Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae

LEO NDIYO NIMEAMINI WAANDISHI WA HABARI BONGO NI VITUKO...YAANI KIKONGWE WA 81 NAYE ANAITISHA PRESS conference NANYI haraka mnamkimbizia mic , Mimi siyo mwana habari ila nadhani kuna pahala mnafeli sanaaaa
Pole sana mkuu,maana wasukuma hamtaki vikongwe ndiyo maana mnawakata mapanga ila wanyambo/ Wahaya awana huo utamaduni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezikuta jamii za watu walioelimika na kustaarabika mambo haya.
Nikweli uwezi kusikia mwananchi wa marekani, ujerumani, England, wakitukana serikali zao na nchi zao kwenye vyombo vya habari vya Russian, Iran, China, Korea kaskazin.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwaamini wanasiasa ni kujipalia makaa, sisi hapa jf ni wafauata upepo tu ndio maana hapa watu walishupalia weeee lkn sasa hatuoni tena zile kelele
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka siku Kabendera amepelekwa mahakamani na Zito akaenda kutaka kukaa pembeni yake kwenye benchi, kama vile nafasi haikutosha Zito akahamia benchi LA pembeni kuna jamaa tuliekuwa nae alisema Zito anamponza huyo jamaa.
Ile kauli sikuitilia maanani lakini badae niliielewa vizuri na ninazidi kuelewa, hawa watu ndio waliomponza na sasa anasota wao wanapiga mluzi tu mtaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku baada ya kutoka kwenye madaraka mkuu wenu yatamkuta mambo na kila mtu hata aliyekuwa mpambe wake wa karibu atamkimbia na atachekwa na kila mtu hadi waliojifanya washkaji wake.
Time will tell.
 
Mr perfect.
Uliyefunzwa vizuri. Hongera sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku baada ya kutoka kwenye madaraka mkuu wenu yatamkuta mambo na kila mtu hata aliyekuwa mpambe wake wa karibu atamkimbia na atachekwa na kila mtu hadi waliojifanya washkaji wake.
Time will tell.
Kwa mfumo wa uongozi wa Serikali hapa Tanzania hayo unayoyaombea hayatatokea kamwe, niseme tu sahau hizo ndoto zako. Kama unafahamu wakati wa machafuko Zanzibar na DSM (mwembechai) kuna watu walisema Mkapa akitoka madarakani atapata tabu sana mara atapelekwa ICC na maneno mengi, lakini mpaka sasa hivi anakula mafao yake na hakuna wa kumgusa so ht kwa huyo unayemzungumzia itakuwa hivyo hivyo, kwa Tanzania sahau mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mashitaka yoote yanayomkabili kabendela ni matokeo ya ukaribu aliokuwa nao kwa marehemu Rwajabe hayo mengine ni kupotezea mda tu, Kabendera anaweza akawa anatumika ili hali wahusika wanajificha kwenye tukio ambalo huenda wanajua wakimwacha kabendera akiwa huru atalimwaga na watu watajua hata kama wanajua lakini pasiwepo wa kulielezea , kumbukeni yuko wapi Azory na story za Mkiru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla hujafa hujaumbika , hivi kama kweli Kabendera ni mtakatisha pesa huyu mama angelia namna hii ? endeleeni na ukatiri wenu lakini mtakuja kulipa tu
Mama hawezi jua mishe zote za mtoto wake. Kama kabendera hana kosa naunga mkono aachiwe ila kama ana makosa hakuna wa kumsaidia hata mama alie vipi haisaidii kitu.
 
Wapi Gadafi, wapi Saddam, wapi Hitler, wapi Mugabe? Ukijiuliza hawa wote wako wapi basi utaelewa kuwa mambo ya dunia ni ya kupita na kwa haraka sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah umeugusa moyo wangu! Kinachoniuma wale wote waliokuwa wanashirikiana nae wamekaa pembeni anapata tabu peke yake,

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa mkuu, hasa mama anasema Erick alikuwa anafanya kazi zake nyumbani hadi saa saba za usiku! Bila shaka hizo kazi ndio zile Makala alizokuwa anazi leta Pasco humu kila siku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…