Mama amteka mtoto wake ili apate milion 20 kutoka kwa mumewe

Mama amteka mtoto wake ili apate milion 20 kutoka kwa mumewe

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Dunia imeharibika sana. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mama mmoja amemteka mtoto wake wa miaka 3 na kumficha mtoto huyo kwa mama yake mzazi (bibi wa mtekwaji) ili kufanikisha mpango ovu wa kuvuna Tsh 20,000,000 kutoka kwa mume wake (baba wa mtekwaji).

Kufuatia utekahi huu, mkuu wa mkoa wa Mbeya, kwa kushirikiana na polisi, wamefanikiwa kuwanasa wahalifu wote, akiwemo mwanaume mmoja aliyekuwa akishirikiana na mama wa mtoto ili kujipatia kitita hicho bila jasho.

Hivi wanawake kweli wamefikia ukatili wa kiasi hiki? Huyu mwanamke hatifautiani na yule askari polisi aliyekula njama za kumuua mume wake kule Arusha ili anyakue mali zake. Wanawake wanajifanya wapole lakini wana roho mbaya zaidi ya nyoka. Mungu anawaona.

View: https://youtu.be/FSkfOIB4Gl0?si=XGRKpAJ71CD7p7OD
 
#HABARI Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili wanaohusika na tukio la kumteka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 5 mwanafunzi wa shule ya awali Isaiah Samartan iliyopo jijini Mbeya.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, DCP David Misime akiwa mkoani Kilimanjaro amesema baada ya kuripotiwa na baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye Layson Mkongwi, mfanya kazi wa kampuni binafsi huko jijini Mbeya alipokea simu kutoka kwa mtu asiyefahamika na kumweleza kuwa hatompa mtoto wake hadi atakapomtumia kiasi cha shilingi milioni ishirini.

"Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya walianza ufuatiliaji na mei 24 ,2024 majira ya saa nne usiku walifanikiwa kumkamata Winfred martin komba mwenye umri wa miaka 36 mngoni, mkazi wa vingunguti jijini Dar es salaam ambaye ndiye aliyekuwa akimpigia simu baba mzazi wa mtoto akimtisha asipotoa fedha hizo hatompa mtoto wake."

Baada ya kuhojiwa alieleza ni kweli walikula njama na mama mzazi wa mtoto huyo aitwaye Agness Jacob mwalubuli mkazi wa Isyesye Mbeya ili kujipatia kiasi hicho cha fedha.

"Pia alieleza baada ya kupanga njama hizo alifanikiwa kumchukua mtoto huyo mei 15 na kwenda kumficha kwa rafiki yake aitwaye Hamida Gaudience Njuu anaeishi jijini Mbeya, ufuatiliaji ulifanyika na mei 24 ,2024 majira ya saa saba kasoro usiku mtoto huyo alikutwa nyumbani kwa Hamida Gaudience njuu huko simike Mbeya."

Watuhumiwa hao ambao ni Winifred Martin Komba, Agness Jacob Mwalubuli na Hamida Gaudience Njuu wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwaajili ya kukamilisha taratibu nyingine ili wafikishwe mahakamani. #EastAfricaTV
 
Maoni ya mwanamke mmmoja haya hapachini
=======================
Hii ni story ya kweli, kina jamaa alinipa kazi yakumtafutia mke nikiwa University, for sure nilikosa . Nilimwona mmoja tu mwenye nidhamu. Wakati najipanga kumpa mrejesho kuwa Kuna niliyemwona, nikaletewa kadi ya mchango na yule Binti kuwa anaolewa.Nikanyoosha mikono na kumrudisha majibu kuwa nimemkosa katika wanachuo zaidi ya elfu kumi. Malezi yameharibu sana watoto wengi na bado yanaendelea kuharibu.Nawaonea hura sana vijana wanaotafuta wake na mateso watakayokumbana Nayo. Mimi Kwa Sasa ni mama nayaona magumu watakayoyapitia ila sioni namna yakuwasaidia. Mwenyezi mungu awanusuru vijana wote wa kiume na awape uso wa kuona haya vijana wote wa kike waache kuchetua akili🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Dunia imeharibika sana. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mama mmoja amemteka mtoto wake wa miaka 3 na kumficha mtoto huyo kwa mama yake mzazi (bibi wa mtekwaji) ili kufanikisha mpango ovu wa kuvuna Tsh 20,000,000 kutoka kwa mume wake (baba wa mtekwaji).

Kufuatia utekahi huu, mkuu wa mkoa wa Mbeya, kwa kushirikiana na polisi, wamefanikiwa kuwanasa wahalifu wote, akiwemo mwanaume mmoja aliyekuwa akishirikiana na mama wa mtoto ili kujipatia kitita hicho bila jasho.

Hivi wanawake kweli wamefikia ukatili wa kiasi hiki? Huyu mwanamke hatifautiani na yule askari polisi aliyekula njama za kumuua mume wake kule Arusha ili anyakue mali zake. Wanawake wanajifanya wapole lakini wana roho mbaya zaidi ya nyoka. Mungu anawaona.

Bila shaka huyu ni sungle mother....hawa wanawake wana matatizo sana
 
Back
Top Bottom