Mama ananiingiza kwenye shimo la giza bila kujua

Mama ananiingiza kwenye shimo la giza bila kujua

Kuna jambo ambalo linatatiza akili yangu mpaka nahisi kuchanganikiwa

Kuna siku moja mwaka jana mimi na mke wangu tulikuwa tumelala ilikuwa mida ya saa tano usiku simu ya mke wangu iliita nikapokea kwasababu yeye alikuwa tayari kwenye usingizi mzito nikasubiri aliyepiga aongee nikaona kimia akakata ilikuwa namba ambayo ilikuwa bila jina

Kama kawaida yangu ile namba nika save ndani ya simu yake na kwenda kuangalia kama ana whatsap ili nione picha yake kwa bahati nzuri alikuwa ameweka picha kwenye whatsap prifil yake nikamuona alafu nikapotezea asubuhi alivyoamuka nikamwambia kuna mtu ambaye alikuwa anakupigia simu usiku nime save namba yake kwa jina la sikujui akachukuwa simu yake akaona namba na kuniambia kijana uyo ni bodaboda wake nikapotezea sikutaka kumuuliza maswali mengi yakapita miezi kazaa sasa mwezi wa kwanza zilikuwa tariki 14 hivi nilirudi nyumbani kwa kushtukiza tu maana mke wangu anazoea mimi kurudi jioni nikakuta nyumbani kwangu kuna ugeni kijana mmoja hivi alikuwa sebuleni nilivyo muona tu

Nikamfananisha na kijana ambaye nilimuona kwenye profil picha ya yule kijana aliyepiga simu usiku wa siku ile yeye yupo sebuleni. na mke wangu alikuwa anapika jikoni alafu nguo ambazo alikuwa amevaa ni aibu kuvaa mbele ya mwanaume ambaye sio mume wake ndo alikuwa amevaa siku hiyo alivyoniona naingia tu ndani maana niliacha na salimia kijana uyo na kwenda zangu chumbani mara moja mke wangu akaja chumbani kule na kuja kuniambia kuwa yule kijana ni ndugu yake sijui ni mtoto wa shangazi yake yaani anajiongelesha wakati sijamuuliza chochote nilijibu sawa nikaenda pale tukawa tunaongea naye kama kawaida

Jioni niliomba simu yake nikaingia tu whatsap nikatafuta namba za yule boda wake kwenda kujihakikishia kweli kama yule boda ndo yule kijana ambaye mke wangu ananiambia ni ndugu yake au la kwa bahati nzuri nilikuta bado ile profil picha yake ipo nili screenshot picha ile na kujitumia kesho yake nilimtumia mke wangu picha ile pamoja na sms ambayo nilikuwa na muuliza tu kama yule boda wake na mtoto wa shangazi yake ni mapacha nilitumia njia hiyo kwasababu niliona nikimuuliza face to face tunaweza kufikia pabaya .

Hakujibu chochote sasa siku hiyo kipindi narudi tu home nikakuta mke wangu hayupo nilijaribu kumcheki kwenye simu alikuwa hapokei nikafikiri ametoka ameenda kwa mama maana mlango ulikuwa umefungwa. siku hiyo nilikuwa nipo tu home simu ya mama ikaingia nikapokea. Mama akaanza kunifokea eti mimi nimefukuza mke wangu na watoto wote kwangu nilishindwa kujibu nikaacha mama amalize kuongea alivyo maliza nilijaribu tena kumpigia simu mke hakupokea nikamuachia voici message alichojibu tu hataki tena kurudi nyumbani n nilishangaa sana mpaka nikashindwa na la kusema baada ya siku mbili nikamfuata mama kwenda kumwambia chanzo cha uyu mwanamke kuondoka cha kushangaza mama hakutaka hata kabisa kunisikiliza yeye anachojua mimi ndo nimefukuza mke wangu nimeiga tabia za faza sijui yaani najaribu

Kumuonyesha ukweli halisi ilikuwa vipi na sababu ya mke wangu kuondoka kwao lakini eee mzee mawazo yake tu ni mimi kurudisha mke wangu tulee watoto hayo mengine yeye hataki kabisa kusikia yeye kilio chake ni wajukuu wake kuishi na wazazi wao wote wawili tu basi haoni kabisa mwanae ananiingiza kwenye shimo mpaka wa leo mama hakanyangi kwangu wala kuongea na mimi mpaka pale mtakapo rudisha mke wangu ambaye aliondoka mwenyewe baada ya kujua nimejua uchafu wake ambao alikuwa anafanya
Samahani mkuu, but inaonekana bi mkubwa wako alikuwa anamcheat mshua wako ndo maana hapo anakwambia unataka kuwa kama faza wako. So kwake kucheat anaona kawaida maana ndio ilikuwa tabia yake kwa mshua.
 
Pale ambapo mapenzi hutuzidi ujazo halisi. Mkuu hakikisha mwanamke anakupenda wewe ili iwe rahisi kumumudu, tatizo huanzia mwanamme ndio akampenda zaidi mwanamke.

Mama yako mpende na kumheshimu ila katika issue za mahusiano mhusishe baba ambae ni mwanaume mwenzio
 
mwanae ananiingiza kwenye shimo mpaka wa leo mama hakanyangi kwangu wala kuongea na mimi mpaka pale mtakapo rudisha mke wangu ambaye aliondoka mwenyewe baada ya kujua nimejua uchafu wake ambao alikuwa anafanya
Mkeo aligongwa na bodaboda mkuu, pole sana hawa bodaboda wanawamaliza sana wake za watu
 
Mama yako mpende na kumheshimu ila katika issue za mahusiano mhusishe baba ambae ni mwanaume mwenzio
Ndio kweli upo sahihi ila hapo inaonekana huyo malaya kakimbilia kwa mama yake na unaweza kuta hata hao watoto jamaa sio wa kwake kabisa na huko alipokimbilia kwa mama yake huyo bodaboda anaenda kujipigia hukohuko hata akirudi kashakamuliwa sana, presha za nini wazee kwani tukifa si tunaiacha hapa au tunazikwa nayo?
 
Kosa kubwa sana ulilofanya ni siku ile ulipomkuta huyo kwako na ukakubali kudanganywa
Jamaa ni mdebwedo sana au tuseme ni mpole kupitiliza mpaka mkewe anamdharau!
Hivi kwa hali ya kawaida umerudi nyumbani unakuta njemba ambalo unahisi kabisa linamtafunaga mkeo eti unarelax kabisa !
Tena si ajabu jamaa walikula chakula pamoja mezani halafu muda wa kulala likatandikiwa na kitanda kabisa likalala hapo halafu asubuhi jamaa akaenda kazini akawaachia uwanja wakiwashe cha asubuhi😀
 
"na dediketi kwako kibao cha bizzman"
aseh kumbe kuna watu unaeza kutana nao road wako smart kimavazi lkn kichwan box yam unataka uingie kweny tanuri la jahanam et kisa kumsikiliza mtu et mama mama mama aseh...hapo hujaoa mke bali umeoa malaya
 

Achana Na Mambo Ya Kuumizana Kichwa,,Na Mtu/Watu Wazima....Yapo Mambo Mengi Sana Ya Msingi Na Ya Maana Mnoo,Yakufanya Kwa Ajili Ya Ustawi Wako Akili,,Mwili,,Na Roho....###MaraBoda###MaraMtotoWaShangazi###​
 
Samahani mkuu, but inaonekana bi mkubwa wako alikuwa anamcheat mshua wako ndo maana hapo anakwambia unataka kuwa kama faza wako. So kwake kucheat anaona kawaida maana ndio ilikuwa tabia yake kwa mshua.
💯🎯
 
Back
Top Bottom