Mama awashinda watoto wake Kesi ya Mirathi ya Nyumba Kariakoo

Mama awashinda watoto wake Kesi ya Mirathi ya Nyumba Kariakoo

Dini yenu ndo inasema mali alizotafuta baba na mama.. baba akifariki mali wanapewa watoto??? Bhasi hiyo dini ni takatakaaa.
Kila mtu anapata mgao wake,mama anapata 1/8.Yaani mali inagaiwa mafungu 8,fungu moja anapewa mama,iliyobakiya wanagaiwa watoto na wazazi wa marehemu kama wako hai,kila mmoja anakuwa na sehemu yake Hili somo la mirathi,ni somo kamili.Na kabla ya kugawana,kwanza kunalipwa madeni,anayodaiwa marehemu,kama alijenga kwa mkopo wa benki,mpaka anafariki mkopo haujalipwa.Au kuna wanaomdai,wakiwa na vithibitisho vya maandishi.
 
Yaani watoto wanashitakiana na mama yao ,hivi hao wangese wanajielewa kwelii
 
Vipi kama miaka 25 nyuma ,mama alitaka kuolewa na mwanaume mwingine na kutaka kuishi nae hapo nyumbani baada ya Baba wa watoto kufariki...?

Vipi kama mgogoro wao ulianzia hapo?
 
Wajukuu ni watoto wa wanawe ambao anagombana nao mahakamani
Wajukuu wote sidhani kama walikuwa wanakubaliana na maamuzi ya wazazi wao kutaka, kumsumbua Bibi Yao. Hii habari ya "Samaki mmoja akioza wote wameoza" ni habari ya madalali kutaka kumuumiza mwenye mzigo kwenye bei.
 
Kizazi chake kishakuwa batili Bora ampe Mungu kama wototo wote wameunga kumuumiza mama Yao hapo hamna kizazi tena
Mkuu kwa kweli siungi Mkono hoja yako kwa sababu hoja yako imejikita kwenye lugha ya madalali kutaka kuwaumiza wenye bidhaa, ni Ile lugha ya "Samaki mmoja akioza wote wameoza"
 
Mkuu kwa kweli siungi Mkono hoja yako kwa sababu hoja yako imejikita kwenye lugha ya madalali kutaka kuwaumiza wenye bidhaa, ni Ile lugha ya "Samaki mmoja akioza wote wameoza"
Hapana kwasababu wajukuu ni watoto wa watesi wake uhuenda walikuwa wanaunga mkono unyama wa babazao
 
Hyo sheria yako au yenu baki nayo kwanza.. sheria za nchi ndo zimempa mams haki.. mali ya mume ni ya mke pia. Hapa hatupo kwenye nchi inayotumia sheria za dini ndgu.
Zanzibar wao wanatumia sheria za kiarabu.
 
Kila mtu anapata mgao wake,mama anapata 1/8.Yaani mali inagaiwa mafungu 8,fungu moja anapewa mama,iliyobakiya wanagaiwa watoto na wazazi wa marehemu kama wako hai,kila mmoja anakuwa na sehemu yake Hili somo la mirathi,ni somo kamili.Na kabla ya kugawana,kwanza kunalipwa madeni,anayodaiwa marehemu,kama alijenga kwa mkopo wa benki,mpaka anafariki mkopo haujalipwa.Au kuna wanaomdai,wakiwa na vithibitisho vya maandishi.
Assume wazazi wa marehemu (baba) nao walishafariki kabla yake, marehemu kaacha mjane mmoja na mtoto mmoja, na nyumba haikuwa na deni lolote; hapo ratio ya mgao bado inabaki 1/8 kwa mama? Kwamba mtoto ana haki kuliko mama? Kama mama alishiriki kuitafuta mali, nyumba say, ratio inakuwaje? Kama mama ndiye katangulia kwanza na kaacha watoto wasiokuwa wa baba, ratio ya baba inakuwaje? Haya mambo ni very complex.
 
Vipi kama miaka 25 nyuma ,mama alitaka kuolewa na mwanaume mwingine na kutaka kuishi nae hapo nyumbani baada ya Baba wa watoto kufariki...?

Vipi kama mgogoro wao ulianzia hapo?
Suppose ingekuwa kinyume chake; katangulia mama, baba anataka kuoa mke mwingine na aishi naye hapo? Mtoto hana uhalali wowote wa kuingilia mahusiano ya mzazi wake kwani naye ni matokeo ya mahusiano hayo hayo!

Hata hivyo, busara ni mzazi kutoolewa/olea hapo hapo but it is not sheria kwani ni mali yake at least kwa sheria za nchi.
 
Mrungi unazingua sana jogoo kwenye show
Unaweza ukawa sahihi namna fulani na wrong namna fulani.

Sasa mtu unachanja pisi nzima unategemea utapiga show?

Kama una show piga nusu ruba, pata andas la kiasi afu nenda kwenye show utanishukuru kesho, hiyo show yake sio ya kitoto
 
SHow na busta madhara ni makubwa sana bdae zingatia hilo
 
Unaleta ujuaji na huruma za hivyo...huyo mama haki yake katika mirathi ni kupewa thumni ya mali zote za urithi(yaani kama sijakosea anatakiwa apewe theluthi ya mali yote) na sio kupewa mali yote yeye kama mke au mama wa hao watoto....daraja la mama ni kubwa lakini aliweka hilo daraja ndio huyo huyo aliyempa haki ya kupata thumni katika urithi,kama alitaka haki yake basi wangekusanya mali zote kama zinauzwa halafu yeye apewe theluthi tu ndio haki yake......usilete huruma za kibidamu Mwenyezi Mungu kisha fafanua kila kitu....tamaa za hiyo familia wameshindwa kugawana mirathi kwa sheria za Mwenyezi Mungu wamekimbilia mahakamani hatimae limegeuka hata huyo mama kapewa tu lakini ataadhibiwa kwa kudhulumu haki za watu.
Pure Insanity!

Ipo siku Muslim women watasimama na kulidai hilo “daraja la juu” mnalopenda kulisema sana huku vitendo ni tofauti.

Kwamba Mungu hatambui kabisa mchango wa nyama, damu na mifupa aliyotoa mama katika Maisha yake yote ya ndoa kiasi malipo yake ni “thumni” ya mali zake yeye na mume wake mwenyewe?!

A day will come. InshaAllah.
 
Vipi kama miaka 25 nyuma ,mama alitaka kuolewa na mwanaume mwingine na kutaka kuishi nae hapo nyumbani baada ya Baba wa watoto kufariki...?

Vipi kama mgogoro wao ulianzia hapo?
Kwani mahusiano ya kingono ya mama yao yanawahusu nini?

Halafu baba angefanya hivyo baada ya mama yao kufariki wangethubutu?
 
Kwani mahusiano ya kingono ya mama yao yanawahusu nini?

Halafu baba angefanya hivyo baada ya mama yao kufariki wangethubutu?
Kwa mfano...

Angalia umri wa huyo mama ,rudisha 25 nyuma ....alikuaje pengine kiasi Cha kuanzisha mfano mahusiano ya kingono na mtu kwenye nyumba alioacha Baba yao ambayo ni kama nyumba yao maana Cha Baba yao ndo chao na wala sio Cha mama yao SI chao... .........unaona inakaa poa au sio ?

Watu hurithi vya Baba yao SI kwa mama yao ......Ndo maana wala kusingekua na hio purukushani .sababu Mali ingekua bado ipo kwa mwenye nayo...(Kwao)

Hata hivyo SI kawaida kukosekana upendo kiasi hicho kati ya mama na watoto .....tena mama mzazi.......naamini Kuna fitna Kali Sana imepenyezwa katikati yao ........na wasioitakia familia mema......
Bondi ya mama na watoto huwa ni strong Sana lakini mpaka ilofikiwa haikuwa nzuri ......nafikiri Kuna kitu hakijawekwa wazi hapo .....so tusijudge Sana ......

Tuweke Akiba ya maneno..
 
Angalia umri wa huyo mama ,rudisha 25 nyuma ....alikuaje pengine kiasi Cha kuanzisha mfano mahusiano ya kingono na mtu kwenye nyumba alioacha Baba yenu ambayo ni kama nyumba aliewaachia Baba yenu .........unaona inakaa poa au sio ?
Haijalishi. Personal relations za mama Yao haziwahusu sawa na ambavyo baba Yao angeleta mama mdogo humo ndani endapo mama angetangulia.

Watu hurithi vya Baba yao SI kwa mama yao ......Ndo maana wala kusingekua na hio purukushani .......
Huyo baba bila huyo mama hao watoto wangetoka hewani?!

Jamii (hasa ya kiume) Bado imegoma kutambua thamani, umuhimu na mchango wa mwanamke/mama katika jamii kwa ujumla wake. Maumivu yatandelea mpaka ieleweke.
 
Back
Top Bottom