Ikulu.

Malawi wamemaliza Kazi yao!

Muda ni hakimu mzuri, watanzania tujiandae kuyapokea mageuzi ya kiuongozi.
Ni ngumu kwa taifa lililojaa wajinga na mang'ombe
 
Hayo maneno yanafaa kutamkwa na mtu aliye kata tamaa ya maisha
Ni Jambo jema kama Upinzani utaibuka Mshindi huko, ila kuyafananisha ya Malawi na Tanzania ni Kumfananisha Lionel Messi na Ditram Nchimbi.
 
Hao ni wananchi wa Malawi wakiongozwa na jeshi la nchi hiyo kwenye maandamano nchini Malawi
IMG_20200625_165810.jpeg
 
Sasa hiyo 1% ni yupo huyo?
1% are enjoying national cake [emoji513]

Elimu ya bongo imewajengea wengi ujinga na unafiki mkubwa Sana + uswahili uliopo huko ndio mtasubiri sana ........

Solution mngedai katiba ile ya mzee warioba kwa pamoja mpk kieleweke 2018 April mngekinukisha kweli msingekuwa hapo, mnaendeshwa na maamuzi ya mtu 1
 
Bila Tume huru nakatiba mpya hiyo itabaki ndoto za mchana jamani.
 
Ebu tutolee ushamba na kuramba viatu
Kwani Chadema huwa hamuweki mawakala? Mbona mlipata wabunge zaidi ya sabini? Na hao mawakala si huwa wanalinda na kusimamia kura cha Chadema. Sasa nani ataiba kura wakati kila chama kina wakala.
 
Ni kweli. Malawi wana independent judiciary, jeshi neutral na wananchi wanaojielewa. Matokeo yanaruhusiwa kupingwa mahakamani. Kwa kweli Malawi kuna demokrasia kubwa sana. Malawi polisi siyo ya chama tawala. Ni ya wananchi. Hiyo ni tofauti kubwa kati ya Malawi na Tanzania.
 
Kama ingekuwa tunafanya kila kitu kwenye mitandao ya kijamii basi tungekuwa tushaitoa ccm kitambo.
 
Mgombea wa Chama Kikuu cha Upinzani Nchini Malawi (MCP) Dr. Lazarus Chakwera anaongoza kura kwa zaidi ya 60% dhidi ya Prof. Peter Mutharika anayetakiwa kuondoka Ikulu ya Malawi wakati wowote kuanzia sasa.

Hatua hii ni baada ya Mahakama kutengua Ushindi wa hujuma uliofanywa na Serikali ya Chama tawala cha DPP chini ya Prof. Peter Mutharika anayeondolewa Ikulu.

Malawi wamemaliza Kazi yao!

Muda ni hakimu mzuri, watanzania tujiandae kuyapokea mageuzi ya kiuongozi.
Lakini ukumbuke MCP kilikuwa chama tawala hadi wakati wa Dr Kamuzu Banda. Kinarudi madakarakani kwa mara ya 2.
 
Back
Top Bottom