Mama awashinda watoto wake Kesi ya Mirathi ya Nyumba Kariakoo

Mama awashinda watoto wake Kesi ya Mirathi ya Nyumba Kariakoo

Haijalishi. Personal relations za mama Yao haziwahusu sawa na ambavyo baba Yao angeleta mama mdogo humo ndani endapo mama angetangulia.

Huyo baba bila huyo mama hao watoto wangetoka hewani?!

Jamii (hasa ya kiume) Bado imegoma kutambua thamani, umuhimu na mchango wa mwanamke/mama katika jamii kwa ujumla wake. Maumivu yatandelea mpaka ieleweke.
Sawa.
 
Fatma Awadh mkazi wa Kariakoo amemshukuru Rais Samia na aliyekuwa waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Silaa (sasa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari) baada ya kushinda kesi ya Mirathi ya Nyumba dhidi ya watoto wake.

Kesi hiyo iliyoanza 2006 imepata majibu baada ya kudumu mahakamani kwa miaka 18 ambapo Mama amewashinda watoto wake kwenye Mirathi ya nyumba iliyopo Kariakoo Dar es salaam.
View attachment 3170874
Kesi Miaka 18 ?..
 
Watoto wanagombania Mali na mama mzazi ! Au mama wa kufikia au mama wa kambo

Vyovyote vile Ila haileti maana ni aina fulani ya familia za kijinga .kuanzia Mama MTU na watoto .
 
Uswahilini kuna mambo mengi ambayo mengine kama hayajaripotiwa kama hivi hauwezi kuyajua. Imagine mtu mwenye akili timamu unasimama mahamakani kutaka umdhulumu mama yako mzazi nyumba ambayo pengine unaweza kuhonga au kutumia hila kushinda kesi alaf baada ya siku mbili nyumba hiyo inaanguka na kuuwa watu kama ile iliyoua na kujeruhi watu juzikati hapo kariakoo.
Una hakika ni mama yao mzazi!
Kwani mtu ukimuita mama ni lazima awe amekuweka tumboni miezi 9?
 
Fatma Awadh mkazi wa Kariakoo amemshukuru Rais Samia na aliyekuwa waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Silaa (sasa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari) baada ya kushinda kesi ya Mirathi ya Nyumba dhidi ya watoto wake.

Kesi hiyo iliyoanza 2006 imepata majibu baada ya kudumu mahakamani kwa miaka 18 ambapo Mama amewashinda watoto wake kwenye Mirathi ya nyumba iliyopo Kariakoo Dar es salaam.
View attachment 3170874
Hatari sana.
 
Kila mtu anapata mgao wake,mama anapata 1/8.Yaani mali inagaiwa mafungu 8,fungu moja anapewa mama,iliyobakiya wanagaiwa watoto na wazazi wa marehemu kama wako hai,kila mmoja anakuwa na sehemu yake Hili somo la mirathi,ni somo kamili.Na kabla ya kugawana,kwanza kunalipwa madeni,anayodaiwa marehemu,kama alijenga kwa mkopo wa benki,mpaka anafariki mkopo haujalipwa.Au kuna wanaomdai,wakiwa na vithibitisho vya maandishi.
mpaka wazazi wa marehemu??? hivi unajitambua wee kijanaa..
 
Watoto wanagombania Mali na mama mzazi ! Au mama wa kufikia au mama wa kambo

Vyovyote vile Ila haileti maana ni aina fulani ya familia za kijinga .kuanzia Mama MTU na watoto .

Haya Man si ungepata sikiliza au soma kidunchu

Hayajakukuta yanayowakuta

Mama mzazi huyo
 
Acha ujinga wewe, hao ni watoto wake wa kuzaa, wamekaa tumboni kwake miezi 9, hivyo kama kudhulumu angewadhulumu wakati akiwa hajawazaa kwa kutoa mimba zao.

Hivi unaijua thamani ya mzazi uliekaa tumboni kwake miezi 9? Je akiwarudishia hiyo mirathi akawaomba na wao wamlipe kwa kukaa tumboni kwao miezi 9 halafu ndo wamzae kama alivyowazaa wao wataweza?

Bila yeye kuwazaa au kuwalea mpaka wakakuwa wakubwa hiyo mali wangeweza kuirithi? Yani mali au nyumba ndio isababishe ukasimame na mama yako mzazi mahakamani? Nyumba inaweza kuungua au ikaanguka kama lilivyoanguka lile jengo la juzi hapo kariakoo lkn mzazi atabaki kuwa mzazi miaka yote ya maisha yenu iwe kwa raha au kwa shida.
Ukiona hivyo jua mama ana watoto wengine nje ya hao na baba yao aliaacha amewarithisha.
 
Fatma Awadh mkazi wa Kariakoo amemshukuru Rais Samia na aliyekuwa waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Silaa (sasa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari) baada ya kushinda kesi ya Mirathi ya Nyumba dhidi ya watoto wake.

Kesi hiyo iliyoanza 2006 imepata majibu baada ya kudumu mahakamani kwa miaka 18 ambapo Mama amewashinda watoto wake kwenye Mirathi ya nyumba iliyopo Kariakoo Dar es salaam.
View attachment 3170874
Ndio hasara ya kufuga matoto badala ya kulea wapate akili za kutafuta za kwao.
 
Back
Top Bottom