CHAPTER 10
kumbuka aunty alikuwa na matatizo ya pressure na mashetani kuna siku mmoja akapandisha ikabidi tumpeleke kwa sheikh mmoja hivi ambae ni jirani yetu mitaa ya kigogo hapo.
yule sheikh alikuwa na tatizo mmoja anasoma soma madua yake weeeeeh alafu anatulia hivi kama anazima nadhani yale madudu yake yalikuwa yanamtuliza hivi.
sasa baada ya aunty kutulia lakini kalala hapo tumemfunika na kanga na sheikh kukaa sawa uncle si akaanzisha mada kuwa kuna sehemu yeye anaijua na kuna mada kazisikia kuna shimo linatoa madini.
ila hiyo sehemu ipo Mkoa X ndani ndani huko, sheikh akaingilia mada akasema yeye hiyo ndoto kashawahi kuiota kuwa kaongozana na watu wawili waenda kufata madini sehemu lakini yeye hajui ni sehemu gani wala sura za ao watu usingizini hakuzijua ni za kina nani ila alikuwa anaongea nao ila sura zao hakuzijua ni za kina nani.
INAENDELEAAAA....
Mada hiyo ikafa tukamchukua aunty tukarudi nae nyumbani. lakini yoyote ya yote ile mada pale kuwa kuna sehemu kuna madini kila mtu ilimchanganya akili hivi.
kwa maelezo ya mjomba kuwa huyo mtu wa kwanza kupata ayo madini alikuwa anachimba shimo la choo. dakika ya mwisho akakutana na kitu kama kigae hivi.
so aliingia hofu ila akampa mtu ambae anaenda mjini akaulizie ni nini kile kitu kwa masonara baada ya kufika mjini sasa yule jamaa aliyetumwa akaanimbiwa kweli yale ni madini.
kwahiyo akarudi kijijini tena akamshitua jamaa wakabeba na kigae kingine wakaenda kuuza mjini now jamaa ni tajiri mkubwa tu Dar es salaam.
na habari ikatapakaa kuwa sehemu fulani kuna mali habari nzuri utembea haraka serikali ikapata taarifa kwahiyo watu wakapigwa marufuku hata kusogea lile eneo lakini ndio kijijini ndani ndani uko.
hiyo story mwanzo kabisa mimi mwenyewe sikuiamini amini hivi niliona kama mjomba anatufunga kamba ila baada ya kujikuta nina shida ya pesa ya ada ya kwenda chuo na fursa nilipewa pesa ikaisha kwa jimama.
nikaona acha na mimi nijitoe sadaka tu. so siku kama ya jumamosi mimi mjomba na yule ostadh tukatoka zetu dar es salaam mpaka mkoa X tulifika kule kama mida ya saa 11 jioni hivi.
ila mjomba alitoa wazo kuwa tukae pale stand kwanza kila mtu amalize aja yake kabisa mwenye kutaka kula akale mwenye kujisaidia na pia kila mtu anunue maji yake hajisaidie hapo kila mtu mgongon ana jembe lila bila mpini sururu, panga na torch.
maana safari ya kwenda uko kwenye hilo shimo hakuna magari usafiri pekee ambae unaweza kumfikisha mtu uko ni bodaboda ila kwa vile tunaends kufanya inshu za magendo itabidi twende kwa miguu tu hakuna kuchukua bodaboda.
tukaa pale stand saa 1 tukaanza kuupiga mguu sasa kuelekea uko kijijini. uko tulipokuwa tunaenda ni mbali sana yani tulikuwa tunapiga story njiani mpaka ikafikia hatua sasa kila mtu akabaki kimya. ila safari ilichukua kama mda wa masaa manne hivi mpaka tunafika kule kijijini.
tukafika ikabidi kwanza tupumzke kama dakika kadhaa alafu tutafute miti kwa ajili ya kutengeneza mipini ya jembe.
ili iwe inatusaidia wakati tunachimba lile shimo uwenda na sisi tukabahatika kupata japo kipande cha kigae cha dini tuje mjini kula kiki kwa mrija.
tukapata miti ya mipini fresh kumbuka tupo kijijini lakini porini sana na hiyo ilikuwa kama mida ya saa 5 usiku hivi.
kijijini kimetulia na nyumba moja ipo hapo nyingine ipo mbali sana kama kilometres mbili hivi hadi tatu.
ostadh akatoa wazo kuwa kabla hatujaingia mule shimoni kuanza kazi lisomwe dua maana mara nyingi mambo ya mali mali majini nao hawachezi mbali anaweza akaingia mtu shimoni likamvaa jinu ikawa mtihani sasa na kule ni porini hakuna msaada wa mtu.
vuta picha kutoka hapo mpaka stand kwa miguu ni masaa manne sasa unadhani itakuwaje au nani ataweza kumbeba mtu masaa yote yao sindo munajuikuta mpaka asubuhi mupo njiani tu wana kijiji wanakuja kuwakamata kirahisi.
ostadh akapiga visomo vyake soma soma somaaaa weeeeh. dakika ya mwisho tukamuona kazima katulia tuli tukajua mambo teyali sasa sisi wawili mimi na mjomba tuzame shimoni moja aende chini mwengine akae juu kucheck usalama.
daaah hatari katika lile eneo tulikutana na mauza uza ya ushirikina na uchawi hatari. pale wakati tunachimba kuna mda tunasikia kama sauti za watu hivi wanakuja kwahiyo fast sana tunatoka tunaenda kujificha alafu ukichungulia hakuna watu wala nini.
mukienda tena kinatokea kituko kingine mara musikie kama mwanamke analia hivi yani sauti fulani hivi kama mwanamke kapigwa alafu analia.
yani tulichimba kidogo tu tukaona hapa pazito tuondokue haraka sana.
Tuliondoka lakini mipango yetu tukae siku kadhaa turudi tena kule kijiji kujaribu bahati yetu kwa round ya pili.
Daaah hii round ya pili ndo ilikuwa ngumu zaidi kuliko ile ya kwanza.
Gusa hapa kupata muendelezo ππππ
Post in thread 'Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike' Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike