Mkuu kama una watoto wa kike basi wana hasara kubwa ya kupata baba kama ww.
Ww unasema watoto wa kike hawawezi kujizuia vipi kuhusu watoto wa kiume ndo wenye uwezo wa kujizuia?
Mlinzi wa kwanza wa mwili wako ni ww mwenyewe maana ndo unajua thamani yako na si kutegemea mtu ambaye mmekutana ukubwani eti akulindie thamani ya mwili wako huo utakuwa ni upumbavu wa hali ya juu.
% 95 ya masingo mother ,usingo mother wao walijitakia tena waliutafuta kwa nguvu.
Kati ya hao masingo mother wapo ambao kipindi cha ubinti wao walisha fuatwa na wanaume kibao wa maana wenye nia nzuri ya kujenga nao familia lakini waliwakataa kwa kisingizio cha hawana hisia nao sijui ni washamba alafu wakaenda kutembea na mabad boy wanyoa viduku,bodaboda,wabani sidii,wavuta bangi.
Wapo walio fuatwa na wanaume wenye nia nzuri ya kuwaowa wakawakataa badala yake wakaenda kufanya umalaya na waume za watu huku wakiwa wanajua kabisa.
Wapo masingo mother walio onywa juu ya mienendo yao na watu wazima wao wakajibu mimi nimesha kuwa mtu mzima nina uwezo wa kujiamlia.
Kinacho ponza wanawake wa siku hizi ni tamaa na uzungu wa kipumbavu na ndio maana hata baada ya kuolewa bado wanaendelexa umalaya wakati ana mme ndani.
Nyinyi wenye tabia za kuwaaminisha wanawake kuwa watatizo yao yana sababishwa na wanaume ndo waharibifu wakubwa wa wanawake wa kizazi cha sasa.
Familia za sasa zimeharibika si kwa watoto wa kiume wala wa kike kwasababu nyinyi wazazi mmeendekeza uliberali kwenye familia.
Mimi bado sijabahatika kuwa na mtoto ila nikibahatika nitajitahidi kwa kiwango changu kumlea katika namna ile ambayo nataka awe huku nikiwa najua kuna umri fulani akifikia mambo mengi yatabaki kuwa mikononi mwake na watu wengine ambao atawaamini kama ambavyo ananiamini mimi...
Ndoa ni swala la maisha na maisha ukomo wake ni kifo so before ya ukomo inatakiwa uyafurahie maisha yako so huwezi walaumu waliowakataa wanaume kwa sababu ya kutokuwapenda, mwisho wa siku Kila mtu anamachaguo yake, namimi nawapongeza kwa hilo kwa maana huwezi kujilazimisha kuishi na mtu ilimradi na wewe uonekane uko ndani ya ndoa wakati haufurahii ndoa yako... Halafu huu nao ni ukandamizaji wawazi, haiwezekani wanaume ndio wao wawe wenye machaguo pekee kuliko wanawake kwenye maswala haya ya ndoa, hata kama wanaume ndio waoaji ila Binti nae anatakiwa achague ni nani wa kuolewa nae kati ya wale wanaomfuata kwa lengo hilo.
Lakini pia umeelezea vizuri sana hapo kuanzia kumkataa mtu fulani na kwenda kumkubali mtu fulani kwa maana hii ndio ile aina ya upendo niliyoizungumzia ya kwamba mwanamke akipenda huwa anakua msikilizaji zaidi ya kuamua, na hao wanaojiita bad boys kwasababu huwa wako na swags na wanajua hawa wanawake wanataka nini ndio maana mara nyingi huwa wanawin, kwasababu mapenzi ni mchezo wa hisia zaidi kuliko akili.
And naomba nisisitize hili, siko hapa kumtetea mwanamke wala kumkandamiza mwanamume, ila nnachojaribu kusema hapa ni kwamba swala hili la kuzalia nyumbani haliwezi kuzuiliwa na mtoto wa kike pekee bali kwa wote kwa maana ya mtoto wa kike na wakiume.
So, wafunzeni hao vijana wenu wanaojiita mabad boy, wajaribu kuwalinda hao wanawake zao, kwa maana wao ndio huwa wanadrive hii game so wanachoamua wao mara nyingi huwa ni kama Sheria kwa hao wanawake na ndio mimba nyingi zinaanzia hapo.
Narudia tena, hili tatizo la kuzalia nyumbani haliwezi kupungua kama wanaume tutaamua kulikwepa na kujiona sisi hatuhusiki na kuelekeza lawama zote kwa hawa mabinti, ila tukiwajibika ipasavyo nadhani kwa sehemu kubwa sana haya mambo yatapungua.
Tujaribu kujiona na sisi pia ni sehemu ya hili tatizo halafu tuangalie namna ya kukabiliana nalo, najua umeshakua kwenye mahusiano mara kadhaa na yapo ambayo ulikua unamlaghai Binti ilihali ukijua fika hakuna future yoyote kati yenu ila upo nae kwaajiri ya kuendesha muda tu, lakini huyo Binti alikua anaamini karibia yote uliyokua unamwambia, sometimes unamlazimisha aje mfanye mapenzi hata akiwa kwenye siku zake za hatari tena bila kinga kwa kisingizio cha kumwaga nje na kwakua anakupenda na anajua wewe ndio future yake anakukubalia kwa moyo mmoja.... (Aisee hili tatizo hatuwezi kulikwepa kaka, na sitajari watu wanasemaje kwenye huu Uzi ila Mimi nitabaki na msimamo wangu ya kwamba tukubali kuwajibika ili tuwasaidie hawa mabinti) nukta!