TANZIA Mama mzazi wa Mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019


Ngoja niwaachie Members wengine hapa waniambie Kosa langu ni lipi hasa kwa kile ambacho nimekiandika ambacho Kimekukwaza.
 
Kwani sisi ndio DPP?

Mbele za Mungu kila mtu ataubeba msalaba wake " yeye mwenyewe"
Nyinyi ni makatili wa roho za watu! Basi hilo tu! Na waliomsaidia Jiwe kutekeleza ukatili watabeba msalaba vile vile
 
RIP Mama.
Kiukweli muwe na akili kidogo tu, kila mama ya mtu akilia so mtuhumiwa aachiwe?
Acheni ufala nyinyi kabendera aenjoy tu makosa yake huko alipo.mahakama ndo itaamua kama kaonewa au kafanya makosa kweli
Ni rahisi kufurahia yanapomkuta mwenzako,hakuna mtu anasema kabendera aachiwe kwa kuwa mama yake "analia lia", kinacholeta mashaka ni aina na namna mashtaka yake yalivyoelezwa,ilionekana wazi kwamba makosa yake yanatafutizwa...

Anyway,katika yooote wanaomtesa wanaujua ukweli Kama wanamuonea au ni stahili yake kwa makosa ya uhujumu uchumi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais wa wanyonge huyu mama alikuomba umuachie mwanae kwani ndo anasimamia matibabu yake masikio ukaweka pamba....apumzike kwa amani na mwanga wa milele umuangazie
Ujuha wa watanzania wanadhani kuwa Rais ana mamlaka katika kila kitu. Na hii inasababishwa na wanasiasa wanaopenda kupotosha umma. Rais amuachie kwani yeye ndiye aliyemkamata? Tangu lini Rais akaiamrisha mahakama imuachie mtuhumiwa? Badala ya kwenda mahakamani kudai haki ya mtoto wenu mnakimbilia kumwambia rais amuachie. Mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kumuachia mtuhumiwa na siyo Rais.
 
Mahakama ndo iliyomkamata,? Halafu na wewe unajiita njuaji??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio machawi hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
So sad,pumzika kwa amani mama.Pole kwa WAFIWA WOTE,NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.
 
RIP mamaa.
Napata tabu kidogo hapa. Hivi mtuhumiwa yoyote anaweza kuachiwa kabla mahakama haijadhibitishwa mashitaka juu yake kisa ana mgonjwa, watoto au majukumu fulani? ( wajuzi wa sheria mtusaidie).
Endapo kasingiziwa na mtu kwakweli tutupe lawama ila vinginevyo uwezo wetu wa kufikiri ni shiiida tulio wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…