Mama amegoma kumnyonyesha mtoto wake kisa amefunga. Je, hii ni sawa?

Mama amegoma kumnyonyesha mtoto wake kisa amefunga. Je, hii ni sawa?

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,843
Reaction score
29,350
Salaam wanabodi!

Bila kupoteza muda, naingia kwenye mada moja kwa moja. Hapa mtaani kwetu, jirani yangu mmoja ameghairi kabisa kumnyonyesha mtoto wake wa mwaka mmoja kwa kisingizio kuwa amefunga kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Nilipomshuhudia akimnyima mtoto ziwa kwa mara ya kwanza nilidhani ni utani lakini baada ya kuchunguza kwa kina nimegundua yupo serious na kweli amemnyima mtoto kunyonya completely. Kitendo hiki kimenihudhunisha sana, hasa ukizingatia kwamba mtoto bado hajawa na uwezo mkubwa wa kula vyakula vya ziada.

Baada ya kujiridhisha na ukatili huu, ndipo nilipopata ujasiri wa kumuuliza kwa nini anamnyima mtoto huyu mdogo haki yake ya msingi ya maziwa ya mama. Akanijibu kwamba amefunga kula (kwa mujibu wa imani yake) hivyo, hata mtoto hatakiwi kunyonya!

Tuzingatie kuwa serikali inaagiza mtoto anyonye maziwa ya mama kwa muda usiopungua miaka 2. Sasa huyu mama anapomnyima mtoto maziwa, mtoto ata-survive namna gani? Tukio hili kusema kweli limenifikirisha sana, hadi nimewaza kumshtaki huyu mama kwa viongozi wa serikali kwa ukatili anaomfanyia mwanaye. Hata hivyo, nimejiuliza kwamba hata nikimshitaki serikalini huenda asichukuliwe hatua yoyote kwa sababu serikali haina dini. Pia, hili linaweza kuchukuliwa kama suala binafsi zaidi ya suala la kijamii. Lakini kwa upande mwingine, nafikiri kitendo cha mama kugoma kumnyonyesha mtoto kinaweza kuchukuliwa kama ukatili kwa mtoto. Lipi kati ya haya mawazo yangu linaweza kuwa sahihi? Nimebaki katika utata sijui la kufanya. Je, huyu mama achukuliwe hatua au hili ni suala binafsi, yeye na familia yake?

Kwa kuwa humu kuna wataalamu wa mambo ya imani, familia na haki za watoto, nimeona ni vizuri kuliweka hadharani ili tusaidiane kupata utatuzi wa pamoja. Isije mtoto akapata utapiamlo kwa kunyimwa lishe ya maziwa halafu mimi nikalaumiwa kwa kukaa kimya. Je, nini kifanyike ili kuweka jambo hili sawa?

Nawasilisha.​
 
Mambo mengine nikuyaendekeza tu, huyo mama mwenye kichanga hakupaswa kufunga......
 
Kwa hiyo amemfungisha na mtoto, hivi mama zetu sometimes wanawaza kupitia nini!? hili jambo ni la dini kweli!? hapa tusiipe dini negativity sidhani kama ni sheria huyo ana yake..
 
Kwa hiyo amemfungisha na mtoto, hivi mama zetu sometimes wanawaza kupitia nini!? hili jambo ni la dini kweli!? hapa tusiipe dini negativity sidhani kama ni sheria huyo ana yake..
Ndio maaana nimeweka jambo hili hapa ili wadau wanaofahamu vizuri walitolee ufafanuzi. isije ikwa tunamlaumu bure mama kumbe yupo sahihi 100%😳🙄😵
 
Kuna mwamba mmoja matata sana hata kum tag naogopa,naona uzi huu hajauona
[emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
 
Kuna mwamba mmoja matata sana hata kum tag naogopa,naona uzi huu hajauona
[emoji23][emoji23][emoji23]

Ova
Sawa, muite aje kutusaidia kuchambua jambo hili mkuu
 
Back
Top Bottom