Malezi ya sasa hivi ni mabovu kabisa

Malezi ya sasa hivi ni mabovu kabisa

Ndugu zangu hakuna bingwa wa malezi mtoto akiamua kukengeuka anakengeuka tu hata uwe mkali kama mzee Masawe au mzee Jumbe (i. e wazee wakaksi na wakali mtaana niliokulia) ila bado kuna watoto wao walishindikana na kuwa vivuruge kupita maelezo
Inategemea na marafiki na mazingira aliyokulia nayo mtoto. Kama marafiki wa mtoto wako ni wavuta bangi piga unavyo piga ila huyo mtoto anaweza kuwa mvuta bangi. Kama mtoto wako kila siku anaingia kwenye mitandao ya kijamii na kufuatilia vitu vya kipuuzi na yeye anaweza kukengeuka.

Hakikisha akili ya mtoto wako inalishwa vitu salama.
 
Wazazi hamuongei na binti zenu.

Ishu sio kujiamulia hata asipojiamulia kama hana maarifa mimba atapata tu.
Ufinyu wa maarifa ndio huzalisha hizo mimba mfululu, kama baba/mama unaona aibu kumfundisha binti yako ajikinge vipi na mizagamuo usitegemee miaka hii ya technology vitisho vyako vitamzuia kupigwa pipe.

Assume unaishi jiji kama Dsm, Mwanza,Arusha eti umfukuze binti kigori wa miaka 17 utegemee atakosa pa kwenda, utaishia kumpoteza zaidi.

Maisha yanabadilika wakuu, tusipokubali kubadilika na kuzidi kusolve matatizo kizamani basi tutazidi kukuza tatizo.
 
Zamani binti asiye na shughuli kuishi nje ya nyumba ya wazazi wake kabla ya kutolewa mahali ilikuwa ni tusi kwa mzazi, binti asiye na shughuli yupo home kumpa mzazi hela au zawadi yoyote ni tusi kwa mzazi.Siku hizi wazazi wanapokea hawajui binti kavitoa,wapi mpaka madingi siku hizi nao wanapokea vitu wasivyojua mabinti zao wamevitoa wapi,ndio maana wazazi hawanaga kauli binti anatoka mda wowote na kurudi mda autakao,binti anamiliki vitu vya thamani wakati hana issue, utakuta mpaka bi mkubwa wake anawajua mabwana wa mtoto wake na home wanakuja.Ndio maana binti akipewa mimba wazazi wanakuwa hawana kauli.

Ukija kwa vijana kiume,hawapitishwi kwenye lile tanuli la wanaume walio pitishwa wazee wetu,hii 50/50 na haki sawa imeharibu mind na akili za vijana wengi wa kiume ndio wengi wanashindwa kuwajibika kwa familia zao hasa watoto. Zamani kwanza dingi ukikosea anapewa dozi na mineno yako mikali.Ila siku hizi mtoto wa kiume analelewa kimayaimayai.Tena wazee wazamani wakikuona umeanza kurukaruka na binti, dingi anakuita anakwambia ukweli, kwamba ukitia mimba binti yoyote unaoa na kwake unahama hamna mjadala hapo.Siku hizi vijana wanatia mimba,then mitoto anachiwa bibi na kuna wengine hata hela ya matumizi hawatoi,zigo anaachiwa bibi na babu.

Jando na Unyago hivyo vitu vilifanya vijana wajijue wao ni nani na wajibu wao katika familia na jamii kiujumla. Siku hizi vitu vipo hovyo Social networks kuna fujo tupu na marole model wa hovyo, ukija mashuleni mwendo mafunzo ya 50/50 na usawa wa kijinsia,wazazi hawana time na watoto wanatafuta hela, kazi ya malezi wamewachia wadada wa kazi kwa kifupi vurugu mechi kwenye familia na jamii kiujumla.
 
Kuna wazazi sasa hivi mnausasa wa kuwaacha watoto wajifanyie wanavyo taka wao yaani wanajifanyia maamuzi ndio maana sasaivi wasichana wengi wamezalia nyumbani na mmelizikia hivi ni kawaida mtoto wa kike kazalia nyumbani mtoto wa kwanza ukasema bahati mbaya na wa pili anazalia nyumbani na baba tofauti na bado unaendelea kumlea hapo kwako kweli?

Zamani haikuwa ivyo kabisa watu walikuwa wanajichunga ila sasaivi uhuru umepitiliza embu wazazi acheni usasa ndio maana sasa hivi mwanaume apewi thamani yake kama zamani wakati kipindi cha nyuma mwanaume alikuwa anathaminiwa sana tofauti na sasa mwanaume wanatumika tu vibaya hii lekebisheni wazazi wafunzeni watoto wakike wajue thamani ya mwanaume wajue kuwa mwanaume ni nan
Tatizo wazee wa Sasa wengi wanapenda kitonga Kuna wezee unakuta anahudumiwa na Binti ayise na kipato ila anaona na hajaolewa na anajigamba mtaani kabisa
 
Hata wanao wapachika hizo mimba nao ni shida vile vile mtu kamdanganya mtoto wangu kwa vi chipsi chipsi na kumpeleka geto la kuazima kwa masela wake mtoto nae kajaaa kapigwa mimba baadae anakuja kujua aliempa mimba hana chochote pengine hata godoro hana na binti kutoa mimba anaogopa sasa akishajifungua unadhani kirahisi rahisi ataenda kukaa kwa huyo kijana ilhali kwao anakaa pazuri anakula vizuri....hawa vijana wanao vaaa haya mayebo yebo yamepanda juu na vi soksi ndo shida nyingine kwa watoto wetu...
 
Sasa sasa hivi utamuozesha mtu ambae bado anasoma? Utaiambiaje jamuhuri ili ikuelewe? Inshort mambo yameshabadilika kwa maana hiyo zamani unayoisemea wewe hata kijana ambae tayari ameshabalehe na ameshaanza maisha ya kujitegemea lazima aoe na asipooa vikao vitakaliwa ili aseme ako na shida gani ila siku hizi watu hadi wanaota mvi hawaoi na wala hamna cha kuwafanya kwasababu si jambo la ajabu tena siku hizi.

Kwahiyo siku hizi ni utapeli tu ndio umejaa kwenye mapenzi, na utapeli huu unawaumiza zaidi watoto wa kike kuliko wa kiume kwa maana mtu aliyetia mimba Hana alama ila aliyetiwa anabaki na alama ya maisha.

Tuwafunze watoto wetu wakiume wawe wanaume ili wajue namna ya kuwalinda Hawa wanawake hasa katika upande huo wa kuzalia nyumbani.

Kwasababu hakuna maadili yatakayoweza kuwazuia watoto wakike waache kufanya mapenzi, as long as wanakula na kushiba, lakini je, wanafanyaje hayo mapenzi? Hapo ndio pakupafanyia kazi.
Mkuu kama una watoto wa kike basi wana hasara kubwa ya kupata baba kama ww.
Ww unasema watoto wa kike hawawezi kujizuia vipi kuhusu watoto wa kiume ndo wenye uwezo wa kujizuia?
Mlinzi wa kwanza wa mwili wako ni ww mwenyewe maana ndo unajua thamani yako na si kutegemea mtu ambaye mmekutana ukubwani eti akulindie thamani ya mwili wako huo utakuwa ni upumbavu wa hali ya juu.

% 95 ya masingo mother ,usingo mother wao walijitakia tena waliutafuta kwa nguvu.
Kati ya hao masingo mother wapo ambao kipindi cha ubinti wao walisha fuatwa na wanaume kibao wa maana wenye nia nzuri ya kujenga nao familia lakini waliwakataa kwa kisingizio cha hawana hisia nao sijui ni washamba alafu wakaenda kutembea na mabad boy wanyoa viduku,bodaboda,wabani sidii,wavuta bangi.
Wapo walio fuatwa na wanaume wenye nia nzuri ya kuwaowa wakawakataa badala yake wakaenda kufanya umalaya na waume za watu huku wakiwa wanajua kabisa.
Wapo masingo mother walio onywa juu ya mienendo yao na watu wazima wao wakajibu mimi nimesha kuwa mtu mzima nina uwezo wa kujiamlia.
Kinacho ponza wanawake wa siku hizi ni tamaa na uzungu wa kipumbavu na ndio maana hata baada ya kuolewa bado wanaendelexa umalaya wakati ana mme ndani.

Nyinyi wenye tabia za kuwaaminisha wanawake kuwa watatizo yao yana sababishwa na wanaume ndo waharibifu wakubwa wa wanawake wa kizazi cha sasa.
Familia za sasa zimeharibika si kwa watoto wa kiume wala wa kike kwasababu nyinyi wazazi mmeendekeza uliberali kwenye familia.
 
Watt wenyew wazaz mdio tuna wahatibu hv mtt mdog inanzaje mkukata nywele kama kichwa cha chn mtt wa kike mama leo nalala kwa kina Nancy
Kuna birthday sijui shule jratu mpk jpl huna tatjmin humo humo watt wananza kuharibika
Kabisa wazazi ndio sababu mtoto wa kiume anafuga nywele na ana sukwa na mama yake aibu
 
Ndugu zangu hakuna bingwa wa malezi mtoto akiamua kukengeuka anakengeuka tu hata uwe mkali kama mzee Masawe au mzee Jumbe (i. e wazee wakaksi na wakali mtaana niliokulia) ila bado kuna watoto wao walishindikana na kuwa vivuruge kupita maelezo
Timiza wajibu wako kwanza hata akikengeuka akengeuke mwenyewe, ila wewe unacho takiwa kutimiza wajibu wako.

Sijajua imani yako,hata Yesu aliwafundisha wanafunzi wake ila bado mmoja akakengeuka ila alikiwa tayari kishatimiza wajibu wake.
 
Watoto wanaozalia nyumbani wengi ni wa masikini, wazazi hawatimizi majukumu yao ya kuhudumia watoto.
Sio kweli ata wakishua now ni kuzaa tu ila uko uswahilini ndio unakuta mama ana mimba na mtoto ana mimba
 
Kuna wale timu kataa ndoa, hao nao ni mchango wa tatizo. Wanajisifu kula tunda kimasihara, lakini hawataki kuwajibika. Sasa hapo utasema kuna mtoto wa kiume au sifuri. Mtoto wa kiume anadiriki kusema kwenye ndoa zenu kuna watoto wetu. Wakati enzi zetu tulikuwa tukipigania watoto. Hawa jamaa ni mbuzi kabisa. Na wengi wao ni akina kalubandika au wanaita Yahya, wenyewe siku hizi wanaita marioo. Hawana wanachokijua, wenyewe wanafikiria ngono tu. Hawajui kwamba wanapimwa kwa ngono wakiwa na umri wa chini ya 45. Lakini wakiwa zaidi ya hapo, hakuna kitu. Tena hawa kizazi cha chips yaani ndiyo kabisa. Matokeo yake wakiwa na miaka 45 tu unakuta mtu kachoka utafikiri ana 65+. Kitu kinachomtafuna ni hana hela kwa sababu muda ambao alitakiwa kutafuta hela yeye alikuwa akichakata mbususu, hana ndoa kwa sababu wakati wenzake wanajenga familia na kujenga uwezo wa kiuchumi yeye alikuwa akila bata na hana nguvu za kiume tena kwa sababu ni lofa, hana kitu. Anakuwa mtu wa kudharauliwa tu. Hatimaye presha inapanda anakufa. Kwisha habari yake
Nachoona now vujana wakiume wanashindana ili aonekane kidume kwa kula tunda
 
Ndugu zangu hakuna bingwa wa malezi mtoto akiamua kukengeuka anakengeuka tu hata uwe mkali kama mzee Masawe au mzee Jumbe (i. e wazee wakaksi na wakali mtaana niliokulia) ila bado kuna watoto wao walishindikana na kuwa vivuruge kupita maelezo
Sawa ila mtoto wa kike lazima umtengene awe na haiba ya kike
 
Mtoto wa kike aliyelelewa bila baba yake kichwani hamna kitu, atapita njia zilezile alizopita mama yake!
Hata mafanikio ya watoto kike waliyolelewa na single mother ni ya kutokana na uzinzi!
 
Serikali Ina Wajibu Wa Kusimamia Heshima Na Maadili Ya Raia Wake Wengi Hamlitazami Jambo Hili Kwa Upande Huo
Familia Inaweza Ikampa Malezi Mazuri Binti Yao Ila Sasa Kuna Shule,Mtaa,Social Media Vyote Vinamsubili Huyo Mtoto Aliyelelewa Vyema Ili Vimuhalibu
Je Unaona Redio Na Vipindi Vyake Jinsi Vinavyoharibu Maadili? Serikali Iko Wapi? Vipindi Vya Tv Navyo Unaona Vitu Wanavyoonyesha Je Serikali Kuna Jitihada Zinachukua?
Hivi Serikali Ikipiga Marufuku Mambo Mengi Yanayoonekana Ya Hovyo Hamuoni Kidogo Jamii Yetu Haitasalimika?
Jamii Kama Za Kihindi Na Wakorea Mbona Wako Kwenye Zama Hizi Hizi Za Utandawazi Na Wamebaki Kuwa Vile Vile Kama Wako Karne Ya 19?

Mambo Yote Ya Hovyo Mbeba Lawama Ni Serikali Kuiacha Jamii Ifanye Inavyotaka Wanachosubiri Wasikie Mtu Kabaka Wampeleke Mahakamani Badala Ya Kuzuia Ubakaji Wanangoja Watu Wauwane Kwenye Mahusiano Waitishe Press Kuelezea Tukio.
Wakati Walikuwa Na Njia Nyingi Za Kufanya Narudia Tena Hata Kama Umlee Mtoto Wako Kimaadili Kiasi Gani Bila Serikali Kusimamia Ni Sawa Na Bure.
Kwa Maana Malezi Yana Sehemu Kubwa Sio Tu Nyumbani Ni Kuanzia Ngazi Ya Familia Mtaa,Wilaya,Mkoa Mpaka Kitaifa Vinginevyo Acha Tu Tuendelee Kuishi.

Na Hii Mimi Nadhani Ni Mipango Maalum Ya Kuendelea Kuzifanya Jamii Zizidi Kuwa Na Matabaka Kwamba Mtoto Wa Rais Kawa Rais Hii Michezo Inapatikana Kwenye Jamii Za Hovyo Kama Ilivyo OtherWise Tuongozane Kifalme.
TATIZO NI SERIKALI.
 
Mambo yamegeuka na hapo hajaolewa, atazaa tena na mwanaume mwingine, kipindi cha nyuma wanawake wakiambiwa ni kiwanda cha kuzalisha walikuwa wanakuwa wakali, sasa saizi binti anapewa mimba, anazaa mwanaume anaingia mitini, anakuja mwanaume mwingine anaweka anasepa anakuja mwanamke mwingine naye anasepa

Yaani saa hii ni shida. kuna moja ilitokea huyo singo maza alikuwa na watoto wawili moja wa kike na mwingine wa kiume huko kanda ya ziwa. Wakubwa wote wako chuo kikuu. Sasa mara binti kabebeshwa mimba huko chuoni. Kapambana, kajifungua baada ya muda fulani mtoto kaachiwa bibi, yaani mama wa binti, ili binti aendelee na masomo. Mara baada ya muda fulani, naye wa kiume akabebesha mimba binti huko chuoni alikokuwa anasoma. Wakalea mimba kimya kimya, mara yule binti wa watu akajifungua. Sasa ukitaka kujua hawa watoto vichwa vibovu, naye akapanga na mzazi mwenzake kwamba mtoto tukamuache kwa maza, bila hata kumuonea huruma kwamba mama yao ni singo maza. Basi kijana akawa anampigia mama yake, "halo mama shikamoo, kuna mjukuu wako namleta hapo home". Mama naye "mjukuu wangu yupi?". Kuna binti nasoma naye ndiyo tumezaa. Maa akamchenjia. "Huyo mjukuu simjui, kaeni naye nyie wenyewe". Lile likijana lilivyo lijinga, likaanza kusema, mbona mtoto wa dada yangu uko naye. kwa nini unamkataa huyu mtoto wangu. Mama akasema hiyo mimi sijui. Likijana lile lilvyo lipuuzi likajiua. Likamuachia mama yake majonzi yasiyopimika. Hao ndiyo aina ya watu wanaoitwa gen-zii, yaani ni zii kweli
 
Back
Top Bottom