Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

Mama mwenye hali ngumu anakaa na binti mdogo mjamzito ambaye sio ndugu yake

Aiseee huyo jamaa yako ana roho ya ibilisi kabisa
mkuu hilo ni tukio moja, nikieleza hapa huwez amini jamaa ana roho mbaya mnooo.
ila yeye sasa anapenda saidiwa balaa, mtaa anao kaa hakuna mtu anapatana nae. ofisini ni mtu mkubwa tu ila akijua haumkubali ama una urafiki na mtu asiye mkubali basi anakupiga zengwe ufukuzwe

kifupi jamaa ana roho mbaya sana
 
roho nzuri ama mbaya ni mtu kuzaliwa nayo

nna mshikaji wangu ana roho mbaya ana roho ya uchoyo hata yeye analijua hilo

kuna siku tumekaa analaumu kwa nini mtoto wake wa kwanza ni me hana roho ya mbaya (uchungu na kitu chake )

anamfurahia mtoto wake wa kike kumfata roho ya uchoyo (yeye anaita uchungu na kitu chake)
Duuh mkuu, hii mbona ni balaa sasa??
 
Hawajali hilo na nadhani pia wapo sahihi!, kuna raha gani kumalizia uzee na drip za insulin pamoja na madawa ya presha wakati mzaramo anapiga chai chapati hadi anaingia kaburini
Tunayachukulia maisha seriously sana lakini mwishoni impact yake ni magonjwa ya gharama
A sad truth
 
A sad truth kongole mkuu
 
Mambo vp wadau??

Ninaomba radhi kwa uandishi m-bovu.

Kuna mama mmoja yeye ni mzaramo. Ni mama mkaanga Samaki amepanga chumba na sebule huku mtaani kwetu (Kodi Jumla 30,000/= kwa mwezi). Huyu mama muwewe alifariki kama mwaka na nusu hivi umepita. Sasa kulikuwa na Binti mmoja alibeba ujauzito hapa mtaani, huyo Binti hana baba wala mama (umri kama miaka 16 au 17 hivi).

Huyu Binti ni Mnyakyusa wa Mbeya wazazi wake wote walifariki katika vipindi tofauti tofauti ila wa mwisho kufa alikuwa ni mama yake mzazi.

Sasa cha kushangaza huyu mama muuza Samaki, ambaye anaishi maisha magumu mno (faida ya Samaki labda ni 10,000 tu kwa siku) ameamua kumchukua huyu binti anakaa naye hapo alipopanga ilhali hana hata undugu naye.

Wanapika, wanakula, jioni wanaenda kuuza Samaki zao za kukaanga barabarani, huyu dada akiwa na tumbo la ujauzito.

Hii roho ya huyu mama mkaanga dagaa mpaka ninaogopa kwa maana katika hali ya kawaida watu wengi wenye vipato vidogo wanaogopa mizigo zaidi, lakini huyu mama kamchukua huyu Binti anakaa naye kama vile ndugu yake. Hivi wakuu, roho kama hizi huwa mtu anazaliwa nazo au inakuwaje??

Watu wa Pwani (Wazaramo, Wandengereko,n.k) Mwenyezi Mungu awabariki sana.

NB: Mimi ni kabila la mkoa wa Mara..
Wazaramo wakarimu sana ila hao wandengereko sidhani kama upo sahihi.
 
mkuu hilo ni tukio moja, nikieleza hapa huwez amini jamaa ana roho mbaya mnooo.
ila yeye sasa anapenda saidiwa balaa, mtaa anao kaa hakuna mtu anapatana nae. ofisini ni mtu mkubwa tu ila akijua haumkubali ama una urafiki na mtu asiye mkubali basi anakupiga zengwe ufukuzwe

kifupi jamaa ana roho mbaya sana
Aisee hiyo ni ibilisi.
Sio mpare huyo mtu?
 
Mkuu, may you please elaborate this more??
Yes , I can elaborate it .
Yesu alitoa mifano mingi.
Mmoja alisema wazinzi na walevi watawatangulia kuingia kwenye ufalme wa mbinguni alimaanisha kuwa kuacha tabia ya uzinzi na ulevi haitoshi kukudanya uingie mbinguni ikiwa moyo wako huwaza mabaya juu ya mwingine, au ikiwa huleti furaha katika maisha ya mtu mwingine.
Kuhusu haki yenu isipozidi haki ya Mafarisayo hamtairithi mbingu maana yake ni kwamba watu wa Mungu wanapaswa kuwa na moyo safi na matendo safi zaidi kuliko watu wa dini.
Yaani you should do more than religious people they do.
 
Back
Top Bottom