Malengo yangu mwaka 2021 ni kuacha pombe, umalaya na ku-bet

Nakusudia kuacha kama wewe lakini naona muda ambao nilikuwa natumia kunywa pombe, umalaya na kubet nitakuwa nafanya nini ili nisiviweke kwenye ratiba
Jiunge ma gym uwe unafanya mazoezi, soma vitabu, tafuta vitu ama passion mpya ya kujifunza iwe kupiga gitaa, kinanda, drums, nk.
 
Sinywi pombe, sitembei na malaya, sibet wala sivuti sigara, unataka kuniambia sijakamilisha maisha? Tuache kutukuza haya mambo bhana.

Ulevi, umalaya na kubet kunaharibu maisha ya vijana wengi sana sasa hivi, wanatumikishwa bila kujijua. Jana kuna kijana kaja ofisini akanambia amekunywa dawa fulani saa tano asubuhi, anaweza kunywa pombe? Aliponitajia jina la dawa nikamwambia asubiri mpaka masaa 48 yapite akafadhaika sana, baada ya nusu saa akarudi anataka kujua madhara akiamua kunywa tu, nikamwambia kama umechoka kuishi kanywe.

Acheni umalaya

Acheni kubet

Acheni pombe

Hazina faida kwenu zaidi ya kuwatia hasara tu.
 
Hongera sana mkuu
 
Mwaka 2020 ndiyo unaisha soon...mwakani unampangi gani mazee?
 
nakubaliana nawe kwa hoja ya tabia zako binafs uko sawa na unaishi kwa tahadhari. lakin ukubali kuwa ulivyo leo ni matokeo ya vitu vitatu muhim; GENES, MALEZI, NAFAS YAKO KATIKA JAMII. usiishangae hobby au starehe HALALI ya mtu ambayo ni kero kwako. nasisitiza tu kuwa na kias katika kila jambo. umetoa mfano wa mtu aliyekwisha vuka mstari wa ukawaida! ameshakuwa addicted, ni mgonjwa tayari. binadam wote na heka heka zote hizi tunatafuta jambo moja tu lile lile - FURAHA. lakin haijawai kuwa na rangi moja.
 
Mm ni muumini.wa namba 2 ila haini shida sana kwasababu kuona nimeonga 10000 ujue huyo mtu anakaribia kua mke kabisa kwahiyo wanao lialia na namba 2 ni wavivu wa kutongoza wanakimbilia kuhonga na kuishia kufirisika. Kuna mdada unamaproach asubui hujafika nyumbani anataka pesa ya simu na kulipia chumba pumbav kwangu ninacheka na kunywa maji ili nilale. Usitawaliwe na tamaa mtu haelewek anataka pesa acha na vumilia utampata ambaye anauhitaji kama wako.
 
Mi kuacha tu bila kuweka matangazo, hii kuweka matangazo hutafanikiwa asilani, mimi nilikuwa natangaza kuacha pombe na umalaya lakini najikuta ndio nimeharibu kabisa bora mwaka ulioisha.

Ila baadaye niliacha kimya kimya, kaenye pombe nipunguza kwa asilia 60

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mwanachuo katika ubora wako....sasa huyo jamaa hajaelewa umesema nini
 
Siyo kweli. Mtu akiamua, huwa ameamua; labda kama hajaamua, hilo ni suala lingine. Mtu anaweza kushawishiwa vizuri kabisa kinyume na convictions zake, lakini kama hajawa na utashi basi mawazo yake ndiyo yatapewa kipaumbele kwa kufuata na kufanya atakacho mwenyewe hata kama anajua fika yanampeleka mrama. Ndiyo maana maamuzi yetu hayana budi kuwa activated (kuchomelewa) na nguvu kutoka juu.

Halafu, kutangaza juhudi nzuri ni namna bora ya kujihami na kuwasaidia wengine wanaostruggle au waliopiga hatua. Chances za kushinda huwa inaongezeka zaidi. Nadhani unajua mambo ya accountability & transparency. Huko nako zinaapply.
 
Hii ni poa sana
 

Mwenyezi Mungu azidi kukubariki
 
Naona uvumilivu wako unafika kiwango fulani tu. Mbona usivumilie ukajitoa kwenye hiyo misala mazima!??? Utakuwa unaishi kwa amani na furaha sana. Most problems that we find in our lives, we put there ourselves.
 
Hapo kwenye umalaya hapo dah..vijana mmekua addicted na "kwa mpalange" inahitaji kujitoa sana chief.
 
Hakuna kitu kinaitwa kunywa kwa kiasi. Watu. Kama umwshindwa kujizuia kunywa ukiwa sober, huwezi hata kidogo wakati ushaanza kunywa eti kufanya maamuzi ya kuwa na kiasi. Solution ni prevention siyo cure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…