Uchaguzi 2020 Mama Salma Kikwete achukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea jimbo la Mchinga kupitia CCM

Uchaguzi 2020 Mama Salma Kikwete achukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea jimbo la Mchinga kupitia CCM

Salma Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Mchinga mkoani Lindi kupita Chama cha Mapinduzi (CCM).

Huyu mama angetulia tu nyumbani na Rais Mstaafu Jakaya ingetosha, ameshakaa ikulu kama First Lady kwa miaka 10 na hatimaye kama mbunge wa kuteuliwa kwa miaka mitano. Ridhiwani anatosha kuweka alama ktk familia sasa ktk familia.
 
Anajiona Hillary Clinton wakati uwezo ni mdogo sana. Wacha wampitishe tutamgalagaza ili akapumzike vuzuri na aibu yake. Jimbo la Mchinga wimbo wetu wa kampeni ni ule wa Babu, wa Salma.
 
Sina chuki na mama lakini ukweli lazima usemwe, akichaguliwa yeye ni upotevu wa nafasi bure tu.

Mama angeweza kufanya mambo mengine na mataasisi yao akaachia wengine hiyo nafasi ya bungeni.

Kwanza yeye na mumewe wote wanapata huduma za serikali vizuri tu hana njaa ya pesa.

Kama anajiona bado kijana hapendi kukaa hivi hivi angejikita hata kwenye miradi ya kilimo na ufugaji ya familia. Watu wenye mitaji na mitandao (Business network connections) kama hawa ndio hufaa kuonesha mfano wa kufanya biashara kubwa za kusafirirsha nje bidhaa au mazao ya kilimo na ufugaji kwenda nje ya nchi. Huko atazalisha ajira nyingi sana.
Siasa awaachie wanawe akina Ridhiwan a.k.a Riz-moko (Riz1).
Kuna watu bila vyeo vya kisiasa wanajiona hawajakamilika.

Usishangae akajifanya Hilary Clinton kutaka kugombea urais.
 
Hahah wazee watamaindi kishenzi.

Hivi mkuu kwa hio huyo mama akipita kwny mchujo mume wake(JK) atakua nae anakuja kupanda jukwaani kumnadi sio?
Bill Clinton alifanya..... si kitu ya ajabu.
 
Sina chuki na mama lakini ukweli lazima usemwe, akichaguliwa yeye ni upotevu wa nafasi bure tu.

Mama angeweza kufanya mambo mengine na mataasisi yao akaachia wengine hiyo nafasi ya bungeni.

Kwanza yeye na mumewe wote wanapata huduma za serikali vizuri tu hana njaa ya pesa.

Kama anajiona bado kijana hapendi kukaa hivi hivi angejikita hata kwenye miradi ya kilimo na ufugaji ya familia. Watu wenye mitaji na mitandao (Business network connections) kama hawa ndio hufaa kuonesha mfano wa kufanya biashara kubwa za kusafirirsha nje bidhaa au mazao ya kilimo na ufugaji kwenda nje ya nchi. Huko atazalisha ajira nyingi sana.
Siasa awaachie wanawe akina Ridhiwan a.k.a Riz-moko (Riz1).
Acha fikra potofu mkuu, watu wanaoamini mtu hutafuta nafasi ya uongozi ili kujipatia pesa hafai kuwa kiongozi.
Ina maana Hilary Clinton huko kote alikopitia kisiasa ilikuwa ni sababu ya tamaa zake za pesa?

Mama Salma ni mwanasiasa Kama wanasiasa wengine. Kikwete kuwa Rais mstaafu siyo kizuizi cha familiya yake kushiriki siasa.

Acha familiya itumie damu na uzoefu wa JK kisiasa na kiungozi kuitumikia Tanzania, ndio talanta yao.
 
Kuna watu bila vyeo vya kisiasa wanajiona hawajakamilika.

Usishangae akajifanya Hilary Clinton kutaka kugombea urais.
Kwani shida itakuwa wapi?

Kuna kipengele cha Katiba kinachomzuia?
 
Back
Top Bottom