Mama aliyedaiwa kufanya ukatili na video yake kusambaa mitandaoni akimpiga mtoto akamatwa

Ila watoto wa siku hizi tunawadekeza sana! Hicho hakiwezi kuitwa kipigo au kumshambulia mtoto. Ni cha kawaida sana kwa mtoto mtovu wa nidhamu. Kama huwa anampiga kila siku hiyo ni habari nyingine lakini kama ni pale anapokosea, ni kawaida sana!
Utawaweza baba na mama junior? Ndio hao wanaona huyo mtoto kapigwa sana yaani angeweza kufa.
 
Watu wanashadadia upuuzi sana.

Mtoto kapewa adhabu ya kawaida sana.

Huwezi kumlea mtoto bila adhabu. Utavuna mabua.

Mtoto hufundishwa akiwa mdogo, utii, nidhamu na uwajibikaji hayaji tu hivi hivi. Awe mama yake au sio mama yake mzazi binafsi sijaona ukatili hapo. Tena kampiga vibao vinne tu kama sijakosea.

Kwa malezi ya online, no wonder watoto wanatukana wazazi wao mitandaoni huko, watoto hawali mpaka uwawekee cortoon zao pendwa, watoto wawatuma hadi dada wa kazi πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wananchi walipaza sauti Heko kwao...viongozi waliochukua hatua...ndio kazi yao...mwezi huu wanakula mshahara kutoka kwaa wananchi walipa kodi kihalali.
Yaani upige mwanangu kiasi hiki nikuache salama?
Labda sio mimi
 
Utawaweza baba na mama junior? Ndio hao wanaona huyo mtoto kapigwa sana yaani angeweza kufa.
Ukiona mtoto amefikia hatua ya kutosikia ujue chanzo kikuu ni mzazi.
Siku hizi watoto hawana malezi bora na kipigo cha namna hiyo hakisaidii
 
Watu wanashadadia upuuzi sana.

Mtoto kapewa adhabu ya kawaida sana.

Huwezi kumlea mtoto bila adhabu. Utavuna mabua.
Ni ujinga tu kupiga watoto. Ninao wanne wa kwanza 18 wa mwisho 11 sijawahi wapiga hata siku moja na wote wana tabia njema. Tena mitoto inayo pigwa pigwa ndio inakua minunda na katili.
 
Shida ipo kwenye Mimba za utotoni na umasikini. . Unakuta mama katelekezwa na mwanaume haudumii ndo maana unakuta vitendo hivyo vinatokea . Afya ya akili ni muhimu unamkuta mama kajaa tu hasira anachukua maamuzi ya kumpiga mtoto kiasi hicho. Sizani kama familia inapata basic needs kama chakula, maradhi na mavazi pia mama ana hudumiwa ipasavyo hali hio ingetokea. Pia afya ya akili ni muhimu ( huenda huyo mama ana tatizo)

Serikali ingewasaidia kwa kuwapa fedha ili wawe stable kimaisha waondoe Umaskini ndo maaa kero hizo za unyanyasaji kwa watoto zinaendelea kutokea, kumkamataa sio kumaliza tatizo. Tatizo n umasikini na hali ya maisha. Mfikishieni waziri anaehusika.......
 
Bila kupepesa macho nilikuja mbio nikitegemea ntaona ukatili wa hali ya juu na nilipoona yale madumu nikawaza hii video ikiendelea huyu mama atampiga na madumu huyu dogo kumbe duuuh hebu tuwe serious hivi vipigo tulivyopewa na wazee wetu si zaidi ya hivyo hapo jamani
 
Huu ndiyo ujinga wa wazazi wa tamthilia. Wajinga sana!
 
Reactions: I M

Maisha haya ninawaza hadi ninajikuta ninajiuliza hivi kama siyo adhabu na kichapo ningekuwa wapi?

Huwa ninawasikitikia watoto waliodekezwa enzi zetu aisee wamekuwa watu wa hovyo.
 
Ni ujinga tu kupiga watoto. Ninao wanne wa kwanza 18 wa mwisho 11 sijawahi wapiga hata siku moja na wote wana tabia njema. Tena mitoto inayo pigwa pigwa ndio inakua minunda na katili.

πŸ˜„ Umri wa 18 years bado ni mtegemezi na yupo kwako na bado hujamaliza malezi.

Kawaida tabia halisi ya mtoto ni namna anavyohusiana na jamii ya watu baki haswa akianza kujitegemea.

Wazazi wengi mkiambiwa tabia za wanenu mnakataa na kuwatetetea.

Kudekeza mtoto siyo malezi.
 
Ukiona mtoto amefikia hatua ya kutosikia ujue chanzo kikuu ni mzazi.
Siku hizi watoto hawana malezi bora na kipigo cha namna hiyo hakisaidii
Wewe mbona kipigo kilikusaidia? Watoto wasiosikia mara moja moja unamtandika. Mbona wengi wananyooka tu.
 
Ni ujinga tu kupiga watoto. Ninao wanne wa kwanza 18 wa mwisho 11 sijawahi wapiga hata siku moja na wote wana tabia njema. Tena mitoto inayo pigwa pigwa ndio inakua minunda na katili.
Kuna wazazi siku wanaambiwa watoto wao ni majambazi huwa hawaamini. Hongera kwa kukuza raia wema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…