Mama mzazi wa Martha Mwaipaja alia kwa uchungu, akithibitisha kuwa mwanae huyo hamsaidii kutokana na mzozo na mdogo wake Beatrice

Mama mzazi wa Martha Mwaipaja alia kwa uchungu, akithibitisha kuwa mwanae huyo hamsaidii kutokana na mzozo na mdogo wake Beatrice

Tutasikia mengi wakati huu, mwaka unaisha kwa kiki.
Lol
 
Mwenye picha ya Joan tafadhali! Binti yatima anayeishi na Martha Mwaipaja! Binti anayeaminika na kusikilizwa kwa kila kitu na Martha Mwaipaja! Binti anayeaminika kuwa chanzo kikuu cha hili sakata.

Picha yake tafadhali....!
Screenshot_20241219-212749.png
 
Mama mzazi wa Martha Mwaipaja amezungumza na kuthibitisha kuwa yale yaliyosemwa na mdogo wake, Beatrice Mwaipaja kuwa muimbaji huyo wa 'Hatufanani' hamsaidii.

Akizungumza kwa uchungu kwenye mahojiano na Wemu Online TV, Mama huyo amesema alizaa watoto watatu wakiwemo Martha na Beatrice wanaopishana miaka 2 ambapo mtoto wa kwanza alifariki dunia. Mume wake, baba yao Martha na Beatrice alifariki 1995.

Anasema hadi sasa ana wajukuu wanne tu, mtoto wa Martha ambaye ni wa kiume aliyezaa na aliyekuwa mume wake, watoto wawili wa Beatrice, na mmoja aliyeachwa na marehemu mwanae wa kwanza.

Pia, Soma: Beatrice Mdogo wa Martha Mwaipaja aanika mabaya ya dada yake kwamba ana fedha nyingi lakini hamsaidii mama yake

Amesema, Joan alienda kwa Martha kama mfanyakazi wa ndani na kwamba alimweleza kuwa ni mtoto yatima anayehitaji msaada. Mama huyo amedai kuwa kwa sasa Joan ndiye anayeamua kila kitu katika maisha ya Martha na kwamba yeye ndiye amekuwa akimzuia asimsaidie.

Ameeleza kuwa hata mjukuu wake, mtoto wa kuzaa wa Martha naye amekuwa akiishi maisha yasiyo na furaha. "Yule mtoto (Joan) ndiye ambaye ametanda pale sebuleni," ameeleza Mama Martha kwenye mahojiano hayo.

"Mtoto wangu mpaka ninamuita 'Martha hebu njoo umuangalie mtoto huku jua linampiga halafu ninyi mmekaa sebuleni, hujui' alikuja tu akashika tu kidevu akaangalia mwanangu, akaondoka. Mtoto yule hana raha na mama yake."

Mama huyo anasema amefanya kila awezalo lakini amemshindwa Joan. "Mimi kama mimi nimemshindwa, na ndio maana Beatrice ameamua kuongea, umma umsaidie, naomba mtusaidie," ameeleza.

Anasema Martha na Beatrice wameanza kugombana mara baada tu Joan alipoingia kwenye maisha ya Martha.

"Kwasababu [Joan] ameoana kwamba Beatrice anaufahamu kwamba huyu ndiye anamchanganya dada yake, kwahiyo akiangaza kuongea, huyu binti ndipo anaanza kugeuza maneno na kumpandikizia roho ya kwamba mdogo wako hakupendi."
View attachment 3180128
Martha anajitafutia laana bure, machozi ya mzazi sio mchezo. Mungu amsaidie sana.
 
Kweli dada mdogo na mama walikuwa sahihi kusema Martha anampenda Sister Joan kuliko mtoto wake pekee wa kumzaa mwenyewe! Achilia mbali mama na mdogo wake. Yaani hiyo picha inaonesha those two people are in deep love! 👩‍❤️‍👩
Hawa wanaoita Mungu Mungu! Siku ya mwisho wengi watakua kwa shetani
 
Kila familia ina matatizo,acheni kuwa wasemaji. Hawa watakuja kupatana yawashuke..
 
Hawataki kusema kiini cha tatizo. Ukweli ni kwamba huyo Joan ndio mume wa Martha anamsugua rosecoco yake hao ni malesbian Joan ndiye anayeamua kila kitu sababu yeye ndio mume. That mwimbaji ni just another daudghter of satan ndio maana hawezi hata kumjali mtoto wala ndugu zake. Saitani mkubwa.
 
1)SI LAZIMA mtoto amsaidie mzazi wake.Wala si kosa kisheria mtoto asipomsaidia mzazi wake.
Si lazima mtoto awe rafiki na mzazi wake wapo watoto walioweka uadui na wazazi wao.

2)njia waliyoitumia ya kulalamika kwenye vyombo vya habari si ya busara,wangeweza kutumia vikao vya ukoo familia,au viongozi wa kiroho makanisa,ai njia nyingine tyoyote ya mabaraza ya usuluhishi ya kijamii.

3)mzazi amejishushia heshima mana afikirie kipindi kabla hajamzaa huyo mtoto au kabla mtoto hajakuwa na mad
fanikio aliyonayo,au kama asingekuwepo au asingekuwa na mafanikio aliyonayo...au aingekuwa hai...au akifikisika akawa fukara ..je maisha hayataendelea bila kuhitaji msaada wa mwanaye.
 
Back
Top Bottom