1. Watoto walifungua mirathi. Hawakumjumuisha mama yao kwenye orodha ya warithi.
Hivyo, Mama akawa nje ya warithi. Akaondolewa kwenye mirathi.
2. Mama akapinga hilo. Akataka nayeye awe miongoni mwa warithi.
3. Mama ameshinda kesi. Mahakama imeona kuwa mama huyo nayeye ana haki kwenye mirathi hiyo. Mama amerejeshwa kwenye mirathi. Anakuwa miongoni mwa warithi.
N.B: Watoto wapo 6. Kati ya hao sita, ni mtoto mmoja tu ndiye alikuwa upande wa mama akimtetea ajumuishwe kwenye mirathi. Watoto wengine 5 walikuwa hawataki mama awe kwenye mirathi. 😎
-Kaveli-