Mama wa watoto 8 atorokwa na mumewe, aomba msaada

K tamu
 
Inasikitisha sana, huyu jamaa aliyeitelekeza hii familia hatapata mafanikio huko alipo.
 
Inakuwaje maskini kama hiyo anazaa watoto 8, huwa anategemea nani wa kuwahudumia. Huna nyumba wala kazi ya maana lakini kutwa kuzaa. Waafrika tuna shida mahali.
Wanaamini Kila mtoto huja na riziki yake, wengine huona kama hawana mali basi angalau wawe na watoto wengi.
 
Kuna mtu aliwahi kuleta uzi humu JF kwamba haioni haja ya kuzalisha watoto wakati matunzo hana na itapelekea watoto kuteseka sana. Hoja yake ilipingwa sana na akatazamwa kwa mtazamo hasi na kumshangaa kwa nn haoni faida ya kuwa na watoto. Hapa ndio ninaamini usemi wa AKHERI NUSU SHARI KULIKO SHARI KAMILI
 
Kuna watu hawajui kutazama mazingira na kuchanganua hali ya maisha aliyonayo
 
Nimejaribu kujiuliza tu. Hivi huyo jamaa hela za kumpeleka uyo mke hospital kujifungua watoto wote hao alizipatia wapi? Na hawana makazi. Au huko vijijini watu wanajifungulia nyumbani. Au huduma za kujifungua kwa vijijin ni bure?
Kijijin kujifungua ni buree
 
Hawa ndio waliosikiliza na kufuata ushauri wa kipuuzi wa jiwe kuwa fyatueni watoto elimu ni Bure na mnapokuwa wengi mnapata maendeleo kama China na India! Mawazo ya mtu mwenye PhD eti!
Kabla ya jiwe hakuna walokua wanazaa watoto zaidi ya kumi,au ndo chuki binafsi kwa mwendazake!?
 
K
Kwa hio watu wakishazaa bila mpango ni kazi ya Waziri kwenda kuwasaidia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…