Mama ananiingiza kwenye shimo la giza bila kujua

Mama ananiingiza kwenye shimo la giza bila kujua

Kiliwahi kunikuta kitu kama hiki mke nilimfumania kwao na mchungaji mmoja hivi wa TAG live kabisa aisee Kibao kikanigeukia mimi...chakushangaza wazazi wangu na ndugu zangu wanadai nimsamehe tulee mtoto licha ya kuwasimulia mikasa mingi ya usaliti wa yule malaya.Ila kwakuwa maisha ni yangu nikafanya maamuzi magumu nikampiga chini mwanamke na nikatafuta mwingine bila kumuhusisha yeyote yule nikakaa mwaka nimekata mawasiliano nao na hawamjui mke niliyemuoa
Ulifanya vyema
Nikiwa mkubwa nitapenda niwe kama wewe mkuu
 
Kiliwahi kunikuta kitu kama hiki mke nilimfumania kwao na mchungaji mmoja hivi wa TAG live kabisa aisee Kibao kikanigeukia mimi...chakushangaza wazazi wangu na ndugu zangu wanadai nimsamehe tulee mtoto licha ya kuwasimulia mikasa mingi ya usaliti wa yule malaya.Ila kwakuwa maisha ni yangu nikafanya maamuzi magumu nikampiga chini mwanamke na nikatafuta mwingine bila kumuhusisha yeyote yule nikakaa mwaka nimekata mawasiliano nao na hawamjui mke niliyemuoa
Vipi now mawasiliano nao yamerudi !?

Mimi nataka nikae hata milele bila mawasiliano nao ndugu wengine ni Cancer
 
Huyo mkeo nae ni mama imagine watoto wako wakaja kumuendekeza na kusikiliza ushauri wa mama yao ambae ni huyo mkeo

Tukubaliane kua kuna watu tunazaliwa na wamama wasio na busara,maadili, tunapokua wakubwa na wenye akili timamu tusiwaendekeze watatupoteza
 
Pale ambapo mapenzi hutuzidi ujazo halisi. Mkuu hakikisha mwanamke anakupenda wewe ili iwe rahisi kumumudu, tatizo huanzia mwanamme ndio akampenda zaidi mwanamke.

Mama yako mpende na kumheshimu ila katika issue za mahusiano mhusishe baba ambae ni mwanaume mwenzio

Inakuaje baba ahusike kwenye Familia ambayo sio yake? Hatuwezi kufanya maamuzi mpaka wazazi wahusike.
 
Kiliwahi kunikuta kitu kama hiki mke nilimfumania kwao na mchungaji mmoja hivi wa TAG live kabisa aisee Kibao kikanigeukia mimi...chakushangaza wazazi wangu na ndugu zangu wanadai nimsamehe tulee mtoto licha ya kuwasimulia mikasa mingi ya usaliti wa yule malaya.Ila kwakuwa maisha ni yangu nikafanya maamuzi magumu nikampiga chini mwanamke na nikatafuta mwingine bila kumuhusisha yeyote yule nikakaa mwaka nimekata mawasiliano nao na hawamjui mke niliyemuoa

Huu ndo uanaume sasa...

Watu wanaweza kushinikiza kusamehe, ila katika same situations wao hawawez kusamehe
 
Kuna jambo ambalo linatatiza akili yangu mpaka nahisi kuchanganikiwa

Kuna siku moja mwaka jana mimi na mke wangu tulikuwa tumelala ilikuwa mida ya saa tano usiku simu ya mke wangu iliita nikapokea kwasababu yeye alikuwa tayari kwenye usingizi mzito nikasubiri aliyepiga aongee nikaona kimia akakata ilikuwa namba ambayo ilikuwa bila jina

Kama kawaida yangu ile namba nika save ndani ya simu yake na kwenda kuangalia kama ana whatsap ili nione picha yake kwa bahati nzuri alikuwa ameweka picha kwenye whatsap prifil yake nikamuona alafu nikapotezea asubuhi alivyoamuka nikamwambia kuna mtu ambaye alikuwa anakupigia simu usiku nime save namba yake kwa jina la sikujui akachukuwa simu yake akaona namba na kuniambia kijana uyo ni bodaboda wake nikapotezea sikutaka kumuuliza maswali mengi yakapita miezi kazaa sasa mwezi wa kwanza zilikuwa tariki 14 hivi nilirudi nyumbani kwa kushtukiza tu maana mke wangu anazoea mimi kurudi jioni nikakuta nyumbani kwangu kuna ugeni kijana mmoja hivi alikuwa sebuleni nilivyo muona tu

Nikamfananisha na kijana ambaye nilimuona kwenye profil picha ya yule kijana aliyepiga simu usiku wa siku ile yeye yupo sebuleni. na mke wangu alikuwa anapika jikoni alafu nguo ambazo alikuwa amevaa ni aibu kuvaa mbele ya mwanaume ambaye sio mume wake ndo alikuwa amevaa siku hiyo alivyoniona naingia tu ndani maana niliacha na salimia kijana uyo na kwenda zangu chumbani mara moja mke wangu akaja chumbani kule na kuja kuniambia kuwa yule kijana ni ndugu yake sijui ni mtoto wa shangazi yake yaani anajiongelesha wakati sijamuuliza chochote nilijibu sawa nikaenda pale tukawa tunaongea naye kama kawaida

Jioni niliomba simu yake nikaingia tu whatsap nikatafuta namba za yule boda wake kwenda kujihakikishia kweli kama yule boda ndo yule kijana ambaye mke wangu ananiambia ni ndugu yake au la kwa bahati nzuri nilikuta bado ile profil picha yake ipo nili screenshot picha ile na kujitumia kesho yake nilimtumia mke wangu picha ile pamoja na sms ambayo nilikuwa na muuliza tu kama yule boda wake na mtoto wa shangazi yake ni mapacha nilitumia njia hiyo kwasababu niliona nikimuuliza face to face tunaweza kufikia pabaya .

Hakujibu chochote sasa siku hiyo kipindi narudi tu home nikakuta mke wangu hayupo nilijaribu kumcheki kwenye simu alikuwa hapokei nikafikiri ametoka ameenda kwa mama maana mlango ulikuwa umefungwa. siku hiyo nilikuwa nipo tu home simu ya mama ikaingia nikapokea. Mama akaanza kunifokea eti mimi nimefukuza mke wangu na watoto wote kwangu nilishindwa kujibu nikaacha mama amalize kuongea alivyo maliza nilijaribu tena kumpigia simu mke hakupokea nikamuachia voici message alichojibu tu hataki tena kurudi nyumbani n nilishangaa sana mpaka nikashindwa na la kusema baada ya siku mbili nikamfuata mama kwenda kumwambia chanzo cha uyu mwanamke kuondoka cha kushangaza mama hakutaka hata kabisa kunisikiliza yeye anachojua mimi ndo nimefukuza mke wangu nimeiga tabia za faza sijui yaani najaribu

Kumuonyesha ukweli halisi ilikuwa vipi na sababu ya mke wangu kuondoka kwao lakini eee mzee mawazo yake tu ni mimi kurudisha mke wangu tulee watoto hayo mengine yeye hataki kabisa kusikia yeye kilio chake ni wajukuu wake kuishi na wazazi wao wote wawili tu basi haoni kabisa mwanae ananiingiza kwenye shimo mpaka wa leo mama hakanyangi kwangu wala kuongea na mimi mpaka pale mtakapo rudisha mke wangu ambaye aliondoka mwenyewe baada ya kujua nimejua uchafu wake ambao alikuwa anafanya
*** off ndoa ni ungese sana
 
Vipi now mawasiliano nao yamerudi !?

Mimi nataka nikae hata milele bila mawasiliano nao ndugu wengine ni Cancer
Walinitafuta wao wenyewe na sio mimi kuwatafuta wao...hivi waza mkuu unakuta mkeo analiwa live hata kama ni kwao mke halafu mtu anakuletea eti ushauri wa oooh samehe tu muleee mtoto....nikwamba nilichojifunza maishani mke akianza kuchepuka fanya maamuzi haraka
 
Mistake ya kwanza ni kuruhusu dogo akae sebuleni huku akiandaliwa pishi na mkeo, hiyo ni dharau kubwa
 
Back
Top Bottom