Mama ananiingiza kwenye shimo la giza bila kujua

Mama ananiingiza kwenye shimo la giza bila kujua

mtetezi12

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
24
Reaction score
138
Kuna jambo ambalo linatatiza akili yangu mpaka nahisi kuchanganikiwa

Kuna siku moja mwaka jana mimi na mke wangu tulikuwa tumelala ilikuwa mida ya saa tano usiku simu ya mke wangu iliita nikapokea kwasababu yeye alikuwa tayari kwenye usingizi mzito nikasubiri aliyepiga aongee nikaona kimia akakata ilikuwa namba ambayo ilikuwa bila jina

Kama kawaida yangu ile namba nika save ndani ya simu yake na kwenda kuangalia kama ana whatsap ili nione picha yake kwa bahati nzuri alikuwa ameweka picha kwenye whatsap prifil yake nikamuona alafu nikapotezea asubuhi alivyoamuka nikamwambia kuna mtu ambaye alikuwa anakupigia simu usiku nime save namba yake kwa jina la sikujui akachukuwa simu yake akaona namba na kuniambia kijana uyo ni bodaboda wake nikapotezea sikutaka kumuuliza maswali mengi yakapita miezi kazaa sasa mwezi wa kwanza zilikuwa tariki 14 hivi nilirudi nyumbani kwa kushtukiza tu maana mke wangu anazoea mimi kurudi jioni nikakuta nyumbani kwangu kuna ugeni kijana mmoja hivi alikuwa sebuleni nilivyo muona tu

Nikamfananisha na kijana ambaye nilimuona kwenye profil picha ya yule kijana aliyepiga simu usiku wa siku ile yeye yupo sebuleni. na mke wangu alikuwa anapika jikoni alafu nguo ambazo alikuwa amevaa ni aibu kuvaa mbele ya mwanaume ambaye sio mume wake ndo alikuwa amevaa siku hiyo alivyoniona naingia tu ndani maana niliacha na salimia kijana uyo na kwenda zangu chumbani mara moja mke wangu akaja chumbani kule na kuja kuniambia kuwa yule kijana ni ndugu yake sijui ni mtoto wa shangazi yake yaani anajiongelesha wakati sijamuuliza chochote nilijibu sawa nikaenda pale tukawa tunaongea naye kama kawaida

Jioni niliomba simu yake nikaingia tu whatsap nikatafuta namba za yule boda wake kwenda kujihakikishia kweli kama yule boda ndo yule kijana ambaye mke wangu ananiambia ni ndugu yake au la kwa bahati nzuri nilikuta bado ile profil picha yake ipo nili screenshot picha ile na kujitumia kesho yake nilimtumia mke wangu picha ile pamoja na sms ambayo nilikuwa na muuliza tu kama yule boda wake na mtoto wa shangazi yake ni mapacha nilitumia njia hiyo kwasababu niliona nikimuuliza face to face tunaweza kufikia pabaya .

Hakujibu chochote sasa siku hiyo kipindi narudi tu home nikakuta mke wangu hayupo nilijaribu kumcheki kwenye simu alikuwa hapokei nikafikiri ametoka ameenda kwa mama maana mlango ulikuwa umefungwa. siku hiyo nilikuwa nipo tu home simu ya mama ikaingia nikapokea. Mama akaanza kunifokea eti mimi nimefukuza mke wangu na watoto wote kwangu nilishindwa kujibu nikaacha mama amalize kuongea alivyo maliza nilijaribu tena kumpigia simu mke hakupokea nikamuachia voici message alichojibu tu hataki tena kurudi nyumbani n nilishangaa sana mpaka nikashindwa na la kusema baada ya siku mbili nikamfuata mama kwenda kumwambia chanzo cha uyu mwanamke kuondoka cha kushangaza mama hakutaka hata kabisa kunisikiliza yeye anachojua mimi ndo nimefukuza mke wangu nimeiga tabia za faza sijui yaani najaribu

Kumuonyesha ukweli halisi ilikuwa vipi na sababu ya mke wangu kuondoka kwao lakini eee mzee mawazo yake tu ni mimi kurudisha mke wangu tulee watoto hayo mengine yeye hataki kabisa kusikia yeye kilio chake ni wajukuu wake kuishi na wazazi wao wote wawili tu basi haoni kabisa mwanae ananiingiza kwenye shimo mpaka wa leo mama hakanyangi kwangu wala kuongea na mimi mpaka pale mtakapo rudisha mke wangu ambaye aliondoka mwenyewe baada ya kujua nimejua uchafu wake ambao alikuwa anafanya
 
Mwanamke mpumbavu ataivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe! Achana naye! Akipigika atakucheki mwenyewe usijipe stress ndoa ni ya watu wawili hayamuhusu hata mama yako! Kama hawakuelewi wote kausha..!
 
Chukua hii, Ukishakua mwanaume kamwe asitokee mtu akakupangia jinsi ya kuishi hapa Duniani.

Unatakiwa kushauriwa tu, lkn mwenye maamuzi ya mwisho ni wewe na asikuingilie mtu.

Kuhusu huyo demu, ww piga kimya tu, endelea na mambo yako mpaka pale maumivu yatakapo pungua ndo utaamua kama ni talaka au vipi.

Kwanza huyo mwanamke ni sumu kabisa, hajajisumbua hata kuomba msamaha, yeye kaenda kupika majungu huko, ningekua mm simrudii hata iweje
 
We nenda kwa mzazi, moangilie ndombolo, mwambie kabisa, yeye anakujua nawe unajijua, kama kakuchoka anataka ufe kwa presha sawa, ama hataki kukuona uraiani anataka uishie jela, basi mwambie mama mwenyewe akakutafutie kesi ufungwe, kuliko kesi ya mauaji ambayo utaipata kwa kumchinja chinja huyo anaemuita mkwewe..

Kos ala usaliti ni STRAIGHT REDCARD haina mjadala, haina VAR
 
Back
Top Bottom