Kaka yake shetani
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 5,771
- 14,732
mama anaupiga mwingi kafungua fursa na maisha ni rahisi kwa sasa.ndio haya watu pesa hakuna mpaka kijiji cha nguruwe kimefunguliwa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili ni tatizo kubwa sana mkuu. Hadi wanawake wanekuwa na roho mbaya zaidi ya shetani, tena wake wa ndoa. Wanaume tutafika tukiwa tumechoka sana.mama anaupiga mwingi kafungua fursa na maisha ni rahisi kwa sasa.ndio haya watu pesa hakuna mpaka kijiji cha nguruwe kimefunguliwa
Usimlaumu huyo mama.maisha ni magumu na ndio yanaleta haya watu kubadilikaHili ni tatizo kubwa sana mkuu. Hadi wanawake wanekuwa na roho mbaya zaidi ya shetani, tena wake wa ndoa. Wanaume tutafika tukiwa tumechoka sana.
When a woman is fed up nothing you can do about it,wanakuwa sumu mbaya sana,kibaya zaidi wengi hawarudi nyuma...#HABARI Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili wanaohusika na tukio la kumteka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 5 mwanafunzi wa shule ya awali Isaiah Samartan iliyopo jijini Mbeya.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, DCP David Misime akiwa mkoani Kilimanjaro amesema baada ya kuripotiwa na baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye Layson Mkongwi, mfanya kazi wa kampuni binafsi huko jijini Mbeya alipokea simu kutoka kwa mtu asiyefahamika na kumweleza kuwa hatompa mtoto wake hadi atakapomtumia kiasi cha shilingi milioni ishirini.
"Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya walianza ufuatiliaji na mei 24 ,2024 majira ya saa nne usiku walifanikiwa kumkamata Winfred martin komba mwenye umri wa miaka 36 mngoni, mkazi wa vingunguti jijini Dar es salaam ambaye ndiye aliyekuwa akimpigia simu baba mzazi wa mtoto akimtisha asipotoa fedha hizo hatompa mtoto wake."
Baada ya kuhojiwa alieleza ni kweli walikula njama na mama mzazi wa mtoto huyo aitwaye Agness Jacob mwalubuli mkazi wa Isyesye Mbeya ili kujipatia kiasi hicho cha fedha.
"Pia alieleza baada ya kupanga njama hizo alifanikiwa kumchukua mtoto huyo mei 15 na kwenda kumficha kwa rafiki yake aitwaye Hamida Gaudience Njuu anaeishi jijini Mbeya, ufuatiliaji ulifanyika na mei 24 ,2024 majira ya saa saba kasoro usiku mtoto huyo alikutwa nyumbani kwa Hamida Gaudience njuu huko simike Mbeya."
Watuhumiwa hao ambao ni Winifred Martin Komba, Agness Jacob Mwalubuli na Hamida Gaudience Njuu wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwaajili ya kukamilisha taratibu nyingine ili wafikishwe mahakamani. #EastAfricaTV
Ameongezq ubunifu wake binafsi mkuuKwanini alambe kwa njia haramu siangetumia njia ya kawaida mkuu?
🤓🤓🤓🤓🤓Huyu mama ana tamaa kama miCCM.
Sasa tunayaona kwetu.Matukio yanayo fanana na haya tulikuwa tukisikia na kuyaona kwenye TV yakitokea kwa wenzetu