View attachment 3309107
Kukiwa na amani, hakuna mizengwe na hali ikiwa shwari kabisa, siyo siri kura zote November ni za Mama Samia kwa zaidi ya 80%.
Hizo 20% zilizobakini za wale walio na hisia zao wenyewe kwa mambo mbali mbali ambayo hapa sitajadili.
Lakini kwa mfumuko wa zengwe la Lissu kuzushiwa kesi ya "uhaini", ni wazi kuwa kwanza ni kichekesho, pili ni kama kuutaka kuzima upinzani kwa mguu wa tembo, ilihali CHADEMA yenyewe ni ubua kisiasa.
Lakini siasa ni hoja, na kwa wale wasiofikiri Tundu Lissu amechoma mkuki sehemu ambayo makada wa CCM hawajui wapi waanzie kujibu.
Makada wamepanic, na wameitumia serikali kisiasa, na moja kwa moja wanamwingiza Mama Samia chaka la kisiasa.
Ukiona hata mzee Warioba anapepesa macho na CCM yake ujue kisiasa CCM haijakaa vizuri.
Mama tunamfahamu, si mtu wa mizengwe, ila ile anayopandikizwa na "washauri" wake.
Si hulka ya mama Samia kuwaweka ndani watu wenye profile kama Lissu.
Sasa siasa ni mchezo wa maneno, ukitumia mabavu kila mtu anajua umelemewa.
Wahauri wa mama ndio waliotufikisha hapa, lakini huo sio mwisho wa mchezo.
Kujitoa hapa tulipo natoa ushauri wa bure, mama Samia watose hadharani walio kushauri vibaya, wewe ndio unabeba lawama zote.
Mama Samia , kwa wanao kufahamu Afrika , na dunia nzima , wanashangaa imekuwaje , na nini kimetokea kwa yule mamam mstahimilivu.
Waliokushauri wabebe mzigo wao wa lawama, Lissu arudi kwenye ulingo wa kisiasa.
Naamini Lissu akijibiwa hoja zake, munkari wa kisiasa utapungua.
Come November 2025, hali ikiwa njema kisiasa, kiusalama, Inshallah, mama bado wapendwa na wengi.