Malezi ya sasa hivi ni mabovu kabisa

Malezi ya sasa hivi ni mabovu kabisa

Maybe mfano huu utanielewa, huyu ni Mtanzania mwenzetu, na huyu ni mwanamke anacheza mziki wa Singeli ambao Waziri ambaye ni mwana CCM anataka mziki kama huu Ndio uwe utambulisho wetu kimataifa.

Hizi nyimbo zinachangia pakubwa Sana mmomonyoko WA malezi na maadili kwenye jamii ambapo huishia kuchagiza Ngono zembe, early adolescents pregnancies na STIS.
KUMBUKA:
hawa ndio CCM wanaowatumia hawa Wa Singeli ili kupata Kura..... nadhani unaanza kunielewa
View attachment 3242823
Mambo haya hata serikali ya ccm inapenda

Ova
 
Kuna wazazi sasaivi mnausasa wa kuwaacha watoto wajifanyie wanavyo taka wao yaani wanajifanyia maamuzi ndio maana sasaivi wasichana wengi wamezalia nyumbani na mmelizikia hivi ni kawaida mtoto wa kike kazalia nyumbani mtoto wa kwanza ukasema bahati mbaya na wa pili anazalia nyumbani na baba tofauti na bado unaendelea kumlea hapo kwako kweli?

Zamani haikuwa ivyo kabisa watu walikuwa wanajichunga ila sasaivi uhuru umepitiliza embu wazazi acheni usasa ndio maana sasaiv mwanaume apewi thamani yake kama zamani wakati kipindi cha nyuma mwanaume alikuwa anathaminiwa sana tofauti na sasa mwanaume wanatumika tu vibaya hii lekebisheni wazazi wafunzeni watoto wakike wajue thamani ya mwanaume wajue kuwa mwanaume ni nan
Sasa shida ni kwamba ukitaka ujaribu kumithirisha haya mambo na zamani kuna kitu pia unatakiwa ukifikirie mkuu.

Zamani mtu akivunja ungo hakai sana anaolewa ila siku hizi mtoto anavunjia ungo shule tena ndio kwanza shule ya msingi, akipata bahati ya kusoma hadi chuo kikuu utaona kuna miaka kibao hapo katikati, na kimsingi mtoto wa kike akishavunja ungo inamaana mwili nao unakua tayari unahitaji ile kitu katika nyakati fulani za mabadiliko ya kimwili.

Kwahiyo atajizuia atashindwa tu na badala yake ataachia watu watafanya uharibifu wao.

Na kutokea hapo kwenye uharibifu unachotakiwa ufikirie zaidi ni kwamba swala la mtoto wa kike kuzalia nyumbani si swala la mtoto wa kike pekee, haya maadili inatakiwa wafunzwe zaidi watoto wa kiume kuliko wa kike kwa maana mtoto wa kike anapoingia kwenye mahusiano na mtu anaempenda huwa anakua msikilizaji zaidi kuliko kuamua, ila mtoto wa kiume anakua muamuaji zaidi kuliko kusikiliza.

Na huo usikilizaji wa mtoto wa kike kwa mwanamume huwa unatokana na imani yake kwake, kwahiyo maamuzi mengi ya kipumbavu ikiwemo ya kubeba mimba zisizotarajiwa huwa zinaanzia hapo.

Watoto wa kiume ndio wenye uwezo wa kuwalinda dada zao na kupunguza wimbi la wao kuzalia nyumbani hasa kama wataamua kupunguza ulaghai au wakiamua kuwa na maamuzi sahihi wanapoliendea hili tendo na watu ambao wanajua kabisa hawana future nao yoyote isipokua wanawalaghai tu ili wapunguze craving yao ya mapenzi.

Hapa tuseme tu ya kwamba jando na unyago vyote vimefeli ila ukitaka umuokoe mtoto wa kike mpe maadili mtoto wa kiume na kuhusu kutokuwaheshimu waume zao hapo sasa wacha turudishe maiki kwao wenyewe watuambie, ni nini mbaya😅
 
Walikuwa wanawaozesha kuepuka kuzalia nyumban yaan kuletewa mtoto ambaye baba yake hajulikani na ndio kinachotokea sasa
 
Exposure ya mitandao ya kijamii,mass media, na utandawazi vimechangia kuharibu watoto hasa wa kike.
Wazazi wanaplay part yao wanajitahidi sana, lakini vishawishi na vichochezi ni vingi na vipo mikononi mwa watoto,sebuleni, mtaani,shuleni na kote waendako.

Kuna mtoto wa mchungaji anafundishwa vyema kabisa maadili na wazazi wapo makini nae, ila kaishia kuzalia nyumbani na ni danga konki.
Mnazungumiaje na sisi watoto wadogo kiume wa miaka 35🤣🙌tupo hatuoi sababu hatuna fedha
 
Walikuwa wanawaozesha kuepuka kuzalia nyumban yaan kuletewa mtoto ambaye baba yake hajulikani na ndio kinachotokea sasa
Sasa sasa hivi utamuozesha mtu ambae bado anasoma? Utaiambiaje jamuhuri ili ikuelewe? Inshort mambo yameshabadilika kwa maana hiyo zamani unayoisemea wewe hata kijana ambae tayari ameshabalehe na ameshaanza maisha ya kujitegemea lazima aoe na asipooa vikao vitakaliwa ili aseme ako na shida gani ila siku hizi watu hadi wanaota mvi hawaoi na wala hamna cha kuwafanya kwasababu si jambo la ajabu tena siku hizi.

Kwahiyo siku hizi ni utapeli tu ndio umejaa kwenye mapenzi, na utapeli huu unawaumiza zaidi watoto wa kike kuliko wa kiume kwa maana mtu aliyetia mimba Hana alama ila aliyetiwa anabaki na alama ya maisha.

Tuwafunze watoto wetu wakiume wawe wanaume ili wajue namna ya kuwalinda Hawa wanawake hasa katika upande huo wa kuzalia nyumbani.

Kwasababu hakuna maadili yatakayoweza kuwazuia watoto wakike waache kufanya mapenzi, as long as wanakula na kushiba, lakini je, wanafanyaje hayo mapenzi? Hapo ndio pakupafanyia kazi.
 
Allow us be free
Maisha yenyewe ndo haya haya kila mtu afanye chenye roho Inapenda😑
 
Back
Top Bottom