IROKOS
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 10,182
- 7,850
Kwa kutumia kifungu gani cha sheria?Nadhani hayupo sahihi. Mshitaki serikali ya mtaani.

Wewe ni mtaalamu wa mambo ya lishe na Afya??.Mwaka mmoja ana uwezo wa kula chakula mbadala.. Tulia.
Avatar yako inatisha Sana aisee, naomba uibadilishe.Mambo mengine nikuyaendekeza tu, huyo mama mwenye kichanga hakupaswa kufunga......
Aisee!!!,Watu na Dini zao bhana.Wewe unashangaa hilo tu? Jirani yangu hapa kanyimwa haki yake ya .... Hapa anaimba wimbo wa "Baba paroko ili kujifariji!
Amefanya kosa kumnyima ziwa mtoto,kama hawezi kufunga na kunyonyesha anatakiwa aache kufunga ili amnyonyeshe na hiyo funga atailipia hapo mbeleniSalaam wanabodi!
Bila kupoteza muda, naingia kwenye mada moja kwa moja. Hapa mtaani kwetu, jirani yangu mmoja ameghairi kabisa kumnyonyesha mtoto wake wa mwaka mmoja kwa kisingizio kuwa amefunga kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Nilipomshuhudia akimnyima mtoto ziwa kwa mara ya kwanza nilidhani ni utani lakini baada ya kuchunguza kwa kina nimegundua yupo serious na kweli amemnyima mtoto kunyonya completely. Kitendo hiki kimenihudhunisha sana, hasa ukizingatia kwamba mtoto bado hajawa na uwezo mkubwa wa kula vyakula vya ziada.
Baada ya kujiridhisha na ukatili huu, ndipo nilipopata ujasiri wa kumuuliza kwa nini anamnyima mtoto huyu mdogo haki yake ya msingi ya maziwa ya mama. Akanijibu kwamba amefunga kula (kwa mujibu wa imani yake) hivyo, hata mtoto hatakiwi kunyonya!
Tuzingatie kuwa serikali inaagiza mtoto anyonye maziwa ya mama kwa muda usiopungua miaka 2. Sasa huyu mama anapomnyima mtoto maziwa, mtoto ata-survive namna gani? Tukio hili kusema kweli limenifikirisha sana, hadi nimewaza kumshtaki huyu mama kwa viongozi wa serikali kwa ukatili anaomfanyia mwanaye. Hata hivyo, nimejiuliza kwamba hata nikimshitaki serikalini huenda asichukuliwe hatua yoyote kwa sababu serikali haina dini. Pia, hili linaweza kuchukuliwa kama suala binafsi zaidi ya suala la kijamii. Lakini kwa upande mwingine, nafikiri kitendo cha mama kugoma kumnyonyesha mtoto kinaweza kuchukuliwa kama ukatili kwa mtoto. Lipi kati ya haya mawazo yangu linaweza kuwa sahihi? Nimebaki katika utata sijui la kufanya. Je, huyu mama achukuliwe hatua au hili ni suala binafsi, yeye na familia yake?
Kwa kuwa humu kuna wataalamu wa mambo ya imani, familia na haki za watoto, nimeona ni vizuri kuliweka hadharani ili tusaidiane kupata utatuzi wa pamoja. Isije mtoto akapata utapiamlo kwa kunyimwa lishe ya maziwa halafu mimi nikalaumiwa kwa kukaa kimya. Je, nini kifanyike ili kuweka jambo hili sawa?
Nawasilisha.
Hahaha hapata kalika humuSawa, muite aje kutusaidia kuchambua jambo hili mkuu
Sijahunga mkono hoja soma unielewekwa hiyo wewe unaunga mkono mtoto kunyimwa protini kwa sababu ya kufunga mkuu? Hebu tufafanulie vizuri isije ikwa tunamlaumu mama bila sababu ya msingi.
Haki za Watoto, Wanawake na Watu wenye ulemavu, Kifungu namba 8 (1).Kwa kutumia kifungu gani cha sheria?
Huyo mama hajui maana ya mfungo kabisaSalaam wanabodi!
Bila kupoteza muda, naingia kwenye mada moja kwa moja. Hapa mtaani kwetu, jirani yangu mmoja ameghairi kabisa kumnyonyesha mtoto wake wa mwaka mmoja kwa kisingizio kuwa amefunga kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Nilipomshuhudia akimnyima mtoto ziwa kwa mara ya kwanza nilidhani ni utani lakini baada ya kuchunguza kwa kina nimegundua yupo serious na kweli amemnyima mtoto kunyonya completely. Kitendo hiki kimenihudhunisha sana, hasa ukizingatia kwamba mtoto bado hajawa na uwezo mkubwa wa kula vyakula vya ziada.
Baada ya kujiridhisha na ukatili huu, ndipo nilipopata ujasiri wa kumuuliza kwa nini anamnyima mtoto huyu mdogo haki yake ya msingi ya maziwa ya mama. Akanijibu kwamba amefunga kula (kwa mujibu wa imani yake) hivyo, hata mtoto hatakiwi kunyonya!
Tuzingatie kuwa serikali inaagiza mtoto anyonye maziwa ya mama kwa muda usiopungua miaka 2. Sasa huyu mama anapomnyima mtoto maziwa, mtoto ata-survive namna gani? Tukio hili kusema kweli limenifikirisha sana, hadi nimewaza kumshtaki huyu mama kwa viongozi wa serikali kwa ukatili anaomfanyia mwanaye. Hata hivyo, nimejiuliza kwamba hata nikimshitaki serikalini huenda asichukuliwe hatua yoyote kwa sababu serikali haina dini. Pia, hili linaweza kuchukuliwa kama suala binafsi zaidi ya suala la kijamii. Lakini kwa upande mwingine, nafikiri kitendo cha mama kugoma kumnyonyesha mtoto kinaweza kuchukuliwa kama ukatili kwa mtoto. Lipi kati ya haya mawazo yangu linaweza kuwa sahihi? Nimebaki katika utata sijui la kufanya. Je, huyu mama achukuliwe hatua au hili ni suala binafsi, yeye na familia yake?
Kwa kuwa humu kuna wataalamu wa mambo ya imani, familia na haki za watoto, nimeona ni vizuri kuliweka hadharani ili tusaidiane kupata utatuzi wa pamoja. Isije mtoto akapata utapiamlo kwa kunyimwa lishe ya maziwa halafu mimi nikalaumiwa kwa kukaa kimya. Je, nini kifanyike ili kuweka jambo hili sawa?
Nawasilisha.
Kwa Dini ya kiislamu mwanamke akijifungua inabidi mwanaume umlipe kukunyonyeshea mtoto wako atakuwa huyo hajalipwa mshahara wake ndio maana kagoma kunyonyeshaNadhani hayupo sahihi. Mshitaki serikali ya mtaani.
Hutaki unaacha...Wewe ni mtaalamu wa mambo ya lishe na Afya??.
Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Kwenye ishu ya talaka nimekuelewa vizuri sana mkuu. Je, kwenye ishu ya kumnyima mtoto ziwa wakati huu wa mfungo hili limekaaje?Kama hujui labda tukusaidie hicho kipengele kipo kwenye talaka,kama umemtaliki mkeo halafu akajifungua Mtoto unaweza ukawa unamlipa ujira kwa ajili ya kukunyonyesha Mwanao. Usilamu kila kitu kiko wazi
Asante kwa ufafanuzi mkuu. Unaweza ukaweka katika lugha rahisi ili kila mdau aelewe?Mjamzito au mwenye kunyonyesha akiwa atahofia nafsi Yake kudhurika kwa kufunga basi anaruhusiwa kula,na atailipia saumu hiyo kama vile mgonjwa kwa kauli ya Mtume (S.A.W) Hakika ya Mwenyezi Mungu amemuondoshea msafiri kufunga,na akamshurutisha Kuswali, na akamuondoshea (akampa ruhusa ya kula)Mjamzito na Mwenye kunyonyesha saumu) Na iwapo atakhofia juu ya Mtoto wake peke Yake bila ya kukhofia nafsi yake anaweza kula,na akailipia baadaye,na anatakiwa alishe kila siku (atakayokula)maskini mmoja;kwa kauli ya Ibn Abbas (Na mwenye kunyonyesha na Mjamzito watakapokhofia juu ya watoto wao wanaweza kula,na walishe maskini mmoja)