Balqior
JF-Expert Member
- Jun 8, 2021
- 2,406
- 8,039
Mama yangu angenitoa na kunitupilia mbali kipindi bado niko kwenye tumbo lake la uzazi, ingekuwa ni faida kubwa sana kwangu, ningejihesabia mwenye bahati sana, sababu nisingekuwa na haja ya kuja Duniani na kupitia mateso, usaliti, hofu, Karaha za kila namna, magonjwa, e.t.c kisha mwisho wa siku dini zinakwambia ukiteleza kidogo kwenye dhambi unaenda kuchomeka motoni milele baada ya kufa.
Kutokana na maisha na majaribu tunayopitia hapa Duniani, sisi binadamu uwezekano wa kwenda motoni baada ya kifo ni mkubwa kuliko kwenda mbinguni. Hii Dunia sio nzuri kabisaaaa, kiuhalisia ni mbaya mno na inatisha sana.
Kungekuwa na uchaguzi wa kuja Duniani au kutokuja duniani kabla ya kuzaliwa, mimi ningekataa katu katu kabisa kuja Duniani.
Najiuliza Mungu anafaidika nini kwa kutuumba sisi binadamu? Alivyotuumba amefaidika nini, na asingetuumba angepungukiwa nini? Yeye si muweza wa yote, amejikamilisha kwa kila kitu? Anatuhitaji sisi binadamu kwa ajili gani? Je, anafurahi sana kuona binadamu kila siku tunavyomkasirisha kwa dhambi, tunavyoteseka na tunavyorukaruka na sarakasi za hapa Duniani?
NB: Sina mawazo ya kujiua, na kwa sasa sina shida kubwa sana ninazopitia, maana kutokana na hii post kuna wengine watafikiria nitachukua maamuzi hayo ya kujiua, wengine watafikiria sasa hivi nina matatizo makubwa sana napitia ndio maana nimeandika hii post, la hasha, siwezi jiua maana najua ntakakoenda baada ya kujiua ni kubaya zaidi ya hapa Duniani. Mimi nimewaza tu.