Mama amegoma kumnyonyesha mtoto wake kisa amefunga. Je, hii ni sawa?

Mimi sio muislamu...lakini hii hadithi ni ya kutunga. Asanteni na kwaherini.
 
Amefanya kosa kumnyima ziwa mtoto,kama hawezi kufunga na kunyonyesha anatakiwa aache kufunga ili amnyonyeshe na hiyo funga atailipia hapo mbeleni
 
Si mfahamu huyo mama lakini kwa uzoefu wangu wa maisha na namna ninavyojua wamama kwa watoto.Hii habari siiiamini kwa asilimia 95.
 
kwa hiyo wewe unaunga mkono mtoto kunyimwa protini kwa sababu ya kufunga mkuu? Hebu tufafanulie vizuri isije ikwa tunamlaumu mama bila sababu ya msingi.
Sijahunga mkono hoja soma unielewe


Huyo mwanamke hajui dini yake vizuri amesahau kuna watu na situation mtu unapewa ruhusa kutokufunga
 
Si bora huyo keshazaliwa na ana uwezo wa kula vyakula mbadala, kuna wajazwazito wanafunga sijui kichanga kilichopo tumboni kinakula nn maskini

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
Huyo mama hajui maana ya mfungo kabisa
 
Nadhani hayupo sahihi. Mshitaki serikali ya mtaani.
Kwa Dini ya kiislamu mwanamke akijifungua inabidi mwanaume umlipe kukunyonyeshea mtoto wako atakuwa huyo hajalipwa mshahara wake ndio maana kagoma kunyonyesha
 
Angeuliza aijue sheria kwa wamama wenye watoto, sheria mtoto anatakiwa afikishe miaka miwili.
 
Amefanya kosa kumnyima ziwa mtoto,kama hawezi kufunga na kunyonyesha anatakiwa aache kufunga ili amnyonyeshe na hiyo funga atailipia hapo mbeleni
Exactly umeongea vizuri sana mkuu. Ubarikiwe sana.
 
Kama hujui labda tukusaidie hicho kipengele kipo kwenye talaka,kama umemtaliki mkeo halafu akajifungua Mtoto unaweza ukawa unamlipa ujira kwa ajili ya kukunyonyesha Mwanao. Usilamu kila kitu kiko wazi
Kwenye ishu ya talaka nimekuelewa vizuri sana mkuu. Je, kwenye ishu ya kumnyima mtoto ziwa wakati huu wa mfungo hili limekaaje?
 
Asante kwa ufafanuzi mkuu. Unaweza ukaweka katika lugha rahisi ili kila mdau aelewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…