"Niwashukuru kwamba nimeweza kusimama tumesalimiana, ninalotaka kuwahakikishia ndugu zangu, Tanzania tuko salama, Tanzania tuko salama. Ni kawaida ya mwanadamu kukaguliwa kaguliwa, mara mafua, mara homa mara chochote kile"
Maneno haya Mama yetu mbona yanaleta maswali sana, Anashukuru ameweza kusimama? Mbona hatujawai pewa taarifa yoyote kua alikua anaumwa? Au kusimama kwa namna gani? Maana hiyo ziara imeandaliwa muda maana ake alijiandaa kwa hilo.
Huyu aliyekaguliwa kaguliwa ni yupi?
Yaani Leo mama yetu kasafiri kutoka DSM ili kuja kutuhisia watanzania tuwe na umoja na kushikamana kipindi hiki. Hiki kipindi anachokisema mama yetu ni kipindi cha namna gani?
Maana huku sisi tunaendelea kujifukiza, na kushagilia nchi yetu pamoja kua dunia inakubwa na korona sisi uchumi umepanda hadi uchumi wa kati.
Leo sijamuelewa kabsa Mama Yetu