Mama amegoma kumnyonyesha mtoto wake kisa amefunga. Je, hii ni sawa?

Maamuzi yake hayako sawa. Aliyefunga ni yeye si mtoto hivyo anatakiwa ampe mtoto lishe yake bila kukosa.
Salaam wanabodi!

Bila kupoteza muda, naingia kwenye mada moja kwa moja. Hapa mtaani kwetu, jirani yangu mmoja ameghairi kabisa kumnyonyesha mtoto wake wa mwaka mmoja kwa kisingizio kuwa amefunga kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Nilipomshuhudia akimnyima mtoto ziwa kwa mara ya kwanza nilidhani ni utani lakini baada ya kuchunguza kwa kina nimegundua yupo serious na kweli amemnyima mtoto kunyonya completely. Kitendo hiki kimenihudhunisha sana, hasa ukizingatia kwamba mtoto bado hajawa na uwezo mkubwa wa kula vyakula vya ziada.

Baada ya kujiridhisha na ukatili huu, ndipo nilipopata ujasiri wa kumuuliza kwa nini anamnyima mtoto huyu mdogo haki yake ya msingi ya maziwa ya mama. Akanijibu kwamba amefunga kula (kwa mujibu wa imani yake) hivyo, hata mtoto hatakiwi kunyonya!

Tuzingatie kuwa serikali inaagiza mtoto anyonye maziwa ya mama kwa muda usiopungua miaka 2. Sasa huyu mama anapomnyima mtoto maziwa, mtoto ata-survive namna gani? Tukio hili kusema kweli limenifikirisha sana, hadi nimewaza kumshtaki huyu mama kwa viongozi wa serikali kwa ukatili anaomfanyia mwanaye. Hata hivyo, nimejiuliza kwamba hata nikimshitaki serikalini huenda asichukuliwe hatua yoyote kwa sababu serikali haina dini. Pia, hili linaweza kuchukuliwa kama suala binafsi zaidi ya suala la kijamii. Lakini kwa upande mwingine, nafikiri kitendo cha mama kugoma kumnyonyesha mtoto kinaweza kuchukuliwa kama ukatili kwa mtoto. Lipi kati ya haya mawazo yangu linaweza kuwa sahihi? Nimebaki katika utata sijui la kufanya. Je, huyu mama achukuliwe hatua au hili ni suala binafsi, yeye na familia yake?

Kwa kuwa humu kuna wataalamu wa mambo ya imani, familia na haki za watoto, nimeona ni vizuri kuliweka hadharani ili tusaidiane kupata utatuzi wa pamoja. Isije mtoto akapata utapiamlo kwa kunyimwa lishe ya maziwa halafu mimi nikalaumiwa kwa kukaa kimya. Je, nini kifanyike ili kuweka jambo hili sawa?

Nawasilisha.​
 
Mambo ya kujua dini ukubwani

Baba muislamu basi na wewe unakuwa mwislamu misingi ya dini huijui madrsa hukusoma
 
Ungemchapa kibao
 
Maamuzi yake hayako sawa. Aliyefunga ni yeye si mtoto hivyo anatakiwa ampe mtoto lishe yake bila kukosa.
Hata mimi nimemshangaa sana mkuu. Nikakumbuka kuwa mbona watu wanafunga na kazi wanapiga kama kawaida? So, kwa kuwa kunyonyesha ni jukumu lake la kimama, angeendelea tu kumnyonyesha mtoto kama kawaida bila tatizo.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Shehe ubwabwa, shehe aliyesema Magufuli Ni zaidi ya mtume Mohammed Tena akaenda mbele zaidi na kusema Magufuli Ni zaidi ya MUNGU, anasemaje kuhusu hili?
 
Mambo ya kujua dini ukubwani

Baba muislamu basi na wewe unakuwa mwislamu misingi ya dini huijui madrsa hukusoma
kwa hiyo wewe unaunga mkono mtoto kunyimwa protini kwa sababu ya kufunga mkuu? Hebu tufafanulie vizuri isije ikawa tunamlaumu mama bila sababu ya msingi.
 
Hiyo stori ya mitani hakuna Muisilam mjinga kiasi hicho,ukitegemea ni mtu mzima, mpaka ana mtoto kwani huko nyuma hakuwahi kufunga,istoshe kama ameslim sasa hivi lazima angekuwa a mefundishwa huyo mleta maada muungo anataka kutuchafulia Dini yetu. Huku sio kwa kusema sijui mafuta ya upako sijui kitambaa,Uisilam umekamilika
 
HAWA MAAMUMA VIPI TENA HADI KUNYONYESHA MTOTO???ACHENI KUTESA WATOTO KWA SABABU YA DINI ZA KULETEWA
 
Hiyo stori ya mitani hakuna Muisilam mjinga kiasi hicho,ukitegemea ni mtu mzima, mpaka ana mtoto kwani huko nyuma hakuwahi kufunga,istoshe kama ameslim sasa hivi lazima angekuwa a mefundishwa huyo mleta maada muungo anataka kutuchafulia Dini yetu. Huku sio kwa kusema sijui mafuta ya upako sijui kitambaa,Uisilam umekamilika
Mkuu naona unataka kutuchafulia mada kabla hata hatujapata ufumbuzi kuhusu hatima ya mtoto huyu anayekosa lishe ya maziwa. Tafadhali sana kama huna cha kuchangia kaa kimya, nakuomba.
 
HAWA MAAMUMA VIPI TENA HADI KUNYONYESHA MTOTO???
Kwa hiyo mtoto kunyonyeshwa ni sawa au sio sawa mkuu? Je, mama yupo sahihi kumnyima mtoto lishe kisa amefunga? Fikiria angekuwa ni mwanao asingekuuma?
 
Wewe Uisilam tofauti na Dini zingine Waumini wake wanajielewa kama wanavyomuamini Mungu mmoja, huwezi ukakuta muisilama anafanya ujinga kama huo,mdanganyane wenyewe
 
Salaam wanabodi!

Bila kupoteza muda, naingia kwenye mada moja kwa moja. Hapa mtaani kwetu, jirani yangu mmoja ameghairi kabisa kumnyonyesha mtoto wake wa mwaka mmoja kwa kisingizio kuwa amefunga kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Nilipomshuhudia akimnyima mtoto ziwa kwa mara ya kwanza nilidhani ni utani lakini baada ya kuchunguza kwa kina nimegundua yupo serious na kweli amemnyima mtoto kunyonya completely. Kitendo hiki kimenihudhunisha sana, hasa ukizingatia kwamba mtoto bado hajawa na uwezo mkubwa wa kula vyakula vya ziada.

Baada ya kujiridhisha na ukatili huu, ndipo nilipopata ujasiri wa kumuuliza kwa nini anamnyima mtoto huyu mdogo haki yake ya msingi ya maziwa ya mama. Akanijibu kwamba amefunga kula (kwa mujibu wa imani yake) hivyo, hata mtoto hatakiwi kunyonya!

Tuzingatie kuwa serikali inaagiza mtoto anyonye maziwa ya mama kwa muda usiopungua miaka 2. Sasa huyu mama anapomnyima mtoto maziwa, mtoto ata-survive namna gani? Tukio hili kusema kweli limenifikirisha sana, hadi nimewaza kumshtaki huyu mama kwa viongozi wa serikali kwa ukatili anaomfanyia mwanaye. Hata hivyo, nimejiuliza kwamba hata nikimshitaki serikalini huenda asichukuliwe hatua yoyote kwa sababu serikali haina dini. Pia, hili linaweza kuchukuliwa kama suala binafsi zaidi ya suala la kijamii. Lakini kwa upande mwingine, nafikiri kitendo cha mama kugoma kumnyonyesha mtoto kinaweza kuchukuliwa kama ukatili kwa mtoto. Lipi kati ya haya mawazo yangu linaweza kuwa sahihi? Nimebaki katika utata sijui la kufanya. Je, huyu mama achukuliwe hatua au hili ni suala binafsi, yeye na familia yake?

Kwa kuwa humu kuna wataalamu wa mambo ya imani, familia na haki za watoto, nimeona ni vizuri kuliweka hadharani ili tusaidiane kupata utatuzi wa pamoja. Isije mtoto akapata utapiamlo kwa kunyimwa lishe ya maziwa halafu mimi nikalaumiwa kwa kukaa kimya. Je, nini kifanyike ili kuweka jambo hili sawa?

Nawasilisha.​
Akamatwe na kulamisha kumnyonyesha malaika huyu. Kwani alipobeba mimba hakujua kuwa angefunga? Mbona dini hailazimishi mama anayenyoshe kufunga? Huyo mama ana matatizo yake.
 
Kama hujui labda tukusaidie hicho kipengele kipo kwenye talaka,kama umemtaliki mkeo halafu akajifungua Mtoto unaweza ukawa unamlipa ujira kwa ajili ya kukunyonyesha Mwanao. Usilamu kila kitu kiko wazi
 
Mjamzito au mwenye kunyonyesha akiwa atahofia nafsi Yake kudhurika kwa kufunga basi anaruhusiwa kula,na atailipia saumu hiyo kama vile mgonjwa kwa kauli ya Mtume (S.A.W) Hakika ya Mwenyezi Mungu amemuondoshea msafiri kufunga,na akamshurutisha Kuswali, na akamuondoshea (akampa ruhusa ya kula)Mjamzito na Mwenye kunyonyesha saumu) Na iwapo atakhofia juu ya Mtoto wake peke Yake bila ya kukhofia nafsi yake anaweza kula,na akailipia baadaye,na anatakiwa alishe kila siku (atakayokula)maskini mmoja;kwa kauli ya Ibn Abbas (Na mwenye kunyonyesha na Mjamzito watakapokhofia juu ya watoto wao wanaweza kula,na walishe maskini mmoja)
 
Serikali hawawezi kugoma kumuadhibu kwa kusita kuingilia mambo ya imani?
We jamaa ni mnafiki....post zako nyingi ni za kidini na kutunga. Alafu ni mnunuaji papuchi na mcheza kamari

Acha dhambi na udini. Nenda kanisani ukatubu.
 
Mleta maada kwenye Uisilamu hatuna maji au mafuta sijui vitambaa vya upako,Uisilamu ni Dini iliyokamilika. Ninayekujibu mimi nilikuwa mkristo mwenzako tena nilikuwa natumikia kanisani. Kule nilifundishwa mafundisho ya kukalili,mfano sema baba yetu,sala ya imani sala ya majuto n.k. Lakini huku ndiko kwenye Elimu,nakukalibisha kwenye Heri Dini ya Uisilamu
 
Kiufupi huyo mama anachokifanya ni kinyume cha sheria, Uislam haukuweka sheria na kukosa kuweka njia za utatuzi kwa wale ambao wenye matatizo. "Mtoto anatakiwa anyonyeshwe miaka miwili.
Hapo kuna mawili sheria inamlinda mama anaweza kula ili amnyoneshe mtoto kama akiona akifunga atakaukiwa/ataona maziwa hayatoki na pia inamlinda mtoto apate haki ya msingi ya kunyonya maziwa ya mama miaka miwili, na ushahidi kutoka kwenye Quran:
(وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ ۖ لِمَنْ أَرَادَ أَن يُتِمَّ الرَّضَاعَةَ ۚ وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ لَا تُكَلَّفُ نَفْسٌ إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَا تُضَارَّ وَالِدَةٌ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوْلُودٌ لَّهُ بِوَلَدِهِ ۚ وَعَلَى الْوَارِثِ مِثْلُ ذَٰلِكَ ۗ فَإِنْ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٍ مِّنْهُمَا وَتَشَاوُرٍ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا ۗ وَإِنْ أَرَدتُّمْ أَن تَسْتَرْضِعُوا أَوْلَادَكُمْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِذَا سَلَّمْتُم مَّا آتَيْتُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ )

البقرة (233) Al-Baqara

Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kaamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha. Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo. Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa kwa kuridhiana na kushauriana, basi si vibaya kwao. Na mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha basi hapana ubaya kwenu mkitoa mlicho ahidi kwa mujibu wa ada. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayo yatenda.

Lakini pia kwa mapokeo ya hadith kuhusu ruhusa hii ya kutokufunga mwenye mimba au mwenye kunyonyesha:

قال النبي صلى الله عليه وسلم : "(( إِنَّ اللَّهَ تَعَالَى وَضَعَ عَنْ الْمُسَافِرِ الصَّوْمَ وَشَطْرَ الصَّلاةِ ، وَعَنْ الْحَامِلِ والْمُرْضِعِ الصَّوْم))َ رواه الترمذي وصححه الألباني في صحيح الترمذي

Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema; (Allaah سبحانه وتعالى) Ameondosha shuruti ya kufunga kwa msafiri, na nusu ya Swalah, na mwanamke mwenye mimba na mwenye kunyonyesha)) [At-Tirmidhiy na ni Swahiyh kutoka kwa Shaykh Al-Abaaniy].
 
Mzee mwenye mji atembeze mkong'oto wa haja ili angalao mtoto anyonyeshwe
 
Back
Top Bottom