Mama Diamond: Mzee Abdul alinikuta nina mimba ya Naseeb (Diamond) na aliikataa. Ricardo Momo na Diamond ni ndugu, baba yao ni Salum Idd Nyange

Mama Diamond: Mzee Abdul alinikuta nina mimba ya Naseeb (Diamond) na aliikataa. Ricardo Momo na Diamond ni ndugu, baba yao ni Salum Idd Nyange

Mzee Nyange alikataa mimba, mzee Abdul nae akakataa mimba lakini akaendelea kujivinjari na mama Diamond.

Kwa maelezo ya mama Diamond amelea mwenyewe. Kasema mzee Abdul tangu akatae mimba hakuwahi jishughulisha na matunzo ya mtoto na akasisitiza japo walikua pamoja yeye aliendelea kumlea mwanae mwenyewe hadi walipotengana

Wanaume mjue tuu wanawake ni wavumilivu lakini kuna point wakifika wanakua wabaya kuliko ubaya wenyewe!!!!! Yaani Mungu alipowaambiwa muishi na wanawake kwa akili na hii ndio maana yake🙌🙌🙌
Kwa hiyo mzee Abdul alikuwa anateleza ,so Diamond ni mluguru wa Morogoro na si mmanyema.
 
Ka-panick kivipi?! Ina maana ka-react hizi habari, au?!
Mzee kaongea hadi mambo ya kitandani, mwisho Kasema diamond akiendelea kutumia jina lake atamshtaki
 
Wao ndio walioanza kumtumia kwenye kiki zao nae akajitokeza kukoleza mambo ona sasa wanayakuza. Wale wanaodiss single mothers hapa watajipatia point muhimu. Mzee alimkubali mama domo akiwa na esma kumbe akabambikiziwa hadi mimba
Na amesema waache kutumia jina lake atawapeleka mahakamani

Ila yalianza zamani kumbe

View attachment 1678269
 
Alisepa kama ambavyo huwa wanasepa mababa wengi, na akarudi kama ambavyo huwa wanarudi mababa wengi! Itakuwa alisepa enzi anaitwa Naseeb, akaja kurudi enzi anaitwa Diamond!! Hivi huoni hata bond ya Diamond na Queen Darleen ni kama ya ku-force tu?! I don't see any affection kutoka kwa Diamond kwenda kwa QD kama ile aliyonayo kwa Esma! Sijawahi kuona wala kusikia Diamond akiwatolea watu povu kuhusu QD lakini mara kibao tu huwa anatoa kwa ajili ya Esma!
Bond ya Diamond na Queen imetengenezwa na mama yake Queen na mama Diamond sababu wote inavyo onekana mzee Abdul hakuwa na time nao,so walivyokuwa wakikutana walikuwa wanafarijiana sababu matatizo yao yanafanana.
 
Kwa hiyo mzee Abdul alikuwa anateleza ,so Diamond ni mluguru wa Morogoro na si mmanyema.
OMG! OMG! OMG! OMG! Hivi unajua kwanini nimeweka hizo OMG nyingi?! Kwanza ndo unanijuza kwamba Nyange ni Waluguru! Pili, nakumbuka kuna siku Diamond kulikuwa na event fulani hivi Morogoro akasema "hapa ni home" lakini watu hawakutilia maanani!!!
 
Habar wanajf,


Aliyesema kuwa wanawake na mama zetu tusiwaamini hakukosea leo kwani huenda wazazi wetu wa kiume walio tulea sio baba zetu.

Leo Rikardo Momo amesema kuwa mzee Abdul sio baba yake Diamond na kusema kuwa yeye na Diamond wanachangia baba na baba yao anaitwa Mzee Salim Nyange.

Haya yote yanaweza kuwa sawa lakini kwanini Diamond anaitwa Naseeb Abdul na siyo Salim Naseeb Nyange? Hivi inawezekana baba mlezi kupewa hadhi ya ubin wa mtoto au ndio mama Diamond anataka amalize mchezo?

Na kama ni kweli Mzee Abdul sio baba yake Diamond huenda mama Diamond alikataliwa hii mimba na mzee Salim Nyange akaamua kumtupia zigo mzee Abdul na bila shaka mzee alikubali kiroho safi ila huenda alikuwa anaambiwa mengi na ndugu pamoja na rafiki.

Apa hii story sioni kama ina utofauti na story iliyopo kwenye mziki wa Stamina na Profesa Jay maana namuona Diamond anamlaumu Mzee Abdul kwa kutokumlea ilihali Mzee Abdul alijua Diamond siyo mwanae na bado akaendelea kuwa baba kwa uwezo wake.

Ila sijaamini kama Mzee Abdul sio baba yake mzazi Diamond sababu sio rahisi mtoto alelewe na baba wa kambo mpaka abadilishe jina la ubin wake pia na kuwapa mpaka watoto zake jina la babu yao feki walitumia kama babu yao.

Hizi ni faulo zinataka kuchezeka hapa Mama Diamond anataka kumaliza mechi.

ina maana maza ake DAi alikuwa anakit**** mpaka anashindwa jua baba wa mwanae?
 
OMG! OMG! OMG! OMG! Hivi unajua kwanini nimeweka hizo OMG nyingi?! Kwanza ndo unanijuza kwamba Nyange ni Waluguru! Pili, nakumbuka kuna siku Diamond kulikuwa na event fulani hivi Morogoro akasema "hapa ni home" lakini watu hawakutilia maanani!!!
Ndio hivyo naona hata Sallam Sk amemtania leo.
 
Wangeacha kumpa lawama za malezi wakati wanajua sio damu yake

Sakata la FA na baba yake ni tofauti na la domo. FA hajawahi kuleta ukaribu na mzee wake ila huyu wa wasafi keshamtumia sana mzee kwenye kiki zake wakati anafahamu sio baba yake.

Wangeweka wazi tangu mwanzo
Sana huyu yeye angekula buyu kama mzee wake Mwana Fa.

Mzee wake Mwana Fa kuna picha yake kapiga,yupo bar anakula nyagi alafu anaonekana hana time kabisa yani na yeye mwenyewe alivyo hojiwa wala hajutii.
 
Kwa hiyo mzee Abdul alikuwa anateleza ,so Diamond ni mluguru wa Morogoro na si mmanyema.

Mzee Abdul alikua anatelezaaa, ila aligoma kutoa huduma

Halafu kuna dogo alisoma na Queen Darleen walikua marafiki sana, baada ya Diamond kuja kuwa maarufu na kumjua kama kaka wa Queen akawa anasema ilikua huyu mzee akatae kumsomesha Nasib wakati alikua anampa Queen pesa na good time kiasi kwamba Queen alikua DonMtoto pale kariakoo?!!

Kumbe mzee alikua na mapesa tuu lakini aligoma kabisa kumsaidia Nasib na sasa Nasib ana pesa yeye analalama kila siku hapati huduma

Mama Diamond kachoka kaamua kutema nyongo💣💣
 
Wangeacha kumpa lawama za malezi wakati wanajua sio damu yake

Sakata la FA na baba yake ni tofauti na la domo. FA hajawahi kuleta ukaribu na mzee wake ila huyu wa wasafi keshamtumia sana mzee kwenye kiki zake wakati anafahamu sio baba yake.

Diamond hajawahi kumtumia huyu mzee kwa kiki,bali Shigongo ndiye kamuibua na kauza sana magazeti kwa kupitia huyu mzee.We mzee mwenyewe kila siku yupo kwenye kamera ,anahojiwa tu hajui anawatengenezea wenzake hela YouTube.Nilishamshangaa mpaka
global walitengeneza kiki na yule Dada wa London kujifanya mwanae,aje ampatanishe na Diamond kume yule mdada alikuwa anatafuta umaarufu nikamwona hana maana.

Yeye angekaza kutafuta hela awatunze watoto wake wa uzeeni huko kishakataliwa achane na hivi vitu.
Wangeweka wazi tangu mwanzo
 
Dar es Salaam. Sanura Kassim maarufu mama Dangote ambaye ni mama mzazi wa msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz amesema baba halisi wa mwanaye ni Salum Iddi Nyange na si Abdul Juma ambaye kwa miaka mingi amekuwa akifahamika kama baba wa mkali huyo wa Bongofleva.

Mama Dangote ameeleza hayo leo Ijumaa Januari 15, 2021 baada ya kupigiwa simu na Dida, mtangazaji wa kipindi cha Mashamsham kinachorushwa na redio ya Wasafi kueleza kuhusu uhusiano kati ya Diamond na Ricardo Momo aliyekuwa akihojiwa na redio hiyo.

Katika majibu yake, mama Dangote amesema Ricardo na Diamond ni ndugu na baba yao ni Nyange ambaye kwa sasa ni marehemu.
Akizungumza na Mwananchi Digital baada ya kumalizika kwa mahojiano hayo, Abdul amesema amefurahi kusikia jambo hilo akidai kuwa hata yeye alikuwa hajielewi wala kujitambua.

“Nadhani mhusika ameshazungumza sawasawa kabisa,” amesema Abdul na alipoulizwa sababu za kutoweka wazi jambo hilo amesema, “si mmeshapata jibu kwa mwenyewe mnataka mimi niseme nini tena wakati yeye ndio aliyebeba mimba.”
 
Back
Top Bottom