Uchaguzi 2020 Mama Salma Kikwete achukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea jimbo la Mchinga kupitia CCM

Uchaguzi 2020 Mama Salma Kikwete achukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea jimbo la Mchinga kupitia CCM

Sina chuki na mama lakini ukweli lazima usemwe, akichaguliwa yeye ni upotevu wa nafasi bure tu.

Mama angeweza kufanya mambo mengine na mataasisi yao akaachia wengine hiyo nafasi ya bungeni.

Kwanza yeye na mumewe wote wanapata huduma za serikali vizuri tu hana njaa ya pesa.

Kama anajiona bado kijana hapendi kukaa hivi hivi angejikita hata kwenye miradi ya kilimo na ufugaji ya familia. Watu wenye mitaji na mitandao (Business network connections) kama hawa ndio hufaa kuonesha mfano wa kufanya biashara kubwa za kusafirisha nje bidhaa au mazao ya kilimo na ufugaji kwenda nje ya nchi. Huko atazalisha ajira nyingi sana.
Siasa awaachie wanawe akina Ridhiwan a.k.a Riz-moko (Riz1).

Ushauri mzuri sana sana!!
 
Huyu hata kupiga kampeni ni kupoteza muda na pesa tu bure
 
Huyu mama jina lake halirudi trust me kashafeli mpaka hapo atakatwa juu kwa juu.kwanza alikutwa na sakata la rushwa mara mbili.ni bora angegombea lindi mjini.nahisi ndoa yao itakuwa na tatizo sehem sitaki kuamini mzee wangu kikwete kampa go ahead.au bimkubwa kwa jeuri yake kaamua kupambana mwenyewe, kumdhirishia mumewe hata bila yeye anaweza.all in all hakubaliki huko anakogombea alikuwa na mda mwingi wa kuwasaidia wana lindi na hakufanya hivo.
 
Anaweza kukatwa na hamna kitu mtafanya,kwani si alishawahi kumwambia Mumewe anawashwa washwa?

Kwa sasa Mwenye Chama ni mmoja tu,wengine wote wameshatwa mkia na cha kufanya hakuna.
Na kwa taarifa mwaka 2015 alipigwa kwenye kura za maoni lindi mjini
 
Mama kama hakuweza kuitumia ipasavyo nafasi ya u-first lady kutoa mchango wake kwa mama Tanzania ktk kipindi hicho, kwa sasa uharibifu wa nafasi ya ubunge na kuongeza tatizo la ukosefu wa ajira. Nashauri wanamchinga wampige chini kwenye sanduku la kura!
Anapigwa mapema sana mzee nipo lindi huku nimekuja kikazi huyu mama akipita kura za maoni basi yale yote anayofanya rais magufuli ni ya uongo.magu yupo siriaz sana mwaka huu.takukuru wanafanya kazi yao vzr kabisa.
 
FB_IMG_1594843402999.jpg


Tutapambana na wewe jukwaani bila kukuonea aibu , kwahiyo ujitayarishe kwa madongo yasiyo ogopa kofia ya Mzee , tunapopambana na mwanaccm yeyote huwa hatubagui .

ulishakuwa First lady na ukaanzisha mfuko wa WAMA , hatujasahau kitu mama yangu , yako maswali kadhaa utajibu upende usipende , aliyekushauri uingie majukwaani kakuchuuza sana , sisi tunakusubiri kwa hamu

Usije kusema hatukukuambia.
 
Back
Top Bottom