Mama wa watoto 8 atorokwa na mumewe, aomba msaada

Mama wa watoto 8 atorokwa na mumewe, aomba msaada

K tamu
Huwa nina hasira sana na wanaume wanao zalisha hovyo kama mapanya halafu kulea hawawezi.

Mijitu ya namna hii ndio inazalisha umaskini na kuongeza idadi ya maskini kuwa wengi duniani.

Na ndio maana huwa nafurahi sana watoto wa namna hii, wanao kulia katika shida hizi, wanapokuja kufanikiwa na kuwatupilia mbali hao baba zao wapumbavu na wazembe wakwepa majukumu.

Li mzazi la namna hii siku likija kukuomba msamaha wewe mtoto wake, Unamfurumusha na mabapa ya panga akafie mbali.
 
Waziri Dkt. Gwajima D kuna hii familia ya kuitazama inahitaji msaada wa kiuchumi na kijamii. Mama wa watoto nane, Belita Deus, ambaye mumewe katoroka.

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto wa Wilaya ya Malinyi, Mkaguzi wa Polisi Michael Rasha, ameguswa na hali ya mama wa watoto nane, Belita Deus (37), ambaye alitorokwa na mumewe kutokana na ugumu wa maisha.
Mkaguzi Rasha, akiwa katika jukumu lake la kutoa elimu katika kijiji na kata ya Kilosa Mpepo, Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro, alipokea ujumbe kutoka kwa mama huyo akiomba msaada wa kutafutiwa mumewe ambaye ametoroka na kumtelekeza pamoja na watoto.
Baada ya kupokea wito huo, Rasha alifika nyumbani kwa Belita na kuelezwa changamoto alizonazo baada ya mume wake kumtoroka. Ameeleza kuwa maisha yamekuwa magumu sana na anakabiliwa na tatizo la makazi, kwani anakaa kwenye kibanda alichopewa na msamaria ambaye sasa anakitaka. Pia, amekosa mahitaji muhimu kwa ajili yake na watoto wake na hawezi kuwaendeleza kielimu.
Belita amesema njia pekee inayomfanya aishi ni kufanya vibarua vya kulima na usafi kwenye nyumba za watu ili apate pesa za kusukuma maisha. Mtoto wake mkubwa ana miaka 14 na alitakiwa kuwa darasa la sita, huku mtoto mdogo akiwa na miezi mitano tu.
Mkaguzi Rasha amempatia Belita kilo 20 za unga, mche wa sabuni, na fedha kidogo ya kujikimu ili kumfariji. Hata hivyo, mama huyo anahitaji msaada zaidi kutoka kwa wasamaria wema walioguswa na hali yake.

Picha: Michael Rasha
Inasikitisha sana, huyu jamaa aliyeitelekeza hii familia hatapata mafanikio huko alipo.
 
Inakuwaje maskini kama hiyo anazaa watoto 8, huwa anategemea nani wa kuwahudumia. Huna nyumba wala kazi ya maana lakini kutwa kuzaa. Waafrika tuna shida mahali.
Wanaamini Kila mtoto huja na riziki yake, wengine huona kama hawana mali basi angalau wawe na watoto wengi.
 
Hayajawahi kunikumba.

Ila napata hasira sana kuona watoto wadogo na wachanga wasio na hatia yeyote ile wakiteseka kwa sababu ya upumbavu na uzembe wa mzazi Mpumbavu mkwepa majukumu.

Wazazi wa namna hii hawafai kabisa. Wanapaswa wahasiwe hizo kende zao.

Maana wana ongeza maskini wengine duniani tu.
Kuna mtu aliwahi kuleta uzi humu JF kwamba haioni haja ya kuzalisha watoto wakati matunzo hana na itapelekea watoto kuteseka sana. Hoja yake ilipingwa sana na akatazamwa kwa mtazamo hasi na kumshangaa kwa nn haoni faida ya kuwa na watoto. Hapa ndio ninaamini usemi wa AKHERI NUSU SHARI KULIKO SHARI KAMILI
 
Hivi mtu unapata wapi ujasiri wa kuzaa watoto zaidi ya wawili kwenye kibanda cha nyasi, chini ya maisha ya kifukara?.

Matokeo yake ndio kuja kutia huruma na kuwapa watu wengine mzigo wa kusaidia malezi. Huyu mama na huyo mume wake wamefanya jambo la kijinga sana, watoto nane hapo kwenye icho kibanda kwelii?, stupid!.
Kuna watu hawajui kutazama mazingira na kuchanganua hali ya maisha aliyonayo
 
Nimejaribu kujiuliza tu. Hivi huyo jamaa hela za kumpeleka uyo mke hospital kujifungua watoto wote hao alizipatia wapi? Na hawana makazi. Au huko vijijini watu wanajifungulia nyumbani. Au huduma za kujifungua kwa vijijin ni bure?
Kijijin kujifungua ni buree
 
Hawa ndio waliosikiliza na kufuata ushauri wa kipuuzi wa jiwe kuwa fyatueni watoto elimu ni Bure na mnapokuwa wengi mnapata maendeleo kama China na India! Mawazo ya mtu mwenye PhD eti!
Kabla ya jiwe hakuna walokua wanazaa watoto zaidi ya kumi,au ndo chuki binafsi kwa mwendazake!?
 
K
Waziri Dkt. Gwajima D kuna hii familia ya kuitazama inahitaji msaada wa kiuchumi na kijamii. Mama wa watoto nane, Belita Deus, ambaye mumewe katoroka.

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto wa Wilaya ya Malinyi, Mkaguzi wa Polisi Michael Rasha, ameguswa na hali ya mama wa watoto nane, Belita Deus (37), ambaye alitorokwa na mumewe kutokana na ugumu wa maisha.
Mkaguzi Rasha, akiwa katika jukumu lake la kutoa elimu katika kijiji na kata ya Kilosa Mpepo, Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro, alipokea ujumbe kutoka kwa mama huyo akiomba msaada wa kutafutiwa mumewe ambaye ametoroka na kumtelekeza pamoja na watoto.
Baada ya kupokea wito huo, Rasha alifika nyumbani kwa Belita na kuelezwa changamoto alizonazo baada ya mume wake kumtoroka. Ameeleza kuwa maisha yamekuwa magumu sana na anakabiliwa na tatizo la makazi, kwani anakaa kwenye kibanda alichopewa na msamaria ambaye sasa anakitaka. Pia, amekosa mahitaji muhimu kwa ajili yake na watoto wake na hawezi kuwaendeleza kielimu.
Belita amesema njia pekee inayomfanya aishi ni kufanya vibarua vya kulima na usafi kwenye nyumba za watu ili apate pesa za kusukuma maisha. Mtoto wake mkubwa ana miaka 14 na alitakiwa kuwa darasa la sita, huku mtoto mdogo akiwa na miezi mitano tu.
Mkaguzi Rasha amempatia Belita kilo 20 za unga, mche wa sabuni, na fedha kidogo ya kujikimu ili kumfariji. Hata hivyo, mama huyo anahitaji msaada zaidi kutoka kwa wasamaria wema walioguswa na hali yake.

Picha: Michael Rasha
Kwa hio watu wakishazaa bila mpango ni kazi ya Waziri kwenda kuwasaidia?
 
Back
Top Bottom