Wakuu salaam!
Mwaka 2020 Nimeamua na nimedhamiria kuacha mambo haya:
1. Pombe
2. Umalaya
3. Ku-bet
Hii combination inafanya natumia zaidi ya laki 6 kwa mwezi wakati kipato changu ni chini ya 500k, najikuta katika madeni ya kijinga kijinga.
Nimedhamiria kumrejea Muumba, yaani kwa dhambi nilizotenda na nilizonazo natamani hata nisali Dini zote!
MARRY X MASS & HAPPY NEW YEAR IN ADVANCE
NB: MNIWEKE KATIKA MAOMBI
Una mipango mizuri ambayo itakutoa hapo ulipo na kukupeleka hatua nyingi sana mbele.
Mimi nilishaweza kutoka hapo no2, ila nikarudi tena,nikatoka tena,halafu nikarudi tena tena. Ila baadaye nikaweza kutoka mazima. Ni jambo ambalo lazima nikiri halikuwa rahisi.ninachoweza kusema Mungu mwenyewe alinishindia baada ya kumuomba msaada wa Roho Mtakatifu through maombi ya nguvu na ya kufunga.
Nilichofanya nikapata muda mwafaka wa kutafakari kwa nini vitu vya kijinga kama hivyo vinifarakanishe na Mungu wangu.kwamba niukose uzima wa milele kwa vistarehe ambavyo hata hivyo vina ni-cost financially na psycologically.
Labda ni kwambie, ni hivi utakavyotangaza kuacha uzinzi na mambo hayo yote uliyodhamilia,umetangaza vita na ufalme wa giza, atakurudishia fursa nyingi kutenda uovu. utashangaa.yaani wale wasichana uliwahi watongoza zamani wakakutosa watakutafuta wenyewe,walio kuacha wemyewe ukiwa bado unawapenda utakuta wanarudi wenyewe kukuomba msamaha ili muendelee.Kama kuna mtu ulikuwa unapata vikwazo vya kumpata utashangaa vikwazo vinayeyuka vyenyewe.inakuwa easy kumpata.
Sasa ukishatangaza hiyo vita,ujue unahitaji usaidizi wa Mungu haraka,
Nenda sehemu unapodhani wanamwabudu Mungu wa kweli kajiungamanishe hapo( Ingawa hata hapo pia unaweza pata vishawishi vya kukurudisha nyuma)
2.Jisemee moyoni mwako na kinywani mwako kwa kumaanisha kwamba umeenda hapo kupata msadaa wa kufunguliwa ktk vifungo vya dhambi(maana hivyo ni vifungo)
3.Hudhuria Ibada na uwashuhudie hao wote ambao ni marafiki zako wa zamani kwamba wewe umekata shauri,umeamua kuacha dhambi
4.Tafuta marafiki wengine wapya wanaoamini (kuwa makini hapa pia,kwa sababu wapo wanaoonekana wanaamini,kumbe ni machoni tuu)
5.Hudhuria vipindi vya ibada katikati ya wiki,pata mafundisho sahihi ya kukujenga kiimani ,sima neno la Mungu kila wakati,usisubiri jumapili tuu,sababu utapoa
6.Badilisha utaratibu wa familia yako,kwa kumweka Mungu mbele.Anza kumuweka mkeo na watoto wako karibu zaidi(sababu watakutia moyo) jitahidi katika matembezi yako uwe na mkeo kama ikiwezekana.
7.Endelea kuichukia hiyo tabia mbaya,penda kulinda huo uaminifu utakaokuwa umesha utengeneza baada ya kuwambia washikaji zako na max wako kwamba wewe umeshaacha hayo mambo.
8.Fanya yote haya kwa kumaanisha,kama ni mkristo endelea kulitumania jina La YESU,sababu linayo nguvu ya ajabu sana
Lastly,maisha yako yatabadilika mpaka kila mtu atakushangaa.uchumi wako utaimarika sana,sababu utakuwa umebarikiwa
Narudia tena,kuacha mambo hayo na mengineyanayofanana na hayo si jambo rahisi Ila pia ni jambo linalowezekana,kata shauri kwa faida yako mwenyewe.