Mama anamtetea mke wangu pamoja na kunisaliti

Umenena vyema mkuu..Naamini amekuelewa
 
Wewe ni mkurya au mzanaki? N jibu
 
Mwisho wa uzinzi ni ndoa kuvunjwa. Hakuna kuishi na mtu mzinzi hata siku moja.
Yote nitavumilia lakini sio swala la uzinzi...
Na..... hili ndilo neno la Mungu.

Tumshukuru Mungu.
 
Ngoja sasa nikushauri....MPE chumba kimoja aishi kama mpangaji
 
Yaani wewe sijui uwekwe fungu gani

Upo busy kumkomoa mkeo bila kuangalia madhara kwa watoto

Uwaache watoto kwa dad yako yeye ndio aliyewazaa?

Huyo mkeo ni malaika hata asikosee????

Pyeee
 
MSAMEHE TU MAANA ametubu makosa yake na wewe umsamehe na kutubu pia na kanisani mwende KUPIGA MAGOTI na kutubu kwa kudhii!.
 
yani kweli ulishindwa mpa kipigo mpaka alale siku saba hospitali basi huyo bibie kashakuchora na hapo haondoki ng'oo
 
Kimsingi kwasababu ulikua na watoto naye; Ni wazi Umeonyesha UBINAFSI kupita kiasi, kwa kujali maugomvi yenu na kupuuza hisia zA watoto wenu. Umepoteza sifa zA kua baba mwema na bora. Huna legacy watoto wanafaa kuiga kutoka kwako. Kwa kumdhalilisha mama yao muda wote huo.. How dare are you?

Pia hujui furaha ya watoto wako, unadhani elimu na Pesa zako ndio kila kitu kwa malezi ya mtoto.

USIDANGANYIKe...Dada yako hawezi kua bora kama mama yao na wewe kwa malezi ya watoto wako.
Si Dada yako tu hata Ndugu zako wengine hawawezi kuwajali wanao kuliko wewe na mkeo.

Believe it or not watoto wako wameshaathirika tayari na tabia zenu.

Nakushauri Msamehe mkeo kwa uzinifu wake na si umsamehe ni bora msameheane manake wote mna makosa. Kisha muanze upya na watoto warudi home ImEDIATELY.


Kushindwa kusamehe sio UBINGWA wala sio UANAUME Bali ni Udhaifu mkubwa sana umeuonyesha kwa Mkeo, watoto na jamii inayokuzunguka.


Ukiwa kama mwanaume na baba wa familia, ulitakiwa kua imara kuchukia na kusamehe, ndio maana ya utu uzima.

Hata ukichukua mke mwingine watakumegea tena, na itakua tatizo juu ya matatizo. Je Utafukuza wangapi?

Tena mkeo anaonyesha ni stronger than you, Mara mia kuliko wewe pamoja na timbwilitimbwili unalomfanyia.

Usiwe dhaifu kwa Wanawake kiasi hicho. Watoto wanahitaji baba na mama. Be a good father by love their mother. Muda haurudi nyuma.
Hakuna Upendo mkubwa kama msamaha wa kosa lililo kubwa.
 
Umewah kuchapiwa mkuu?au nalainisha swali je umewah kusakitiwa?
 
Rahisi tu, maisha popote, hama nyumba kaanze maisha mapya sehemu nyingine bas
 
KWELI PESA SIO KILA KITU yaani mwanamke kaachiwa mshahara wote na kadi kapewa but kashindwa kujizuia kwa miezi 3 TU. Pole mwana! HATA MIMI NISINGESAMEHE
 
Ila kwa kuwa mimi ni.mkirsto na tumefundishwa kuomba msamaha na kusamehe na kwa jinsi ya hayo unayoyafanya but bado yupo kweli amejutia hayo aliyoyafanya so jaribu kurudisha moyo Ila naona adhabu umeitoa upande mmoja . je yule rafiki yako ulimfanyaje?
 
Naomba ufanye jambo kwa huyo rafiki yako bwege aliyekuharibia family yako, tafadhali!
 
Chief nilichomfanya rafiki yangu naomba kibaki siri yangu, maana najua nikisema mtaniona mnyama, hivyo itoshe tu ww kufahamu alipata adhabu kali kushinda ya huyo kahaba
 
KWELI PESA SIO KILA KITU yaani mwanamke kaachiwa mshahara wote na kadi kapewa but kashindwa kujizuia kwa miezi 3 TU. Pole mwana! HATA MIMI NISINGESAMEHE
Nashukuru umeliona hilo, napenda mawazo kama haya, yanatia moyo sana, nikisoma coments zenu nikakutana na coment inasema neno ""samehe"" yaani natamani huyo mtoa comment angekua mbele yangu nimtwange hata vichwa vitano kwa hasira

Kuna mtu kutoka kanisani kwa ex wife aliwahi kuja kunihubiri nimsamehe huyo kahaba nilimpiga huyo jamaa hawezi kusahau alikimbia bila Viatu akipiga kelele za kuomba msaada

Nikisoma neno msamaha nasikia kichefuchefu kikali sana, hivyo naomba watu wasiliandike kabisa hilo neno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…